Uislamu bila propaganda hauwezi kusimama

Uislamu bila propaganda hauwezi kusimama

It doesn't matter ni uzao wa Nani,

It matters unapoona papa anapobariki ushoga, ambayo umepigwa na biblia na anashindwa kubariki watu kuona mke zaidi ya mmoja ambayo haujapigwa na biblia

Na it matters more unapoona waumini hawashtuki. Kwa kifupi ukiristo ni business, ipo siku Catholics au other dominations watawauza waumini wao kama alivowauza kasusura yule wa Uganda
20260110_160058.jpg

hamis77
 
Uislam usingekuwa dini ya haki Ungekuwa umefail,

Instead makanisa yanaendelea kupoteza waumini, na sasa wameamua kubariki sodoma na gomora wakisahau watu waliangamia kwa kubariki hilo

I see the end of Christianity
Dini ya haki Tena!?,Si mnasema ni dini ya amani?!
Mbona mnatuchanganya?
 
Kwamba wanatoa mada za Ukristo wanapambana na Ukristo ?

Nilitegemea ujibu hoja ,cha ajabu unanishambulia utadhani nimevunja Sheria au kumtukana mtu

Njoo na majibu ya kielimu
WATU WA PSYCHOLOGY HUSEMA; KUENDELEA KUPIGANA VITA AMBAYO UNAJUA KWA ASILIMIA MIA (100%) HUTASHINDA, NI UKOSEFU WA AFYA YA AKILI !!!
Unajua kwa nini Waislam hata siku moja huwakuti wakimtukana Yesu, ni kwa sababu wana Afya ya Akili
 
Uislam usingekuwa dini ya haki Ungekuwa umefail,

Instead makanisa yanaendelea kupoteza waumini, na sasa wameamua kubariki sodoma na gomora wakisahau watu waliangamia kwa kubariki hilo

I see the end of Christianity
haimaanishi kwamba uislam utainuka, ndio kwanza unamalizwa, fuatilia nchi za kiislam mashariki ya kati
 
UISLAMU NI DINI ILIYOJENGWA KWA PROPAGANDA
Leo nitatolea mfano fundisho moja ambalo hata wakristo wengi wamejikuta wakiingia kwenye hii propaganda,ila kwakuwa elimu ni bahari,Leo natolea mfano wa hili fundisho la kuwa

MUHAMMAD KATOKA UZAO WA ISHMAEL

Uislamu ni dini iliyojengwa juu ya propaganda kubwa. Karibu kila fundisho lake limefungamanishwa kwa makusudi na kizazi cha Uyahudi na manabii wa Kiyahudi.

Muislamu akikupa andiko, mara nyingi hupotosha maana; akikupa historia, huichanganya na simulizi zisizo na uthibitisho.

Uislamu bila propaganda hauwezi kusimama.
Shukrani kwa teknolojia ya leo, mambo mengi yaliyofichwa kwa karne sasa yanawekwa wazi.

Moja ya propaganda kubwa kabisa ndani ya Uislamu, ambayo hata Wakristo wengine wameanza kuiamini kimakosa, ni madai kwamba Muhammad ni uzao wa Ishmael.

Kuna imani iliyoenea miongoni mwa Waislamu kuwa Muhammad ﷺ ni uzao wa Ismail bin Ibrahim kupitia kizazi cha Adnan. Hata hivyo, ushahidi wa hadith na wanazuoni wa mwanzo wa Kiislamu unaonyesha wazi kuwa Muhammad mwenyewe hakuwahi kuthibitisha nasaba hiyo, na kwa makusudi alikataa madai yanayovuka Adnan.

Muhammad ﷺ alinukuliwa akisema👇👇

"Al-kadhdhābūna fī al-ansāb. Fa-idhā dhakartum fa-qūlū: fulān ibn fulān ḥattā tablughū Adnān."

“Wanaoeleza nasaba (za mbali) ni waongo. Mkisema nasaba, semeni: fulani bin fulani, mpaka mfikie Adnan.”

(Imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas – Musnad Ahmad, Juzuu 1, uk. 344; pia imetajwa na Al-Tabarani)

Kauli hii ni nzito sana. Inaonyesha wazi kwamba Muhammad aliwaita waongo wale wanaodai kujua nasaba inayovuka Adnan hadi kwa Ismail au Ibrahim.

Kama Muhammad mwenyewe alikataa nasaba hiyo, Waislamu wa leo wanaitoa wapi?

Leo hii, Waislamu wametengeneza family trees za uongo, wakimunganisha Muhammad moja kwa moja na Ibrahim kupitia Ismail. Hizi simulizi hazikujulikana wakati wa Muhammad, bali zilianza kusambazwa vizazi kadhaa baada ya kifo chake.

Na mtu aliyeileta hii propaganda ni Ibn ishak mwanauzuoni wa uislamu.Maana ingekuwa vigumu kuwashawishi watu kuhusu uislamu bila kusingizia Muhammad ana nasaba na Ibrahim kuja Hadi kwa ismaili.

Ni propaganda ya baadaye, si historia.
Wanazuoni wakubwa wa mwanzo wa Kiislamu walikuwa waangalifu sana juu ya suala hili.

Imam Malik bin Anas, mwanazuoni wa Madina, alinukuliwa akisema:

“Man za‘ama annahu ya‘rifu nasaba al-Nabiy ḥattā Ādam faqad kadhiba.”

“Yeyote anayesema kuwa anajua nasaba ya Mtume hadi kwa Adam, basi huyo ni muongo.”
(Imenukuliwa katika vitabu vya nasaba na wanazuoni wa Madina, pia ikitajwa na Ibn Abd al-Barr)

Kauli hii inaonyesha kuwa hata katika karne za mwanzo kabisa za Uislamu, madai ya nasaba ya mbali hayakukubaliwa kielimu.

Mwanahistoria mashuhuri wa Kiislamu Ibn Khaldun aliandika wazi kabisa:

“Wa ammā al-nasab fīmā fawqa Adnān fa-lā yaṣiḥḥu minhū shay’.”
“Kuhusu nasaba iliyo juu ya Adnan, hakuna hata moja iliyo sahihi kihistoria.”
(Ibn Khaldun – Al-Muqaddimah, mlango wa Ansab)

Vivyo hivyo, Ibn Sa‘d katika Tabaqat al-Kubra alipoorodhesha nasaba ya Muhammad, aliishia Adnan, na akaandika wazi:

“Tumefikia mpaka Adnan. Yanayozidi hapo hayana uthibitisho wa kuaminika.”

Kwa hiyo, kinyume na propaganda za leo, hakuna ushahidi wa kihistoria wa Kiislamu unaothibitisha kuwa Muhammad ni uzao wa Ismail.

Ni muhimu pia kukumbuka:

👉 Qur’an haijasema popote kwamba Muhammad ni uzao wa Ismail.

Qur’an inamtambulisha Muhammad kama Mtume kwa Waarabu (rasūlan minhum), si kama mzao wa Ibrahim wala Ismail.

Msingi wa utume wa Muhammad haukujengwa juu ya damu au ukoo wa kinabii, bali juu ya simulizi ya wahyi kule pangoni, kiumbe aliyedai kumuona, na kuthibitishwa baadaye na Khadija na Waraqah bin Nawfal.,huku muhamad alisema alikutana na kuchezewa na Mashetani.

Hakuna hata mara moja Muhammad alijenga hoja ya utume wake juu ya kuwa mzao wa Ismail.

Kwa hiyo, fundisho kwamba Muhammad ni uzao wa Ishmael ni ubunifu wa baadaye, uliotengenezwa kwa sababu za kisiasa na kijamii, ili kuwapa Waarabu nafasi katika urithi wa Ibrahim ambao tayari Wayahudi na Wakristo walikuwa wanaujadili.

Hapa nasaba ikawa silaha ya kisiasa, si ukweli wa kihistoria.

