Uislamu bila propaganda hauwezi kusimama

Uislamu bila propaganda hauwezi kusimama

Haujajibu.
Hakuna sehem kwenye quran allah alisema aitwe allah na hakuna ushuhuda wa nani alisikia au kuona mtume akishushiwa wahy.

Ibaki hivyo kwa kumbukumbu.

Pia Siwez kukimbia hoja zako mfu.
Unataka kujua nani aliandika kitabu kipi?.

Hapo ulipo qoute ni mtu aliyesimuliwa ndio anaandika.
Musa ndio alisimulia visa vya Mwanzo..

Kitabu cha Mwanzo (Genesis):

Biblia ya NIV , ukurasa wa 2 imeandika hivi :

Kihistoria, Wayahudi na Wakristo wote wanaamini kuwa Musa ndiye mwandishi/mkusanyaji wa vitabu vitano vya kwanza vya Agano la Kale. Vitabu hivi, vinavyojulikana pia kama Pentateuki (ikimaanisha 'kitabu cha vitabu vitano'), vilitajwa katika desturi za Kiyahudi kama sehemu tano za sheria (ya Musa). Biblia yenyewe inapendekeza uandishi wa Musa wa Mwanzo, kwani Matendo 15:1 yanataja ukeketaji kama 'desturi iliyofundishwa na Musa,' ishara inayorejelea Mwanzo 17. Hata hivyo, inaonekana kuna baadhi ya mabadiliko ya kihariri yaliyofanywa baadaye (angalia, kwa mfano, maelezo ya 14:14; 36:31; 47:11)."

(Kutoka kwenye Maelezo ya Biblia ya NIV [1], ukurasa wa 2)

Kwa hivyo, kwa kweli, kitabu cha Mwanzo kimeingiliwa na binadamu. Kimeharibika.

Ni hatari kuzingatia vyote kama Maneno ya Kuishi ya Kweli ya Mungu Mwenyezi, kwa sababu kufanya hivyo kunatupa hatari ya kuhalalisha dhambi dhidi Yake, kwani tunadai kwamba Alisema maneno ambayo hakusema.

Mwanzo 11

– Je, Musa alikuwa nabii wa uongo, au je, Biblia imeharibiwa?
 – Hasira ya Mungu Mwenyezi katika Isaya 9, Yeremia 5, 14, 23 na 28?

Isaya 9:15
15 Wakuu na watu mashuhuri ndio kichwa, wabii wanaofundisha uongo ndio mkia.

Yeremia 5:31
31 Wabii wanabii uongo, makuhani wanaongoza kwa mamlaka yao wenyewe, na watu wangu wanapenda hivi. Lakini mwishoni mwa siku, mtafanya nini?

Yeremia 14:14
14 Kisha Bwana akaniambia, "Wabii wanabii uongo kwa jina langu. Sijawatuma wala sijawaweka, wala sijawaongea nao. Wanakubebesha macho yenu maono ya uongo, upatanisho wa kishirikina, sanamu, na dhana za akili zao wenyewe."

Yeremia 23:10
10 Nchi imejaa wavamizi wa ndoa; kwa sababu ya laana, nchi imekauka na malisho jangwani yamekauka. Wabii wanafuata njia mbaya na kutumia nguvu zao kwa dhuluma.

Yeremia 23:14

14 "Katika manabii wa Yerusalemu nimeona neno linalochukiza sana; hufanya zinaa; huenda katika maneno ya uongo, hutia nguvu mikono ya watendao maovu, hata ikawa hapana mtu arejeaye na kuuacha uovu wake; wote pia wamekuwa kama Sodoma kwangu, na wenyeji wake kama Gomora.

Yeremia 28:15

15 Kisha nabii Yeremia akamwambia nabii Hananiah, "Sikiza, Hananiah! Bwana hajakutuma, lakini umewashawishi watu hawa kuamini uongo."

Yeremia 23:24-26

24 "Je, mtu anaweza kujificha mahali siri ili nisiwaone?" asema Bwana. "Sidhani kuwa nimejazaa mbingu na nchi?" asema Bwana.

25 "Nimesikia ni nini wanavyosema wabii wanaobii uongo kwa jina langu. Wanasema, 'Nilikuwa na ndoto! Nilikuwa na ndoto!'

26 Je, hili litaendelea kwa muda gani katika mioyo ya wabii hawa waongo, wanaobii dhana za akili zao wenyewe?"

Kutokana na makosa yasiyopingika ya kisayansi na matusi makubwa dhidi ya Mungu Mwenyezi katika mistari ya Mwanzo 11:1-9 iliyotajwa hapo juu, swali linalotakiwa kuulizwa kwa kuzingatia mistari niliyotaja ni:

Je, Musa alikuwa nabii wa uongo, au Biblia imeharibika?

NASABA YA MUHAMMAD ﷺ SI “PROPAGANDA”

  1. Mtume Muhammad ﷺ hakukanusha kuwa mzao wa Ismail, bali alikataza kudai uhakika wa nasaba za mbali zisizo na ushahidi kamili.
    Kauli za Imam Malik na Ibn Khaldun zinasema wazi:
    hatuna uhakika wa majina yote baada ya Adnan,
    hazisemi kuwa nasaba ya Ismail ni ya uongo.

Kutokujua kila jina ≠ kukanusha asili.

  1. Waarabu kabla ya Uislamu walijitambua kama kizazi cha Ismail, jambo linaloendana na Biblia yenyewe:

Ahadi ya taifa kubwa kwa Ismail ilitimia kupitia Waarabu.

