Salaam wakuu!
Naomba kufahamishwa hii sehemu ya nyumba ambayo haijafutwa (chumba na choo chake, sebule na dinning) inaweza kuhitaji tofali ngapi kwa ajili ya msingi tu. Tuchukulie eneo la ujenzi ni flat.
Natanguliza shukrani.
View attachment 2373766
Makadirio ya tofali za msingi;
1. Ramani yako ina jumla ya mita 60.5
2. Kina mita inajengwa na tofali 2.1
3. Hivyo mita 60.5x tofali 2.1 kwa kila mita=tofali 127 kwa laini moja.
4. Ikiwa msingi wako utakuwa na laini 7;
127×7=890.
Kwanini laini 7;
A) Mara nyingi nyumba ya kawaida huchimbwa msingi wa kina cha 50cm kwenda chini
B) ikiwa kina 50cm...blinding/zege nyembamba kabla ya kulaza tofali ni unene wa inch 2=5cm.
Hivyo kina cha 50cm-5cm 45.
C) kina cha 45cm kilichobali zitaingia laino 3 za tofali=127×3=381
D) baada ya laini tatu ambazo zitaishia level/usawa wa ardhi, laini zingi 4 zitakuwa juu ya ardhi sawa 60cm kwenda jui kutoka usawa wa ardhi.
127×4=508
E) Chukua 381+508=889
Msingi wako itakuwa na tofali 890.
Itajengwa na saruji/cement kiasi gani?
Kwa kawaoda tofali za msingi ni saizi ya unene wa inch 6 na hujengwa kwa kulaza tofali.
Mfuko mmoja wa cement hujenga tofali 30 hadi 35
Hivyo 890÷35=26
Note: Tofali zaweza kuengezeka au kupungua kidogo...kadhalika cement