Kama Muhammad mwenyewe hakujinasibisha na Ismail, basi hakuna sababu ya kuendelea kueneza propaganda hii leo kama ukweli wa imani.

Ukweli huu unapaswa kuwafanya wengi wafungue macho.

Uongo ukisemwa mara nyingi huonekana kama ukweli, lakini teknolojia ya leo imeanza kuvua nguo propaganda hizi.

TEKNOLOJIA IMEKUJA KUWEKA UCHI UISLAMU.


NASABA YA MUHAMMAD ﷺ SI “PROPAGANDA”


  1. Mtume Muhammad ﷺ hakukanusha kuwa mzao wa Ismail, bali alikataza kudai uhakika wa nasaba za mbali zisizo na ushahidi kamili.
    Kauli za Imam Malik na Ibn Khaldun zinasema wazi:
    hatuna uhakika wa majina yote baada ya Adnan,
    hazisemi kuwa nasaba ya Ismail ni ya uongo.

Kutokujua kila jina ≠ kukanusha asili.

  1. Waarabu kabla ya Uislamu walijitambua kama kizazi cha Ismail, jambo linaloendana na Biblia yenyewe:

“Ishmaeli… nitamfanya kuwa taifa kubwa.”
(Mwanzo 17:20)

“Nitamfanya mwana wa kijakazi kuwa taifa pia.”
(Mwanzo 21:13)

Ahadi ya taifa kubwa kwa Ismail ilitimia kupitia Waarabu.

  1. Biblia inamkiri Ismail kama mrithi wa ahadi ya kimataifa, si Isaka peke yake:

“Kumi na wawili watakaotokana naye, nami nitamfanya kuwa taifa kubwa.”
(Mwanzo 17:20)

Hivyo kuhusishwa kwa Waarabu na Ismail si propaganda ya Kiislamu, bali ni simulizi ya Biblia pia.

  1. Qur’an haikujenga utume juu ya nasaba, kwa sababu Uislamu haupimi haki kwa damu:

“Hakika aliye bora mbele za Mungu ni yule amchaye zaidi.”
(Qur’an 49:13)

Na hata Biblia inakiri:


“Mungu haangalii uso wa mtu.”
(Matendo 10:34)

  1. Kama Uislamu ungekuwa propaganda ya ukoo, Muhammad ﷺ angejinasibisha wazi kwa Ibrahim. Hakufanya hivyo.
    Huu ni ushahidi wa uaminifu, si uongo

Kwa kumalizia:

Hakuna ushahidi wa kusema “Muhammad si mzao wa Ismail”.
Kilichopo ni tahadhari ya kielimu kuhusu maelezo ya kina ya nasaba — jambo ambalo Biblia yenyewe pia ina migongano ya nasaba (Mathayo 1 ↔ Luka 3).


Kwa Hivyo, madai ya “propaganda” hayasimami kielimu, kihistoria wala kibiblia.
 
Halafu wanakuja na propaganda eti Yesu alikua muislam. 😆😆😆

Majibu

Hakuna propaganda. Waislamu wanaposema Yesu alikuwa Muislamu, hawamaanishi Uislamu wa baadaye wa Mtume Muhammad ﷺ, bali maana ya neno Islam lenyewe: kujinyenyekeza kwa Mungu mmoja.
Yesu mwenyewe alisema anafanya mapenzi ya Mungu, aliomba kwa Mungu, na aliwafundisha watu wamwabudu Mungu mmoja. Hiyo ndiyo maana ya Uislamu.

Qur’ani inasema wazi: “Masihi hakujivuna kuwa mtumwa wa Mwenyezi Mungu” (Qur’ani 4:172).
Kwetu sisi, Yesu alikuwa Nabii wa Mungu aliyemwabudu Mungu mmoja — si Mungu mwenyewe.

Yesu alisema: “Baba yangu ni mkubwa kuliko mimi” (Yohana 14:28)
Na pia: “Namwabudu Baba yangu na Baba yenu, Mungu wangu na Mungu wenu” (Yohana 20:17).
Hiyo inaonyesha Yesu alikuwa anamwabudu Mungu, si yeye Mungu.