  1. Biblia inamkiri Ismail kama mrithi wa ahadi ya kimataifa, si Isaka peke yake:

Hivyo kuhusishwa kwa Waarabu na Ismail si propaganda ya Kiislamu, bali ni simulizi ya Biblia pia.

  1. Qur’an haikujenga utume juu ya nasaba, kwa sababu Uislamu haupimi haki kwa damu:

Na hata Biblia inakiri:

  1. Kama Uislamu ungekuwa propaganda ya ukoo, Muhammad ﷺ angejinasibisha wazi kwa Ibrahim. Hakufanya hivyo.
    Huu ni ushahidi wa uaminifu, si uongo

Kwa kumalizia:

Hakuna ushahidi wa kusema “Muhammad si mzao wa Ismail”.
Kilichopo ni tahadhari ya kielimu kuhusu maelezo ya kina ya nasaba — jambo ambalo Biblia yenyewe pia ina migongano ya nasaba (Mathayo 1 ↔ Luka 3).

Kwa Hivyo, madai ya “propaganda” hayasimami kielimu, kihistoria wala kibiblia.
Tafadhali usi quote Biblia ambayo ime chakachuliwa Sheikh,sio sawa kuchagua mistari ambayo unahisi inakufaa na mingine kuiona takataka.

Tumia Quran na hadithi tu kumtafuta na kumsemea Mohamed kwa sababu ni vitabu pekee ambavyo havija chezewa na waandishi wake.
 
Nilitegemea ujibu hoja zangu ila umekuja na cheap propaganda

Au hoja ni NZITO?
Hapana nimeshasema umejipanga vizuri kihoja. Nachoshangaa mimi ni vipi hawa waliotufikishia dini za kikristo (wazungu) tena wabobezi wa theology leo wakahiari makanisa yao kugeuzwa kuwa misikiti. Sio kuwa masinagogi. Kuwa misikiti. Wao wataswali wapi?
 
Jengo la kanisa likibadilishwa matumizi halibatilishi imani ya Ukristo, kama vile nyumba ikibadilishwa matumizi haimaanishi familia imekufa.

Aidha, makanisa yanauzwa kwa yeyote anayeweza kununua wakati mwingine misikiti, wakati mwingine maktaba, hoteli, nyumba n.k

Wakristo hawaswali kwenye majengo bali katika Roho na kweli (Yoh. 4:21–24).

Ukristo hauko kwenye kuta za mawe bali kwenye waumini; na historia inaonyesha Kanisa liliendelea hata bila majengo, chini ya mateso, na linaendelea hadi leo.

HAYA RUDI KWENYE MADA HUSIKA
 
Jengo la kanisa likibadilishwa matumizi halibatilishi imani ya Ukristo, kama vile nyumba ikibadilishwa matumizi haimaanishi familia imekufa.

Aidha, makanisa yanauzwa kwa yeyote anayeweza kununua wakati mwingine misikiti, wakati mwingine maktaba, hoteli, nyumba au vituo vya sanaa.

Wakristo hawaswali kwenye majengo bali katika Roho na kweli (Yoh. 4:21–24).

Ukristo hauko kwenye kuta za mawe bali kwenye waumini; na historia inaonyesha Kanisa liliendelea hata bila majengo, chini ya mateso, na linaendelea hadi leo.

HAYA RUDI KWENYE MADA HUSIKA
On a similar note, uislamu hautegemei DNA link ya Muhammad to Ishmael, Ibrahim, Adnan, Samson, Mkwawa au Ghengistan. Uislam unategemea Quran & Sunna. Nasaba za mitume WOTE zinapotajwa ni kutusaidia tuu kujua chimbuko lao. Sio kwamba chimbuko lao ndio tukufu
 
Hoja kwamba “Uislamu ni dini mpya kwa sababu Muhammad hakukuta Waislamu” ina kosa la mantiki.

👉 Yesu alipokuja hakukuta Wakristo,
👉 Musa alipokuja hakukuta Wayahudi,
lakini hakuna Mkristo anayesema kuwa kumtii Mungu kulianza na Yesu au Musa.

Yesu mwenyewe alisema:

Hiyo ndiyo Tauhidi / Uislamu = kumtii Mungu mmoja.

Biblia pia inasema kuhusu Yesu:

Mtu anayesujudu na kumuomba Mungu anajisalimisha kwa Mungu, si kwa nafsi yake.

Yesu hakufundisha Ukristo, bali alisema:

Neno “Ukristo” halipo kwenye Injili za Yesu, kama vile neno “Uislamu” halipo kwenye Taurati au Injili — lakini kumtii Mungu mmoja kulikuwepo.

Kwa hiyo:

  • Muhammad hakuanzisha kumtii Mungu
  • alirejesha ibada ya Mungu mmoja kama ya Ibrahim

Biblia inasema wazi kuhusu Ibrahim:

👉 Kumtii Mungu = kujisalimisha kwake
👉 Huo ndiyo Uislamu kwa maana ya Qur’an

Tatizo si historia, tatizo ni kuchanganya jina la dini na maana ya dini.
Una uhakika gani kwamba una quote maneno ya Yesu. Yesu huyo huyo unaye mquote kusali kifudifudi pia alisali siku ya sabato.

Yesu huyo huyo alisema Mungu ni baba yake,alifunga siku 40 bila kula,alibatizwa. Hayo yote waislamu hamyafanyi.

