Uingereza yaitwisha serikali zigo la rada | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uingereza yaitwisha serikali zigo la rada

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Aug 11, 2012.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Aug 11, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,768
  Likes Received: 83,104
  Trophy Points: 280
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #FFFFFF"]
  [TABLE]
  [TR]
  [TD]Uingereza yaitwisha serikali zigo la rada


  na Edson Kamukara
  Tanzania Daima

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  [TABLE]
  [TR]
  [TD]WAKATI Serikali ya Rais Jakaya Kikwete, ikisema kuwa hakuna rushwa kwenye kashfa ya ununuzi wa rada kutoka nchini Uingereza, nchi hiyo imeweka bayana kwamba uamuzi wake hauizuii Tanzania kuwapeleka mahakamani na kuwashitaki watuhumiwa wa ufisadi wa sakata hilo.

  Msimamo wa Uingereza unakuja siku chache baada ya Rais Kikwete na mawaziri wake, Benard Membe wa Mambo ya Nje na Mathias Chikawe wa Utawala Bora, kudai kuwa serikali hiyo iliyokuwa ikichunguza kashfa hiyo imebaini kuwa hakukuwa na rushwa katika ununuzi wa rada.

  Hata hivyo, katika tamko lake la Agosti 6 mwaka huu, Uingereza kupitia ubalozi wake nchini, iliweka bayana kuwa bado iko pamoja na Serikali ya Tanzania katika kusaidia mapambano dhidi ya ufisadi.

  "Serikali ya Uingereza daima imekuwa wazi kuwa itashirikiana na mamlaka za Tanzania katika uchunguzi na kuwashtaki kwa kutumia sheria za Tanzania wale wote waliohusika katika ufisadi wa rada ya BAE System," ilisomeka sehemu ya taarifa hiyo.

  Kwamba Ubalozi wa Uingereza nchini unajua kuwa vyombo vya habari vimelikomalia suala la rada juu ya kama kuna uwezekano wa kuchukua hatua za kisheria kuhusiana na sakata zima.

  "Serikali ya Uingereza inapenda kuweka wazi kuwa mapatano kati ya Ofisi ya Uingereza inayoshughulika na Ufisadi Mkubwa (SFO) kwa upande mmoja na BAE System kwa upande mwingine, hayana nguvu za kisheria katika nchi zingine, na kwa maana hiyo hayaizuii Serikali ya Tanzania kuwapeleka mahakamani na kuwashitaki wanaotuhumiwa na ufisadi huo," ilisema.

  Kwamba ripoti ya Kamati ya Bunge la Uingereza inayoshughulikia Maendeleo ya Kidunia (IDC) kuhusu ufuatiliaji wa jinai ya wizi wa fedha ya Novemba 15, 2011, iliunga mkono wazo la Serikali ya Tanzania la kutaka kuwapeleka mahakamani watu wote waliojihusisha na wizi unaohusiana na manunuzi ya kifisadi ya rada.

  Vilevile, IDC inaona kuwa ni jambo jema kuwapa cha mtema kuni watu wote wanaojihusisha na wizi wa mamilioni ya fedha za umma.
  Kwa mantiki hiyo, Uingereza inaendelea kuahidi kuwa kila wakati itakuwa tayari kufanya kazi bega kwa bega na Serikali ya Tanzania katika kupambana na ufisadi kwa ujumla wake.

  Mbunge wa Bariadi Mashariki, Andrew Chenge (CCM), kwa muda mrefu amekuwa akitajwa ndani na nje ya chama chake kuhusika na kashfa ya ununuzi wa rada kutoka Kampuni ya BAE System.

  Chenge, ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Fedha na Uchumi, anatajwa kuhusika kutoa ushauri wa kisheria wakati huo akiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ushauri ambao unatajwa kuzingatiwa katika hatua za uamuzi.

  Mwingine anayehusishwa na kashfa hiyo ni aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT) Dk. Idriss Rashid.
  Pamoja na hao, wanatajwa wafanyabiashara wenye asili ya India, lakini ambao wanaishi/walipata kuishi Tanzania, Tanil Somaiya, ambaye alikuwa akimiliki kampuni ya uwakala wa simu ya Shivacom na Sailesh (Shailesh) Vithlani kuwa watu wa kati wa biashara hiyo.

  "Kama Uingereza waliochunguza kashfa hiyo wamefika mahala wanasema kulikuwa na makosa ya uchapaji tu, mtu wenu mnamfikisha mahakamani kwa ushahidi upi?" alihoji Rais Kikwete wakati akizungumza na wahahariri wa vyombo vya habari hivi karibuni.

  Mchakato wa ununuzi wa rada iliyoligharimu taifa dola milioni 46, unatajwa kuanzia kwa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Tony Blair kuwa ndiye aliyemshawishi aliyekuwa Rais wa Tanzania wakati huo, Benjamin Mkapa, kununua rada hiyo kutoka Kampuni ya BAE-Systems.

