Kuna kundi la majambazi limeibuka hivi karibuni na kutikisa maeneo ya Goba mpakani na Makongo juu..majambazi hayo yalikuwa takribani ishirini, kumi wakiwa ndani na kumi nje. Ndani ya wiki moja matukio ya aina hiyo yametokea Mara mbili kwa Watu ambao ni majirani. Kundi hili linavamia kwa kulipua mageti ya grill kwa baruti na kuingia ndani hasa mida ya usiku wa manane. Tunaomba Kamanda Kova usikie kilio hiki tupate patrol wakati tukisubiri kituo cha polisi kikijengwa Goba. Naomba kuwakilisha hoja!