Lete mifano ya kwenye Quran na hadithi jinsi Yesu alivyoishi,alivyo sali,alivyo funga nk. Maana ukichukua kwenye Biblia basi Allah ni baba pia,sio hivyo tu hata Yesu ni mwana wa Mungu .
Hapana nimeshasema umejipanga vizuri kihoja. Nachoshangaa mimi ni vipi hawa waliotufikishia dini za kikristo (wazungu) tena wabobezi wa theology leo wakahiari makanisa yao kugeuzwa kuwa misikiti. Sio kuwa masinagogi. Kuwa misikiti. Wao wataswali wapi?
Ukristo sio majengo Chief, Biblia inasema mcheni bwana katika roho na kweli . Ukija kwenye ishu ya makanisa kugeuzwa misikiti,sishangai sana.

Ukienda Ulaya watu wengi wa pale ni wakristo wa asili sio wa imani. Yaani mtu kazaliwa kwa familia ya wakristo lakini haishi katika imani. Hawaendi kusali wala kuishi vile imani inataka.

Majengo ya makanisa yanakosa waumini mengine yanauzwa. Wanao nunua makanisa ni watu gani? Wahamiaji wa kiislamu kutoka middle East,West na North Africa.

Huko walikotoka hawakuwa waislamu halisi,ila kufika Ulaya wanajiona wana mission ya kusambaza dini. Ukienda Ulaya waislam wengi ni wahamiaji sio wakazi wa pale wa asili.

Je uislamu unakua Ulaya kwa kusilimisha watu, hapana. Wahamiaji lakini pia wao kuzaana sana. Bahati mbaya pia kizazi kipya cha waislamu wa Ulaya hawashiki dini ila kuna kelele za wachache ili ionekane kuna nguvu kubwa.

Uislamu ni mfumo wa kisiasa nd ndiyo maana hauruhusu wakristo kwenda kuhubiri injili na kufungua makanisa kwenye nchi zao. Tungekuwa na equal playing field hata uarabuni kungekuwa na mabadiliko makubwa sana.

Mwisho wa siku imani sio game of numbers,Mungu wetu wakristo anahitaji watu watakao mcha kwa roho na kweli. Njia ya kwenda kwake ni nyembamba sana. Tunalijua hilo na ndiyo maana hatuna stress, wenzetu wanataka numbers.
 
On a similar note, uislamu hautegemei DNA link ya Muhammad to Ishmael, Ibrahim, Adnan, Samson, Mkwawa au Ghengistan. Uislam unategemea Quran & Sunna. Nasaba za mitume WOTE zinapotajwa ni kutusaidia tuu kujua chimbuko lao. Sio kwamba chimbuko lao ndio tukufu
Kwanini mnatafuta au mnajisingizia kwa manabii wa kiyahudi ?

Halafu Kauli yako inajipinga yenyewe. Kama kweli Uislamu hautegemei nasaba, basi kwa nini ndani ya Uislamu imejengwa hoja nzima kwamba Muhammad ni uzao wa Ismael ili kujinasibisha na Ibrahimu na kusingizia alifika Makka akajenga Ka‘aba?

Ukweli ni kwamba Quran haijasema Muhammad ni uzao wa Ismael, na Sunna sahihi haijathibitisha hilo, ndiyo maana wanazuoni wenu wenyewe waliishia Adnan na wakakataza kuendelea mbele.

ila sababu Uislamu umejengwa kwa propaganda mnajinasibisha kwa manabii ambao 99.99% ni wayahudi .

Nasaba ya Ismael haikutoka kwa Quran wala Muhammad, bali ilitungwa na Ibn Ishaq karne ya 8 AD, zaidi ya miaka 130 baada ya Muhammad kufa.

Hivyo basi, tatizo si DNA, tatizo ni kudai nasaba ya kidini bila ushahidi wa kimaandiko wala kihistoria.

Kama nasaba ni ya kusaidia tu kujua chimbuko, basi msingeilazimisha kama ukweli wa kidini.

Lakini ukweli unabaki chimbuko la Ismael kwa Muhammad halithibitishwi na Quran, halithibitishwi na Sunna sahihi, na halisimami kihistoria ni UPOTOSHAJI

Uislamu bila kujinasibisha kwa manabii wa kiyahudi au nasaba ya ismael,haupo
 
Fuatilia kwa umakini mafundisho ya Dini ya Uislamu utagundua yana uongo na upotofu mwingi ndani yake hayakutoka kwa Mungu wa kweli bali wa uongo.
Kwa lugha nyepesi ni mafundisho ya Shetani.
 
UISLAMU NI DINI ILIYOJENGWA KWA PROPAGANDA
Leo nitatolea mfano fundisho moja ambalo hata wakristo wengi wamejikuta wakiingia kwenye hii propaganda, ila kwakuwa elimu ni bahari. Leo natolea mfano wa hili fundisho la kuwa

MUHAMMAD KATOKA UZAO WA ISHMAEL

Uislamu ni dini iliyojengwa juu ya propaganda kubwa. Karibu kila fundisho lake limefungamanishwa kwa makusudi na kizazi cha Uyahudi na manabii wa Kiyahudi.

Muislamu akikupa andiko, mara nyingi hupotosha maana; akikupa historia, huichanganya na simulizi zisizo na uthibitisho.

Uislamu bila propaganda hauwezi kusimama.
Shukrani kwa teknolojia ya leo, mambo mengi yaliyofichwa kwa karne sasa yanawekwa wazi.

Moja ya propaganda kubwa kabisa ndani ya Uislamu, ambayo hata Wakristo wengine wameanza kuiamini kimakosa, ni madai kwamba Muhammad ni uzao wa Ishmael.