  Wakati huo aliyekuwa Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa, Clare Short, alikataa katakata Tanzania, moja kati ya nchi masikini kabisa duniani, kutumia kiasi hicho kununua rada.

  Hata hivyo, chenji hiyo ya rada, zaidi ya sh bilioni 75 zimerejeshwa nchini baada ya hati ya makubaliano baina ya pande zinazohusika kusainiwa.


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Aug 11, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,768
  Likes Received: 83,104
  Trophy Points: 280
  Rais wa nchi anapoamua kuwadanganya Wananchi wake ili awakingie kifua mafisadi wenzake basi hakuna sababu ya yeye kuendelea kuwepo madarakani. Dr Slaa hakukosea alipotoa kauli kwenye kampeni za uchaguzi wa Taifa 2010 kwamba "kumchagua" Kikwete katika uchaguzi ule ni "Janga la Taifa."
   
 3. O

  Ogah JF-Expert Member

  #3
  Aug 11, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Mkuu BAK.......... heshima mbele..........hivi ulitegemea JK ajipige "risasi" mwenyewe?.......si umeona kule kwa Prof Mahalu!...mambo yalivyokwenda......au unataka uambiweje.......kuwa "Vyombo vyetu vya sheria vinafanya kazi nzuri sana"!
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Aug 11, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,768
  Likes Received: 83,104
  Trophy Points: 280
  Mkuu Ogah...Mie nataka aachie ngazi kwa sababu ameshindwa kuliongoza Taifa. Tusimuachie mtu ambaye ameshindwa kuliongoza Taifa kuwepo madarakani ili aendelee kukingia kifua mafisadi wenzake. Tumshinikize kwa nguvu zetu zote ili aachie madaraka. Hili la hao wanaojiita viongozi kuendelea kubaki madarakani pamoja na kuvurunda kila kukicha ni tatizo kubwa sana nchini kwetu ambalo linaendelea kuiangamiza nchi yetu.

   
 5. a

  armanisankara JF-Expert Member

  #5
  Aug 11, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 283
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  serikali dhaifu haiwezi kua na maamuzi magumu.
   
 6. W

  Wimana JF-Expert Member

  #6
  Aug 11, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 2,453
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 145
  Serikali ya CCM ni genge la wezi waliolishana yamini kuwa ni mwiko kusalitiana.
  Mwisho wao umekaribia, ukombozi u karibu.
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Aug 11, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,768
  Likes Received: 83,104
  Trophy Points: 280
  UK MPs urge Tanzania to prosecute over bribery allegations in BAE deal

  Parliament's international development committee says individuals should be made to answer in court about payments in BAE Systems' sale of $44m air traffic control system

  Frederika Whitehead

  [​IMG]
  The Tanzanian government plans to spend the $46m reparation money from BAE on education. Photograph: Tony Karumba/AFP/Getty Images


  The UK parliament's international development committee has called on Tanzania to seek prosecutions for bribery in relation to a $44m (£28m) defence deal with BAE Systems. It says Tanzania should bring individuals to court to answer allegations that corrupt payments were made during the sale of a military air traffic control system.

  In 2010 BAE was fined for concealing payments of $12.4m to Sailesh Vithlani. BAE claimed the payments to Vithlani were for lobbying and marketing. After an investigation by the Serious Fraud Office (SFO), BAE was ordered to repay the full value of the contract to the people of Tanzania.

  Last month, the Tanzanian high commissioner in London wrote reassuring the committee of his country's "intention to ensure that individuals involved in this case face justice".

  The chairman of the committee, Malcolm Bruce, said this case was particularly important to the development committee because "corruption undermines the rule of law and hampers development – it cannot be tolerated". He added that the committee "will continue to monitor developments in relation to proceedings against individuals in Tanzania".

  In a report published on Wednesday, the committee recommends that future settlements made by the SFO – as a result of plea bargaining in relation to financial crimes – should be drawn much more tightly than the agreement concluded with BAE. Future settlement agreements should be explicit about what the company is required to do and by when.

  The military radar deal went through just weeks after Clare Short, the then development secretary, had negotiated a big increase in aid to Tanzania to fund universal free education. Tanzania had no air force at the time and was in receipt of debt relief. GDP per head was just £465.

  Worried that the extra aid she had negotiated would be immediately swallowed up to pay BAE's bill, Short attempted to block the deal, but Tony Blair, who was prime minister at the time, intervened and it went ahead.

  The UK's Department for International Development (DfID) and the Tanzanian government plans to spend the $46m (£29.5m) reparation on education. (BAE has been asked to pay back more than the amount in the original deal). The money will be used to buy 4.4m school textbooks, 192,000 desks, 1,196 teachers' houses and 2,900 pit latrines.

  A spokesperson from the campaign group Global Witness welcomed the committee's report but said there were still "a lot of unanswered questions on this story".
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  Aug 11, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,768
  Likes Received: 83,104
  Trophy Points: 280
  Letter from the Tanzanian High Commissioner to the Chair of the International Development Committee

  I thank you for your letter of 10 October 2011, in which you kindly informed me of the BAE's decision to make a payment in full to the Government of Tanzania.

