Ujenzi barabara ya Mwenge - Morocco washika kasi Tigo HQ parking hali tete, hongera mbunge Mdee kwa kusimamia ilani ya CCM

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,012
142,044
Kiukweli mabadilko makubwa yameanza kuonekana na hasa kuanzia Mwenge hadi Bamaga. Nadhani pale zinajengwa njia 8 maana jengo la Nakiete limenusa barabara kabisa.

Pale Tigo HQ makumbusho ndio hakuna parking ya magari kabisa barabara iko jirani na ngazi za kuingilia mjengoni. Binafsi nafurahishwa sana na maendeleo haya.

Pongezi ziwaendee Rais Magufuli, waziri wa ujenzi mh Kamwele, RC Makonda na mbunge Mtulia na Halima Mdee kwa usimamizi na utekelezaji mzuri wa ilani ya CCM.

Maendeleo hayana vyama!
 
Ukifika mwenge kwenda tegeta foleni, ukifika moroko kwenda posta foleni sasa sijui inawawahisha watu wapi hii barabara..
 
Mabafiliko=mabadiliko
Hafi=hadi
Jengi=jengo


Acha pupa,kaa utulie ueleweke
 
Hiyo barabara haina maana,, inaleta umasikini.hizo hera wangewej=ka fly over Mwenge na Morocco kungekuwa hakuna foleni
Picha iko wapi?
 
Katika suala la miundombinu, Magufuli ni wakupigiwa mfano barani Afrika kwa sasa. Hapo nampa "kudos" Rais wangu. Kweli kabisa anajitahidi mno maeneo mengi, tena yenye kuonekana kwa dhahiri kabisa. Nahisi hii itakuwa kete yake muhimu itakayo mpambanua kipekee kuelekea chaguzi za 2019 na 2020.
 
mabafiliko=mabadiliko
 
Mwenge hafi Bamaga ?!
 
mabafiliko!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…