Kuna imani iliyoenea miongoni mwa Waislamu kuwa Muhammad ﷺ ni uzao wa Ismail bin Ibrahim kupitia kizazi cha Adnan. Hata hivyo, ushahidi wa hadith na wanazuoni wa mwanzo wa Kiislamu unaonyesha wazi kuwa Muhammad mwenyewe hakuwahi kuthibitisha nasaba hiyo, na kwa makusudi alikataa madai yanayovuka Adnan.

Muhammad ﷺ alinukuliwa akisema👇👇

"Al-kadhdhābūna fī al-ansāb. Fa-idhā dhakartum fa-qūlū: fulān ibn fulān ḥattā tablughū Adnān."

“Wanaoeleza nasaba (za mbali) ni waongo. Mkisema nasaba, semeni: fulani bin fulani, mpaka mfikie Adnan.”

(Imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas – Musnad Ahmad, Juzuu 1, uk. 344; pia imetajwa na Al-Tabarani)

Kauli hii ni nzito sana. Inaonyesha wazi kwamba Muhammad aliwaita waongo wale wanaodai kujua nasaba inayovuka Adnan hadi kwa Ismail au Ibrahim.

Kama Muhammad mwenyewe alikataa nasaba hiyo, Waislamu wa leo wanaitoa wapi?

Leo hii, Waislamu wametengeneza family trees za uongo, wakimunganisha Muhammad moja kwa moja na Ibrahim kupitia Ismail. Hizi simulizi hazikujulikana wakati wa Muhammad, bali zilianza kusambazwa vizazi kadhaa baada ya kifo chake.

Na mtu aliyeileta hii propaganda ni Ibn ishak mwanauzuoni wa uislamu.Maana ingekuwa vigumu kuwashawishi watu kuhusu uislamu bila kusingizia Muhammad ana nasaba na Ibrahim kuja Hadi kwa ismaili.

Ni propaganda ya baadaye, si historia.
Wanazuoni wakubwa wa mwanzo wa Kiislamu walikuwa waangalifu sana juu ya suala hili.

Imam Malik bin Anas, mwanazuoni wa Madina, alinukuliwa akisema:

“Man za‘ama annahu ya‘rifu nasaba al-Nabiy ḥattā Ādam faqad kadhiba.”

“Yeyote anayesema kuwa anajua nasaba ya Mtume hadi kwa Adam, basi huyo ni muongo.”
(Imenukuliwa katika vitabu vya nasaba na wanazuoni wa Madina, pia ikitajwa na Ibn Abd al-Barr)

Kauli hii inaonyesha kuwa hata katika karne za mwanzo kabisa za Uislamu, madai ya nasaba ya mbali hayakukubaliwa kielimu.

Mwanahistoria mashuhuri wa Kiislamu Ibn Khaldun aliandika wazi kabisa:

“Wa ammā al-nasab fīmā fawqa Adnān fa-lā yaṣiḥḥu minhū shay’.”
“Kuhusu nasaba iliyo juu ya Adnan, hakuna hata moja iliyo sahihi kihistoria.”
(Ibn Khaldun – Al-Muqaddimah, mlango wa Ansab)

Vivyo hivyo, Ibn Sa‘d katika Tabaqat al-Kubra alipoorodhesha nasaba ya Muhammad, aliishia Adnan, na akaandika wazi:

“Tumefikia mpaka Adnan. Yanayozidi hapo hayana uthibitisho wa kuaminika.”

Kwa hiyo, kinyume na propaganda za leo, hakuna ushahidi wa kihistoria wa Kiislamu unaothibitisha kuwa Muhammad ni uzao wa Ismail.

Ni muhimu pia kukumbuka:

👉 Qur’an haijasema popote kwamba Muhammad ni uzao wa Ismail.

Qur’an inamtambulisha Muhammad kama Mtume kwa Waarabu (rasūlan minhum), si kama mzao wa Ibrahim wala Ismail.

Msingi wa utume wa Muhammad haukujengwa juu ya damu au ukoo wa kinabii, bali juu ya simulizi ya wahyi kule pangoni, kiumbe aliyedai kumuona, na kuthibitishwa baadaye na Khadija na Waraqah bin Nawfal.,huku muhamad alisema alikutana na kuchezewa na Mashetani.

Hakuna hata mara moja Muhammad alijenga hoja ya utume wake juu ya kuwa mzao wa Ismail.

Kwa hiyo, fundisho kwamba Muhammad ni uzao wa Ishmael ni ubunifu wa baadaye, uliotengenezwa kwa sababu za kisiasa na kijamii, ili kuwapa Waarabu nafasi katika urithi wa Ibrahim ambao tayari Wayahudi na Wakristo walikuwa wanaujadili.

Hapa nasaba ikawa silaha ya kisiasa, si ukweli wa kihistoria.

Kama Muhammad mwenyewe hakujinasibisha na Ismail, basi hakuna sababu ya kuendelea kueneza propaganda hii leo kama ukweli wa imani.

Ukweli huu unapaswa kuwafanya wengi wafungue macho.

Uongo ukisemwa mara nyingi huonekana kama ukweli, lakini teknolojia ya leo imeanza kuvua nguo propaganda hizi.

TEKNOLOJIA IMEKUJA KUWEKA UCHI UISLAMU.
Dini zote kubwa zina propaganda.

Propaganda ndiyo imeziwezesha kukua.
 
KWANINI UISLAMU UNAHOFIA UKRISTO?
Moja ya masuala makubwa yanayoibua mjadala wa kimataifa leo ni uhuru wa kuabudu. Swali linaloulizwa na wengi ni hili:

Kwa nini katika baadhi ya nchi za Kiislamu Ukristo unabinywa, huku Uislamu ukifurahia uhuru mkubwa katika nchi zisizo za Kiislamu?