  I have subsequently communicated that decision to the relevant authorities in Dar es Salaam. I also agree with you that all those involved in corruption surrounding the BAE radar sale to Tanzania be brought to face justice. I believe this will serve as an assurance to our people that our governments are committed in tackling the scourge of corruption worldwide.

  On our part, the Government of Tanzania has already stated its intention to ensure that individuals involved in this case face justice.

  None the less, I have taken upon myself to inform the relevant authorities in Tanzania of your concern given the crucial role played by your Committee on this matter.

  17 October 2011
   
 9. Masiya

  Masiya JF-Expert Member

  #9
  Aug 11, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 3,691
  Likes Received: 2,123
  Trophy Points: 280
  Utawala bora wa awamu ya nne ndio huu. Ndani ya bunge jamaa wameula. CCM kweli kiboko.
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Aug 11, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,768
  Likes Received: 83,104
  Trophy Points: 280
  Ndio matatizo ya kuwa na Rais fisadi ambaye siku zote hukimbia majukumu yake na kushindwa kufuata utawala wa sheria na hivyo kushindwa kutetea maslahi ya nchi.

   
 11. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #11
  Aug 11, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160

  [​IMG]

  [​IMG]
   
 12. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #12
  Aug 11, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Hapo Kikwete Rais wetu mpendwa anaendelea kutamba na misafara ya kimataifa akichoma mapesa ya walipa kodi kwenye mahoteli ya kifahari ya kimataifa wakati watoto hawa wanataabika vumbini kupata elimu. Safari moja tu ya Rais Kikwetekwenda nchi za nje ingeweza kukjenga madarasa zaidi ya matano vijijini.

  [​IMG]

  [​IMG]
   
 13. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #13
  Aug 11, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Zina maneno ya kueleza zaidi kwani picha zinajieleza


  [​IMG]

  [​IMG]
   
 14. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #14
  Aug 11, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,768
  Likes Received: 83,104
  Trophy Points: 280
  Halafu mimi tabia yake ya kukaa kimya kwenye maswala nyeti inanikera sana. Kwa mfano hajatia kauli yoyote kuhusiana na government officials ambao kwenye Bank accounts zao kule uswiss wamekutwa na $200 million. Na hajatia neno kuhusiana na kauli ya Waziri mpya wa Nishati na Madini kwamba Makampuni ya uchimbaji dhahabu yaanze mara moja kulipa kodi ya 30% bila kutoa excuses za aina yoyote ile vinginevyo wafungashe virago vyao haraka sana.
   
 15. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #15
  Aug 11, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Haya wameumbuka!!
   
 16. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #16
  Aug 11, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,768
  Likes Received: 83,104
  Trophy Points: 280

  Mie nimechoka na hiyo barua ya balozi wetu UK hapo juu sijui kwa nini haina jina la balozi huyo. Hili lilifanywa makusudi au Guardian hawakuona umuhimu wa kuweka jina la balozi huyo? Ila naamini kabisa hawa Guardian jinsi walivyo makini katika kuhakikisha authenticity katika habari zao hawawezi kuliacha jina la balozi muhusika.
   
 17. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #17
  Aug 11, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,768
  Likes Received: 83,104
  Trophy Points: 280
 18. N

  Nhundu Member

  #18
  Aug 11, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 41
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu umenikumbusha mbali sana na picha za shule zetu nchini pindi nasoma shule za aina hiyo kwa wakati huo na nimeweza kupenya kwa mbinde na kusoma kwa mgomo hadi kumaliza elimu yangu ya chuo kikuu lakini bado tena kazini nako hali ni ileile kama ya shule ya msingi, sekondari na chuo kikuu hakueleweki mshahara kidogo.Hivi viongozi wetu wana kipi cha kujivunia katika sekita ya elimu nchini ukiachilia shida na matatizo wanayoyapata watoto wetu wa ngazi ya chini, sekondari na vyuo vikuu? Chenji ya RADA iko wapi maana walisema inapelekwa kuboresha shule nchini je shule za aina hiyo hawazioni au hawajafika huko?
  MUNGU EE MWENYEZI TUSAIDIE NA MATATIZO HAYA KWA NINI NI SISI TU JAMANI TANGU UTOTO WANGU HADI LEO HII MTU MZIMA SASA? Watanzania amukeni bwana?
   
 19. Manyi

  Manyi JF-Expert Member

  #19
  Aug 11, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 3,256
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Siku si nyingi wataumbuka tu, waache walindane, dola ikiwa mikononi mwa wazalendo ndo utakuwa mwisho wao, yale ya Chiluba wa Zambia na wengine wengi yatawakuta tu, time will tell and events will actually happen in real time!
   
 20. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #20
  Aug 11, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,127
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Ni vigumu kutegemea maamuzi ya aina ulioitaja kutoka kwa viongozi wa Tanzania. Uwajibikaji sio utamaduni wao. Kilichobaki kwetu ni kuwaumbua "shame them" mpaka mwisho.
   
Loading...