Ujasusi ni pembe isiyo na nyuzi

IKWETA KONZO M

JF-Expert Member
Oct 3, 2013
716
1,000
Na. Robert Heriel.

Hata sasa hatukuoni lakini wewe watuona. Wala hatusikii usemapo lakini wewe watusikia. Wayajua mawazo yetu lakini sisi hatujui watuwazia nini. Twakuona upo mbali lakini wewe watuona tupo karibu. Hata tukisema tuje kwako tutatumia siku nyingi lakini wewe ujapo kwetu ni kufumba na kufumbua. Umekaa kwenye pembe iliyokosa Nyuzi.

Nami ni kijana mdogo tuu. Nisiyejua mambo mengi. Nimejitaabisha kwa mambo yasiyo na faida naam nimetaka kujua pembe isiyo na nyuzi.

Basi sasa nisikieni enyi ndugu zangu. Kwa maana yeye atuonaye hatumuoni. Tena yeye asemaye ingawa hatumsikii. Basi leo niseme jambo hata kama ni dogo halikosi kuwa na manufaa.

Basi nikachukua kitabu cha Mwanzo nikakisoma katika aya ya kwanza na ile ya pili. Hapo ndipo nikaiona ile pembe isiyo na nyuzi. Pembe kuu iliyoidondosha dunia.

Katika simulizi ile ya kitabu cha mwanzo. Hapo ndipo chanzo cha ujasusi kilipoanzia. Hadithi ya uumbaji wa Ulimwengu. Imenifanya niione pembe kuu isiyo na nyuzi.

Sura ya Kwanza mpaka Sura ya tatu katika kitabu cha Mwanzo kwenye Biblia. Tunaona wahusika wafuatao, ADAMU, HAWA/EVA, NYOKA,na MUNGU. Mhusika Mkuu ni Adamu, Mhusika Msaidizi ni Mungu ambaye kitabu hicho kinamueleza kama ndiye Aliyemuweka Adamu kwenye Bustani. Tunasema Adamu ndiye Mhusika Mkuu kwa sababu kisa kinamhusu yeye na uzao wake.

Mwanzo Tatu aya ya kwanza kwa mara ya kwanza Sanaa ya Ujasusi inazaliwa duniani. Tunamuona Mhusika Nyoka Akifanya ukachero Kwa Hawa. Aya ya kwanza inanifanya nifikiri vizuri na kuniweka kwenye pembe isiyo na nyuzi.

Naomba niinukuu
Mwanzo 3;1
Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani?

2 Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula;

3 lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema,Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa.

Suala la kwanza ambalo linakuja kichwani kwa mtu anayejua kufikiri haswa ni hili.
Je Nyoka alipata wapi taarifa kuwa Adamu na Hawa wamekatazwa Kula tunda?
Hilo lingekuwa suali langu la kwanza kabisa.

Maana ukiliingalia swali la Nyoka ni kana kwamba hakuwepo siku Adamu na Hawa wakipewa amri hiyo. Ikiwa hakuwepo aliyempasha habari ni nani. Je ni Mungu mwenyewe alitaka kuwajaribu Adamu na Hawa. Jibu ni hapana kwa sababu kama Nyoka angekuwa ametumwa na Mungu basi ni wazi Mungu asingempa adhabu alivyokuja baadaye.

Je alitumwa na Adamu. Hapa jibu linaweza kuwa ndio ama hapana. Jibu linaweza kuwa ndio kwa sababu adamu alikubali kula kwa makusudi. Lakini linauwezekano mkubwa wa kuwa ni hapana kwa sababu Adamu anamjibu Mungu kuwa huyu Mwanamke uliyenipa. Ni kama anamlaumu.

Wengine Watasema kuwa Nyoka ni shetani. Jibu ni hapana Kwa maana aya hiyo inaeleza wazi kabisa kuwa Nyoka alikuwa miongoni mwa Wanyama werevu. Neno mnyama linafuta mjadala wa kuwa Nyoka anayezungumziwa ni Lusifa.

Je Lusifa alimuingilia Nyoka mnyama. Jibu linaweza kuwa ndio kwa sehemu kubwa. Lakini swali kuu litakalo tuweke kwenye pembe isiyo na nyuzi ni hili. Je Lusifa alijuaje kuwa Adamu na Hawa Wameambiwa Wasile mti wa Kati wa ujuzi wa wema na ubaya?

Je Lusifa alikuwepo siku Adamu na Hawa wakiambiwa. Kama hakuwepo je Mungu ndiye aliyemuambia. Hili jibu lake ni hapana sio Mungu aliyemuambia kwani asingekuja baadae kutoa adhabu.

Je Lusifa alijuaje kuwa Adamu na Hawa waliambiwa wasile tunda. Kwa nini Lusifa amuone Nyoka ndiye atakaye ifanya misheni nzima mpaka inakamilika. Jibu ni kuwa alikuwa miongoni mwa wanyama werevu. Je Lusifa hakumuona Nyani, Sokwe au Mbwa ambao kwa kiasi kikubwa wanamzidi werevu nyoka.