Katika nchi nyingi za Magharibi:
Waislamu wanaruhusiwa kujenga misikiti
Wanavaa mavazi yao ya kidini hadharani
Wanaswali hata barabarani na viwanjani
Wanahubiri na kusambaza vitabu vyao bila hofu

👉 Hakuna marufuku ya Uislamu kama dini, licha ya nchi hizo kutokuwa za Kiislamu.

Kinyume chake, katika baadhi ya nchi zinazotawaliwa na sheria za Kiislamu:
Wakristo hawaruhusiwi kujenga makanisa mapya
Kuuza au kusambaza Biblia kunapigwa marufuku
Uhubiri wa Kikristo hadharani unaweza kusababisha kifungo au mateso
Kubadili dini kutoka Uislamu kwenda Ukristo huonekana kama kosa kubwa

👉 Hapa ndipo swali la msingi linaibuka:

Kama Uislamu ni dini ya ukweli na inajiamini, kwa nini unaogopa ushindani wa mawazo?

Cha kushangaza zaidi ni kwamba katika baadhi ya nchi hizo hizo:

Matamasha makubwa ya muziki na burudani yameruhusiwa
Baa za pombe na burudani za kisasa zinaidhinishwa
Sherehe zisizo na mizizi ya Kiislamu zinapewa nafasi rasmi

Mifano ya matamasha yanayotajwa mara kwa mara:
Riyadh Season (tamasha kubwa la burudani na muziki)
MDLBEAST Soundstorm (tamasha la muziki wa kisasa)
Sherehe za Halloween katika baadhi ya maeneo ya Ghuba

Dini ya Mashetani ya HALLOWEEN na Sherehe zake zinaruhusiwa:
Angalia Haloween ceremony in Saudi Arabia ujiridhishe:

Ni Demonic Cerebration:
Watu wanajikatakata damu chapachapa:

Lakini
👉 Ukristo? Hapana.
👉 Biblia bure? Hapana.
👉 Kanisa jipya? Marufuku.

JE, HUU NI UHURU AU HOFU?

Uhuru wa kweli wa dini:
Hauchagui dini ipi iruhusiwe
Hauogopi maswali, hoja wala maandiko ya dini nyingine

Haujengwi kwa nguvu, vitisho au marufuku
Dini inayojisitiri kwa mabavu huacha maswali makubwa mioyoni mwa wanaotazama kwa haki.

Ndio maana wanaouacha uislamu katika hizi nchi ni wengi sana, sema hawajutangazi kwa kuogopa kuuwawa
Uislam wala auhofii ukristo ndio maana unakuta uislam umepenya hadi kwenye mataifa ya kikristo lakini ukristo unashindwa kupenya kwenye nchi za kiislam,tena ahitaji hata maelezo mengi mfano angalia tu nilichoandika halafuna article lako uliloandika kunijibu lilivyokua na maelezo mengi
 
Kuna uwanja mmoja wa mapambano au mmoja anabanwa?

Uislam umeenea katika nchi nyingi za Kikristo, lakini sababu si nguvu ya hoja bali ni UHURU WA DINI.,kuzaliana kwa wingi .

Katika nchi hizo

Mkristo kuwa Muislamu (halali)
Muislamu kuwa Mkristo (halali)

Hakuna adhabu ya kisheria
Huu si ushindi wa dini moja, ni matokeo ya UHURU.

Iran 1979, Wakristo waliotoka Uislamu ni mamia, Leo mamia ya maelfu wa WAKRISTO wapo chini ya mateso

Kwenye mazingira haya Bado Ukristo unapenya .Tofauti ni kwamba unapenya gizani, si kwa matangazo.

Kama dini ina uhakika wa ukweli wake, kwa nini ihitaji SHERIA kuilinda?

Ukristo uliingia Ulaya bila dola

Uliingia Roma chini ya mateso

Uliingia China, Iran, Korea bila jeshi

Uislamu unaogopa nini kuruhusu uhuru wa dini nyingine kama ni dini ya kweli?

Uislamu ni sawa na CCM inaogopa tume huru ya uchaguzi ,
 
Nchi za Kiislamu haziruhusu wakristo kufanya mahubiri,kufungua makanisa. Hata kubadili dini ni kosa kisheria,mtu anaweza kufungwa au kuhukumiwa kifo katika baadhi ya nchi.

Ulaya na Marekani dini ni swala binafsi na serikali haihusiki,kuna uhuru wa kuabudu na kubadili dini pia . Asia bibi mwanamke kutoka Pakistan alihukumiwa kifo kwa kusingiziwa kamtukana Mohamed.

Canada ikampa asylum yeye na familia yake ndiyo akatolewa jela ambako alikuwa kwenye death row. Wakristo hatuna hizo mambo za kuua watu kisa dini.
 
Una uhakika gani kwamba una quote maneno ya Yesu. Yesu huyo huyo unaye mquote kusali kifudifudi pia alisali siku ya sabato.

Yesu huyo huyo alisema Mungu ni baba yake,alifunga siku 40 bila kula,alibatizwa. Hayo yote waislamu hamyafanyi.

Lete mifano ya kwenye Quran na hadithi jinsi Yesu alivyoishi,alivyo sali,alivyo funga nk. Maana ukichukua kwenye Biblia basi Allah ni baba pia,sio hivyo tu hata Yesu ni mwana wa Mungu .

Ukristo sio majengo Chief, Biblia inasema mcheni bwana katika roho na kweli . Ukija kwenye ishu ya makanisa kugeuzwa misikiti,sishangai sana.

Ukienda Ulaya watu wengi wa pale ni wakristo wa asili sio wa imani. Yaani mtu kazaliwa kwa familia ya wakristo lakini haishi katika imani. Hawaendi kusali wala kuishi vile imani inataka.

Majengo ya makanisa yanakosa waumini mengine yanauzwa. Wanao nunua makanisa ni watu gani? Wahamiaji wa kiislamu kutoka middle East,West na North Africa.

Huko walikotoka hawakuwa waislamu halisi,ila kufika Ulaya wanajiona wana mission ya kusambaza dini. Ukienda Ulaya waislam wengi ni wahamiaji sio wakazi wa pale wa asili.

Je uislamu unakua Ulaya kwa kusilimisha watu, hapana. Wahamiaji lakini pia wao kuzaana sana. Bahati mbaya pia kizazi kipya cha waislamu wa Ulaya hawashiki dini ila kuna kelele za wachache ili ionekane kuna nguvu kubwa.

Uislamu ni mfumo wa kisiasa nd ndiyo maana hauruhusu wakristo kwenda kuhubiri injili na kufungua makanisa kwenye nchi zao. Tungekuwa na equal playing field hata uarabuni kungekuwa na mabadiliko makubwa sana.

Mwisho wa siku imani sio game of numbers,Mungu wetu wakristo anahitaji watu watakao mcha kwa roho na kweli. Njia ya kwenda kwake ni nyembamba sana. Tunalijua hilo na ndiyo maana hatuna stress, wenzetu wanataka numbers.

Sisi hatujengi imani yetu juu ya Biblia, bali juu ya Qur’an na Hadithi sahihi. Tunamheshimu sana Nabii Isa bin Maryam (Yesu), lakini hatumchukulii Biblia kama chanzo cha mwisho cha sheria.

1. Je, tuna uhakika gani wa maneno ya Yesu?​

Kiislamu:
  • Qur’an ndiyo Kitabu kilichohifadhiwa bila kubadilishwa (Qur’an 15:9).
  • Biblia yenyewe ina matoleo mengi na waandishi tofauti, hivyo hatuna uhakika kamili kwamba kila kauli ni maneno ya Yesu halisi.

Kwa hiyo tunapozungumzia Yesu, tunamzungumzia kama alivyoelezwa na Allah mwenyewe ndani ya Qur’an.

2. Yesu alisali kifudifudi – je, Waislamu hufanya hivyo?​

Ndiyo.

Mtume Muhammad ﷺ alisema:

“Mja huwa karibu zaidi na Mola wake akiwa katika kusujudu.”
(Hadithi Sahih – Muslim)

Na Qur’an inasema:

“Enyi mlioamini, rukuni na sujuduni…”
(Qur’an 22:77)

Kusujudu kifudifudi ni msingi wa Swala ya Kiislamu, sawa kabisa na alivyofanya Yesu.

3. Yesu alisali siku ya Sabato – Waislamu hawafanyi?​

Sabato ilikuwa sheria ya Bani Israil, si ya mataifa yote.

Qur’an inasema:

“Sabato iliwekewa wale waliokhitilafiana juu yake.”
(Qur’an 16:124)

Uislamu una sheria mpya (Sharia) iliyokuja na Mtume Muhammad ﷺ, kama Musa na Yesu walivyokuja na sheria zao kwa wakati wao.

4. Yesu alisema Mungu ni Baba yake – Uislamu unasemaje?​

Qur’an inafafanua wazi:

“Haifai kwa Allah kujichukulia mwana.”
(Qur’an 19:35)

Na:

“Yeye hakuzaa wala hakuzaliwa.”
(Qur’an 112:3)

Katika Uislamu

  • Neno “Baba” halichukuliwi kiuhasilia, bali lilikuwa ni neno la lugha ya heshima, kama Biblia pia inavyowaita watu wema “wana wa Mungu”.
    1. Mathayo 5:9

  • “Heri wapatanishi, kwa maana hao wataitwa wana wa Mungu.”
    1. Mathayo 5:44–45

  • “…wapendeni adui zenu… ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni.”
    1. Yohana 1:12

  • “Lakini wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika wana wa Mungu, yaani, wale waliaminio jina lake.”
    1. Warumi 8:14

  • “Kwa maana wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu.”
    1. Wagalatia 3:26

  • “Kwa maana ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu.”
    1. 1 Yohana 3:1

  • “Tazameni pendo la namna gani alilotupa Baba, hata tuitwe wana wa Mungu.”

  • Allah ni Mola (Rabb) wa wote, si baba wa kibinadamu.

5. Yesu alifunga siku 40 – Waislamu hawafanyi?​

Mtume Muhammad ﷺ:

Alifunga Ramadhan
  • Alifunga funga za hiari
  • Alifunga funga ndefu (wisal)
Qur’an:

“Mmefaradhiwa funga kama walivyofaradhiwa waliokuwa kabla yenu.”
(Qur’an 2:183)

Yesu alifunga, na Waislamu hufunga, wote kwa ajili ya kumuabudu Mungu mmoja.

6. Yesu alibatizwa – Uislamu unasemaje?​

Uislamu hauna ubatizo wa maji, lakini una:

  • Kutakaswa kwa toba
  • Udhu na janaba
  • Kuingia Uislamu kwa imani na matendo

Qur’an:

“Hakika Allah anawapenda wanaotubu na wanaojitakasa.”
(Qur’an 2:222)

➡ Kusudio ni utakaso wa roho, si desturi ya maji pekee.