Sio propaganda, ni tofauti ya maana. Yesu hakuwahi kusema “ni Mungu”, bali alifundisha kumwabudu Mungu mmoja — hilo ndilo Waislamu wanaliita Uislamu.

Kicheko hakibadilishi historia. Hoja hujibiwa kwa hoja, si emoji 😄
 
Wazungu wenyewe wameanza kuamka wanakwambia

Islamic is not a religion but political movements

Wanasema hawataki coexistence na Islamic
Naamini wameonja ugaidi ulivyo

Uislamu ni dini, si ugaidi wala harakati za kisiasa.

Kuhukumu dini kwa matendo ya wachache si haki.

Biblia yenyewe inafundisha: “Msihukumu kwa hukumu ya kuonekana, bali hukumuni kwa hukumu ya haki” (Yohana 7:24), na “Heri wapatanishi” (Mathayo 5:9). Kama Wakristo, mnapaswa kutofautisha kati ya dini na matendo ya watu wachache, si kuhukumu kwa chuki.
 
Uislamu ni dini, si ugaidi wala harakati za kisiasa.

Kuhukumu dini kwa matendo ya wachache si haki.

Biblia yenyewe inafundisha: “Msihukumu kwa hukumu ya kuonekana, bali hukumuni kwa hukumu ya haki” (Yohana 7:24), na “Heri wapatanishi” (Mathayo 5:9). Kama Wakristo, mnapaswa kutofautisha kati ya dini na matendo ya watu wachache, si kuhukumu kwa chuki.
Umejibu vizuri sana kwa busara kubwa.
 
Unawezaje kunitajia muislamu au waislamu wa KABLA ya Muhammad ambao Muhammad alikutana nao ,nitajie hata mmoja

Swali lako linaonyesha mkanganyiko wa msingi. “Muislamu” si jina la kikabila au la Muhammad, bali ni mtu anayejisalimisha kwa Mungu Mmoja.

Biblia yenyewe inawataja watu wa namna hiyo kabla ya Muhammad.


Ibrahimu hakuwa Mkristo wala Myahudi, lakini Biblia inasema: “Ibrahimu alimtii Mungu” (Mwanzo 22:18). Paulo anakiri: “Ibrahimu aliishi kabla ya sheria” (Warumi 4:10–11).

Nuhu aliitwa “mtu wa haki, akienda pamoja na Mungu” (Mwanzo 6:9).

Yesu mwenyewe alisema: “Si kila asemaye Bwana, Bwana… bali afanyaye mapenzi ya Baba” (Mathayo 7:21).


Sasa niulize: kama hawa walimtii Mungu Mmoja, waliisalimisha nafsi zao kwa Mungu, lakini hawakuwa Wakristo, unawaitaje?

Ukisema hawakuwa “Waislamu” kwa sababu jina halikuwepo, basi hata Yesu hakuwa Mkristo, kwa kuwa Ukristo ulianza baada yake.
 
NASABA YA MUHAMMAD ﷺ SI “PROPAGANDA”


  1. Mtume Muhammad ﷺ hakukanusha kuwa mzao wa Ismail, bali alikataza kudai uhakika wa nasaba za mbali zisizo na ushahidi kamili.
    Kauli za Imam Malik na Ibn Khaldun zinasema wazi:
    hatuna uhakika wa majina yote baada ya Adnan,
    hazisemi kuwa nasaba ya Ismail ni ya uongo.

Kutokujua kila jina ≠ kukanusha asili.

  1. Waarabu kabla ya Uislamu walijitambua kama kizazi cha Ismail, jambo linaloendana na Biblia yenyewe:





Ahadi ya taifa kubwa kwa Ismail ilitimia kupitia Waarabu.

  1. Biblia inamkiri Ismail kama mrithi wa ahadi ya kimataifa, si Isaka peke yake:



Hivyo kuhusishwa kwa Waarabu na Ismail si propaganda ya Kiislamu, bali ni simulizi ya Biblia pia.

