Uingereza Yamtimua Balozi wa Libya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uingereza Yamtimua Balozi wa Libya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by sekulu, May 3, 2011.

 1. sekulu

  sekulu JF-Expert Member

  #1
  May 3, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 934
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  UINGEREZA imemfukuza balozi wa LIBYA nchini humo kufuatia shambulio lililofanywa na kundi la watu katika ubalozi wa UINGEREZA mjini TRIPOLI nchini LIBYA. Waziri wa mambo ya nje wa UNGEREZA amesema kuwa Balozi wa LIBYA,Omar Jelban amepewa saa 24 kuondoka nchini humo. Waziri huyo wa mambo ya Nje wa UINGEREZA amelaani shambulio hilo lililofanywa kwenye ubalozi wa UINGEREZA nchini LIBYA pamoja na maeneo mengine ya mashirika ya kimataifa nchini LIBYA.
  Azimio la VIENNA linataka utawala wa GADDAFI kulinda maafisa wa kibalozi waliopo nchini kwake na kushindwa kufanya hivyo serikali itakuwa imekiuka kanuni na taratibu za kimataifa zinazoitaka kufanya hivyo.
  Wakati huo huo Umoja wa Mataifa unatarajia kuwaondoa wafanyakazi wake wa kimataifa kutoka mji mkuu wa nchi ya LIBYA, TRIPOLI kufuatia mashambulio yanayofanywa na makundi ya watu wanaovamia ofisi za umoja huo.
  Majengo ya ofisi za Umoja wa Mataifa pamoja na majengo ya wafanyakazi wengine wa kigeni yamekuwa yakivamiwa na makundi ya watu wenye hasira kufuatia shambulio lililosababisha kifo cha motto wa kiongozi wa LIBYA, Kanali MUAMAR GADDAFI.
  Habari zinasema kuwa maafisa wa Umoja wa Mataifa nchini LIBYA wamesema kuwa watawaondoa wafanyakazi hao wa kgeni na kwamba uamuzi huo utawekwa wazi wiki ijayo.
  Source Hapa
   
Loading...