7. Je, Qur’an inamtaja Yesu alivyoishi?​

Ndiyo.
  • Yesu alikuwa mja wa Allah (Qur’an 19:30)
  • Alikuwa mtume (Qur’an 4:171)
  • Alisali (Qur’an 19:31)
  • Alikuwa mnyenyekevu (Qur’an 43:59)
  • Alikataa kuabudiwa (Qur’an 5:116)
 
Nchi za Kiislamu haziruhusu wakristo kufanya mahubiri,kufungua makanisa. Hata kubadili dini ni kosa kisheria,mtu anaweza kufungwa au kuhukumiwa kifo katika baadhi ya nchi.

Ulaya na Marekani dini ni swala binafsi na serikali haihusiki,kuna uhuru wa kuabudu na kubadili dini pia . Asia bibi mwanamke kutoka Pakistan alihukumiwa kifo kwa kusingiziwa kamtukana Mohamed.

Canada ikampa asylum yeye na familia yake ndiyo akatolewa jela ambako alikuwa kwenye death row. Wakristo hatuna hizo mambo za kuua watu kisa dini.
Nitajie nchi moja tu ya kiislamu
 
Kuna uwanja mmoja wa mapambano au mmoja anabanwa?

Uislam umeenea katika nchi nyingi za Kikristo, lakini sababu si nguvu ya hoja bali ni UHURU WA DINI.,kuzaliana kwa wingi .

Katika nchi hizo

Mkristo kuwa Muislamu (halali)
Muislamu kuwa Mkristo (halali)

Hakuna adhabu ya kisheria
Huu si ushindi wa dini moja, ni matokeo ya UHURU.

Iran 1979, Wakristo waliotoka Uislamu ni mamia, Leo mamia ya maelfu wa WAKRISTO wapo chini ya mateso

Kwenye mazingira haya Bado Ukristo unapenya .Tofauti ni kwamba unapenya gizani, si kwa matangazo.

Kama dini ina uhakika wa ukweli wake, kwa nini ihitaji SHERIA kuilinda?

Ukristo uliingia Ulaya bila dola

Uliingia Roma chini ya mateso

Uliingia China, Iran, Korea bila jeshi

Uislamu unaogopa nini kuruhusu uhuru wa dini nyingine kama ni dini ya kweli?

Uislamu ni sawa na CCM inaogopa tume huru ya uchaguzi ,

Hoja yako inaonekana ina mapungufu kadhaa ya kimantiki na kihistoria.

Kwanza, kuenea kwa Uislamu si matokeo ya kuzaliana tu au “uhuru wa dini”. Kama ingekuwa hivyo, basi dini zote zingekuwa zinaenea kwa kiwango kilekile katika mazingira ya uhuru.
Ukweli ni kwamba Uislamu unaendelea kuenea hata katika nchi zisizo za Kiislamu kwa watu wanaochagua kwa hiari baada ya kusoma, kulinganisha na kutafakari.

Pili, kudai kwamba “Mkristo kuwa Muislamu ni halali kila mahali” si sahihi. Historia inaonyesha wazi kwamba katika maeneo mengi ya Kikristo, hasa zamani na hata leo katika baadhi ya nchi, Muislamu hukumbana na ubaguzi, kufukuzwa kazi, au kuchukiwa kijamii. Hivyo uhuru nao una mipaka yake.

Tatu, suala la sheria za Kiislamu kuhusu uasi wa dini (apostasy) linahusishwa na usalama wa jamii na muktadha wa kisiasa wa wakati huo, si hofu ya hoja. Katika historia ya Kiislamu, uasi mara nyingi uliambatana na uhaini, vita au kuvuruga dola, si mabadiliko ya imani binafsi kama ilivyo leo. Hata wanazuoni wa Kiislamu wana tofauti kubwa juu ya utekelezaji wa hilo.

Nne, kusema “Ukristo uliingia bila dola” si hoja kamili. Baada ya kupata dola chini ya Constantine, Ukristo ulitumia nguvu ya dola kwa karne nyingi:
– Kulikuwa na mateso ya wapagani
– Vita vya msalaba
– Inquisition
– Kulazimisha Ukristo kwa makoloni
Hivyo si sahihi kuwasilisha Ukristo kama dini iliyotumia hoja tu bila mamlaka.

Tano, Uislamu hauogopi uhuru wa dini. Qur’an yenyewe inasema:

“Hakuna kulazimishwa katika dini” (Al-Baqarah 256)

Lakini uhuru katika Uislamu unaambatana na uwajibikaji wa kijamii, kama ilivyo katika mifumo mingine yote ya kisheria duniani.

Mwisho, kulinganisha Uislamu na chama cha siasa ni mlinganisho dhaifu. Dini si chama, na imani haipimwi kwa propaganda bali kwa hoja, maadili na athari zake kwa mwanadamu.

Badala ya kuulizana “nani anaogopa nini”, ni bora kuuliza:

Ni dini ipi inaeleza kwa uwazi zaidi asili ya Mungu, maana ya maisha, na uwajibikaji wa binadamu?

Hapo ndipo mjadala wa kweli ulipo.

Huyu ISSA wa kwenye Quran ambaye Mariam mama yake ni dada wa Musa? Sio Yesu ambaye wakristo tunamfuata.

Jibu madawa haya kwa kutumia Quran

Yesu alizaliwa wapi?
Aliishi na kufanya kazi zake za utume wapi?
Alisurubiwa wapi ?
Ni nani alichukua nafasi yake pale msalabani?
Alikuwa na ndugu wa kuzaliwa wa mama mmoja? Wanafunzi? Wangapi?
Mohamed alitoka kabila la Quraish,Yesu alitoka kabila gani?

Je Yesu ni mkuu kuliko Mohamed aliyekufa? Maana Quran inasema Allah alimchukua kwake akiwa hai.
Sisi hatujengi imani yetu juu ya Biblia, bali juu ya Qur’an na Hadithi sahihi. Tunamheshimu sana Nabii Isa bin Maryam (Yesu), lakini hatumchukulii Biblia kama chanzo cha mwisho cha sheria.

1. Je, tuna uhakika gani wa maneno ya Yesu?​

Kiislamu:
  • Qur’an ndiyo Kitabu kilichohifadhiwa bila kubadilishwa (Qur’an 15:9).
  • Biblia yenyewe ina matoleo mengi na waandishi tofauti, hivyo hatuna uhakika kamili kwamba kila kauli ni maneno ya Yesu halisi.

Kwa hiyo tunapozungumzia Yesu, tunamzungumzia kama alivyoelezwa na Allah mwenyewe ndani ya Qur’an.

2. Yesu alisali kifudifudi – je, Waislamu hufanya hivyo?​

Ndiyo.

Mtume Muhammad ﷺ alisema:

Na Qur’an inasema:

Kusujudu kifudifudi ni msingi wa Swala ya Kiislamu, sawa kabisa na alivyofanya Yesu.

3. Yesu alisali siku ya Sabato – Waislamu hawafanyi?​

Sabato ilikuwa sheria ya Bani Israil, si ya mataifa yote.

Qur’an inasema:

Uislamu una sheria mpya (Sharia) iliyokuja na Mtume Muhammad ﷺ, kama Musa na Yesu walivyokuja na sheria zao kwa wakati wao.

4. Yesu alisema Mungu ni Baba yake – Uislamu unasemaje?​

Qur’an inafafanua wazi:

Na:

Katika Uislamu

  • Neno “Baba” halichukuliwi kiuhasilia, bali lilikuwa ni neno la lugha ya heshima, kama Biblia pia inavyowaita watu wema “wana wa Mungu”.
    1. Mathayo 5:9

    1. Mathayo 5:44–45

    1. Yohana 1:12

    1. Warumi 8:14

    1. Wagalatia 3:26

    1. 1 Yohana 3:1

  • Allah ni Mola (Rabb) wa wote, si baba wa kibinadamu.

5. Yesu alifunga siku 40 – Waislamu hawafanyi?​

Mtume Muhammad ﷺ:

Alifunga Ramadhan
  • Alifunga funga za hiari
  • Alifunga funga ndefu (wisal)
Qur’an:

Yesu alifunga, na Waislamu hufunga, wote kwa ajili ya kumuabudu Mungu mmoja.

6. Yesu alibatizwa – Uislamu unasemaje?​

Uislamu hauna ubatizo wa maji, lakini una:

  • Kutakaswa kwa toba
  • Udhu na janaba
  • Kuingia Uislamu kwa imani na matendo

Qur’an:

➡ Kusudio ni utakaso wa roho, si desturi ya maji pekee.

7. Je, Qur’an inamtaja Yesu alivyoishi?​

Ndiyo.
  • Yesu alikuwa mja wa Allah (Qur’an 19:30)
  • Alikuwa mtume (Qur’an 4:171)
  • Alisali (Qur’an 19:31)
  • Alikuwa mnyenyekevu (Qur’an 43:59)
  • Alikataa kuabudiwa (Qur’an 5:116)
 
Nilijuwa utarukia hapo haraka . Hivi unajuwa maana ya kuwa dola ya kiislamu ??
Uniambie wewe? Hizo nchi zina jitambulisha kama Jamhuri za Kiislamu,wewe unabisha?
 
Nchi za Kiislamu haziruhusu wakristo kufanya mahubiri,kufungua makanisa. Hata kubadili dini ni kosa kisheria,mtu anaweza kufungwa au kuhukumiwa kifo katika baadhi ya nchi.

Wakristo hatuna hizo mambo za kuua watu kisa dini.
Crusader wars, Inquisition, vita ya wakatoliki na waprotestant, ukoloni vyote ni vita vya wakristo dhidi ya wasio wao kueneza dini na wengi waliuawa

Vita dhidi ya Wakristo wenzao (Uzushi)
Karne ya 5–7 waliotofautiana kimafundisho (Arians, Donatists n.k.) waliteswa, kufungwa, kuuawa kwa amri ya makanisa na watawala

Vita vya Msalaba (Crusades)
Papa Urban II alitangaza vita kwa Waislamu, Wayahudi, na Wakristo wengine waliuawa
Inquisition (Mahakama za Kanisa) kuangamiza “uzushi” Wayahudi, Waislamu wa Hispania na Wakristo waliotofautiana walichomwa moto, walinyongwa na waliteswa hadi kufa

Spanish Inquisition(recoquinsita)
Wayahudi na Waislamu Walilazimishwa kubatizwa au kufukuzwa au kuuwawa
Wayahudi wote wafukuzwa Hispania na wengi waliuawa njiani

Vita vya Wakristo kwa Wakristo
1618–1648 BK , Vita vya Miaka 30 vya Wakatoliki vs Waprotestanti zaidi ya watu milioni 8 waliuawa na Ulaya ya Kati ikaharibiwa kabisa

Ukoloni na “uenezi wa Ukristo” • Amerika, Afrika na Asia wakazi asili waliuawa walibatizwa kwa nguvu kwa ajili ya Dini + siasa + rasilimali
 
Back
Top Bottom