  1. Qur’an haikujenga utume juu ya nasaba, kwa sababu Uislamu haupimi haki kwa damu:



Na hata Biblia inakiri:




  1. Kama Uislamu ungekuwa propaganda ya ukoo, Muhammad ﷺ angejinasibisha wazi kwa Ibrahim. Hakufanya hivyo.
    Huu ni ushahidi wa uaminifu, si uongo

Kwa kumalizia:

Hakuna ushahidi wa kusema “Muhammad si mzao wa Ismail”.
Kilichopo ni tahadhari ya kielimu kuhusu maelezo ya kina ya nasaba — jambo ambalo Biblia yenyewe pia ina migongano ya nasaba (Mathayo 1 ↔ Luka 3).


Kwa Hivyo, madai ya “propaganda” hayasimami kielimu, kihistoria wala kibiblia.
Acha porojo za kindezi jamvini.
 
Dini inajifagilia balaa:
Ikishindwa inawatisha waumini:.
Sunan an-Nasa'i 4059
Ibn 'Abbas said:
"The Messenger of Allah [SAW] said: 'Whoever changes his religion, kill him.'"
 
Ona hapa:.
𝐔𝐎𝐍𝐆𝐎 𝐖𝐀 𝐔𝐈𝐒𝐋𝐀𝐌𝐔 𝐍𝐀 𝐌𝐔𝐇𝐀𝐌𝐌𝐀𝐃
𝐂𝐡𝐚𝐧𝐠𝐚𝐦𝐨𝐭𝐨 𝐲𝐚 𝐊𝐢𝐡𝐢𝐬𝐭𝐨𝐫𝐢𝐚 𝐧𝐚 𝐊𝐢𝐦𝐚𝐧𝐭𝐢𝐤𝐢

Waislamu hudai kuwa Uislamu haukuanza na Muhammad, bali ulikuwepo tangu zamani, tangu enzi za Ibrahim, Musa na Issa (Yesu), wakisema kuwa hao wote walikuwa Waislamu kwa maana ya “waliomtii Mungu”.

Hata hivyo, dai hili linapokaguliwa kwa historia na mantiki, linazua maswali mazito ambayo hayajapatiwa majibu ya kuridhisha mpaka leo.

MUHAMMAD HAKUKUTA HATA MUISLAMU MMOJA

Muhammad alipoanza kufundisha kile alichokiita Uislamu:

Hakuwahi kumkuta hata mtu mmoja aliyekuwa tayari ni Muislamu

Hakuna historia inayosema kulikuwa na:

Jamii ya Waislamu

Ibada za Kiislamu

Msikiti

Qur’an

Shahada ya Kiislamu

Swali la msingi:

Kama Uislamu ulikuwepo kabla ya Muhammad,

👉 Kwa nini Muhammad hakuwahi kukutana na hata Muislamu mmoja kabla ya kuanza kuhubiri?

DAI LA “UISLAMU ULITANGULIA” LINAKOSA MSINGI

Waislamu hudai:

“Ibrahim, Musa na Issa walikuwa Waislamu”

Lakini kihistoria:

Wafuasi wa Musa walikuwa Wayahudi

Wafuasi wa Issa walikuwa Wakristo

Hakuna hata maandiko ya kale yanayotaja:

Dini iitwayo Uislamu

Watu waliokuwa wakijiita Waislamu

Ibada za Kiislamu kabla ya Muhammad

Kama hao manabii walikuwa na ushawishi mkubwa duniani: 👉 Ni lazima kungekuwepo mabaki ya waumini wa Uislamu kabla ya Muhammad

Lakini: ❌ Hakukuwa na hata mmoja.

MUISLAMU WA KWANZA ALIKUWA BI KHADIJA

Historia ya Kiislamu inasema wazi:

Mtu wa kwanza kuingia Uislamu alikuwa Bi Khadija

Wa pili alikuwa Abu Bakr

Hakuna hata mmoja aliyekutwa tayari anaamini Uislamu kabla yao

Swali zito la kihistoria:

Kama Uislamu ulikuwepo tangu zamani, 👉 Kwa nini Bi Khadija awe Muislamu wa kwanza?

Hao “Waislamu wa zamani” walikwenda wapi?

WAFUASI WA MANABII WA AWALI WALIPOTEA WAPI?

Kama Musa na Issa walihubiri Uislamu kama inavyodaiwa:

Wafuasi wao walipaswa kuwa Waislamu

Lakini historia inaonyesha:

Wayahudi waliendelea kuwa Wayahudi

Wakristo waliendelea kuwa Wakristo

Hakuna rekodi hata moja ya:

Jamii ya Waislamu kabla ya Muhammad

Harakati za Kiislamu kabla ya karne ya 7

👉 Hii inaonyesha Uislamu haukurithiwa, bali ulianzishwa upya

UISLAMU NI DINI MPYA YA KARNE YA 7

Ukweli wa kihistoria unaonyesha:

Uislamu unaanza karne ya 7 huko Arabia

Mafundisho, sheria, Qur’an na ibada zote:

Zinaanza na Muhammad

Hazikuwepo kabla yake

Dai la kusema:

“Uislamu ulikuwepo tangu zamani”

👉 Ni jaribio la kurudisha nyuma historia, si ukweli wa kihistoria.

Kwa msingi wa historia na mantiki:

Muhammad hakurithi Uislamu, aliutangaza kwa mara ya kwanza

Hakukuwa na Waislamu kabla yake

Uislamu haukuwa dini iliyopo, bali ulianza na Muhammad

Dai la kuwa manabii wa awali walikuwa Waislamu halina ushahidi wa kihistoria

Ninatoa changamoto kwa Muislamu yeyote anayejiweza ajibu maswali haya kwa hoja, si kwa matusi:

❓ Kama Uislamu ulikuwepo kabla ya Muhammad:

Ulikuwa wapi?

Wafuasi wake walikuwa akina nani?

Kwa nini Muhammad hakuwahi kukutana na hata mmoja wao?

Kwa nini Bi Khadija awe Muislamu wa kwanza?
 
Dini inajifagilia balaa:
Ikishindwa inawatisha waumini:.
Sunan an-Nasa'i 4059
Ibn 'Abbas said:
"The Messenger of Allah [SAW] said: 'Whoever changes his religion, kill him.'"

Kuchukua Hadith moja bila muktadha na kusema “dini inatisha” ni udhaifu wa hoja.


Qur’an inasema wazi:


“Hakuna kulazimishwa katika dini” (Qur’an 2:256)

Mtume hakuwahi kumuua mtu kwa kubadili dini tu. Hadith hiyo ilihusu usaliti na vita, si imani binafsi.


Lakini kama tunacheza mchezo wa kunukuu bila muktadha, basi Biblia yenu ina amri za wazi za kuua waasi wa dini:


“Umuue bila huruma… umpige kwa mawe afe”
(Kumbukumbu la Torati 13:6–10)

“Mwanamume au mwanamke akiacha Mungu… auawe kwa kupigwa kwa mawe”
(Kumbukumbu la Torati 17:2–5)

“Usimwache hai yeyote apumue”
(Kumbukumbu la Torati 20:16)

“Lakini hao adui zangu wasiotaka nitawale juu yao, waleteni hapa mkawachinje mbele yangu”
(Luka 19:27)

“Msidhani nimekuja kuleta amani duniani; sikuja kuleta amani bali upanga”
(Mathayo 10:34)

“Waliodharau sheria ya Musa walikufa bila huruma”
(Waebrania 10:28–29)


Je, hiyo inamaanisha Ukristo ni dini ya mauaji? Hapana — kwa sababu tunajua muktadha.


Basi iwe haki hiyo hiyo itumike kwa Uislamu.


Hitimisho:
Hoja ya kunukuu sentensi moja bila muktadha ni propaganda, si elimu.
 
Back
Top Bottom