Swali kuu la Msingi ambalo ndilo limebeba jumbe hii ni kuwa Lusifa alijuaje kuwa Adamu na Hawa waliambiwa Wasile mti wa kati wa ujuzi wa mema na mabaya?

Huo ndio ulikuwa mwanzo wa Ujasusi. Mwanzo wa ukachero. Mwanzo wa upelelezi.

Lusifa alishinda mechi yake ya kwanza na Mwanadamu na kumdondosha. Lakini katika mechi ile tuna mambo ya kujifunza katika fani ya Ujasusi.

Ujasusi ni elimu ya kupeleleza, kuchunguza na kudadisi siri za watu wengine au viumbe wengine. Ni ukusanyaji wa Taarifa zozote kwa kujihami, kujilinda, kujiendeleza au kumkabili adui.

Ukiangalia simulizi hiyo utagundua mambo yafuatayo;
Mosi, Hawa alikuwa hajui anaongea na nani. Alimuona Nyoka lakini kumbe hakuwa nyoka. Pia hakujua lengo la maswali ya Nyoka.

Mbili, Nyoka alikuwa na taarifa zote za Msingi na alilenga Target.
Japo hatujui nyoka alipata wapi taarifa lakini tunachokiona ni kuwa anataarifa za kutosha na anajua anachokifanya. Pia alilenga targeti.

Tatu, Hawa hakuwa na uhakika na matokeo ya kile atakachokifanya.

Elimu ya Ujasusi inahitaji mambo makuu yafuatayo;
1. Taarifa au Data za kutosha
2. Siri. Namna ya kutunza siri.
3. Sehemu ya kupatia taarifa.
4. Utekelezaji wa Taarifa.

Hapo tunamuona Nyoka akicheza maeneo yote muhimu. Ni wazi alishinda.

Ujasusi ni pembe isiyo na nyuzi hicho ndicho naweza kusema.

Katika kudhibiti uibaji wa taarifa baina ya mtu na mtu. Ndipo Sasa Mungu akaja na Mpango mkakati wa kuzuia utokaji wa Taarifa bila ruhusa ya mtu.

Alichokifanya ni Kuweka ukuta baina ya mawazo ya mtu mmoja na mtu mwingine. Yaani mimi Taikon ninachokifikiria mwingine asijue ninafikiria nini. Halikadhalika na wewe ufikiriapo nisijue.

Hekima hii ni kubwa sana. Na hapo ndipo iliposiri ya mafanikio katika jambo lolote. Ukitaka kufanikiwa ni lazima ujue kulinda siri za mafanikio yako.

Mtu asiye na siri kamwe hawezi kufanikiwa. Taifa lisilo na siri kamwe haliwezi kupiga hatua.

Inafahamika kuwa hakuna kiumbe au taifa au sayari isiyo na adui. Hivyo kama mtu au taifa lisipokuwa na njia nzuri ya kutunza siri na mikakati basi maadui huharibu njia hizo.

Mungu kujificha na kuweka mambo kama siri. Kufanya maisha yasieleweke. Kufanya mtu asijue kesho ni hekima. Ni ujuzi mkubwa.

Ila wapo majasusi wanaoibaga siri za Kiroho na ndio hao wanageuka Watabiri na manabii wa uongo. Wengine anaweza kukuambia kesho mvua itanyesha na ikanyesha. Huyo ni Jasusi kiroho aliyeiba au kuletewa taarifa.

Ujasusi ni pembe isiyo na nyuzi yenye manufaa kwa usalama wa ulimwengu au taifa lolote.

Nyenzo kubwa ya Ujasusi ni Kichwa. Kichwa ndicho hubeba siri na ndio njia ya kuaminika ambayo haiwezi kudukuliwa. Ingawa Wataalamu wa zama hizi wanahangaika kutengeneza dhana za kisayansi zitakazosaidia kujua mtu anafikiria nini lakini hii itachukua muda mrefu kufanikiwa.

Katika utangulizi huu. Nimalize kwa kusema. Linda ubongo wako ikiwa unahitaji kufanikiwa. Usiseme mambo ya kichwani mwako kwa watu usiowafahamu. Usijibu maswali kwa watu usiojua lengo la maswali yao.

Kwa mfano mtu anakuuliza. Vipi mipango inaendaje. Au maisha yapoje huko mjini. Au vipi kazi. Au vipi mumeo/Mkeo hakusumbui.

Kuwa makini. Cheza kwa taadhari huu ni Ulimwengu.

Robert Heriel
Taikon Wa Fasihi.
0693322300
 
bad spenko

Member
Jun 22, 2020
67
125
Utangulizi mzuri Kuna somo kubwa sana la kujifunza hapa, ungemalizia thread yote tupate kujifunza zaidi..
 
Makanyaga

JF-Expert Member
Sep 28, 2007
5,647
2,000

Pembe isiyo na nyuzi ni mduara ulio na nyuzi 360
 
Platov agnt

Member
Nov 22, 2018
15
45

Kuna ya kujifunza hapa//pongezi chief umenipa kitu kipya//
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom