Uingereza yaichoma tena serikali

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,268
33,040
UINGEREZA imeendelea kuiweka serikali kwenye hali ngumu baada ya kuieleza kuwa tabia ya kutegemea misaada ya wahisani pekee kwa shughukli za maendeleo hakitaisaidia nchi kujikwamua kiuchumi, ikiwa ni siku chache baada ya kusomwa kwa bajeti ambayo inaonyesha nakisi ya Sh5 trilioni.

Bajeti hiyo ya mwaka 2010/11 ni ya Sh11.1 trilioni na inaonyesha kuwa Sh6 trilioni zitapatikana kutoka vyanzo mbalimbali vya ndani wakati Sh5 trilioni zitatokana na mikopo na misaada ya wahisani ambao tayari wamezuia Sh297 tyrilioni katika bajeti hiyo wakiishinikiza serikali iharakishe mageuzi katika usimamizi wa fedha za umma, ikiwa ni pamoja na kudhibiti matumizi yake.

Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya kuzaliwa Malkia Elizabeth II wa Uingereza mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Diane Corner alisema Tanzania inapaswa kutambua kuwa misaada si nyenzo pekee inayoweza kuiletea maendeleo.

Alisema kuwa matumizi sahihi ya fedha za misaada ni suala kuu katika mfumo wao wa misaada ili kuhakikisha ya kuwa wanafanikiwa kupata dhamani halisi ya kila fedha inayotolewa kwa ajili ya misaada.
"Uwazi bora zaidi si tu kuwa utawaonyesha walipakodi wa Uingereza jinsi fedha zao zinavyowasaidia watu wenye shida, bali pia utawawezesha wananchi wanaosaidiwa kutambua ni kiasi gani wanachosaidiwa na hivyo kuziwajibisha serikali zao juu ya misaada hiyo. Pia uwazi ni silaha madhubuti dhidi ya rushwa," alisema.

Alisema kuwa wanafahamu fika kuwa misaada si nyenzo pekee ya maendeleo na hivyo nchi zinahitaji ukuaji wa uchumi unaotokana na sekta binafsi.
“Inatakiwa uelewa mkubwa kuwa nchi zinahitaji ukuaji wa uchumi unaotokana na sekta binafsi. Uingereza itajikita katika kuboresha mazingira ya biashara, ili biashara iwe ya soko huria, ya haki na yenye uwazi badala ya biashara yenye kuziba fursa za kibiashara,” alisema.

Alisema Uingereza itaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania kuboresha mazingira ya kufanya biashara humu nchini kwa kuondoa vizingiti vinavyoyazuia makampuni ya ndani na ya nje kukua kibiashara, hivyo kutoa ajira na kusaidia kukua kwa uchumi wa taifa.

“Nina fahari kusema nchi ya Uingereza ndiyo inayoongoza kwa uwekezaji nchini Tanzania kuliko nchi nyingine yoyote. Pia leo ninayo furaha kubwa kutangaza kuwa hata sherehe hii imedhaminiwa kwa pamoja na makampuni mbalimbali ya Uingereza ambayo yamewekaza hapa Tanzania,” alisema.

Aliongeza kuwa wingi na ubora wa bidhaa za makampuni ya Uingereza hapa nchini ni uthibitisho wa wazi ni kuwa ni kiasi gani Uingereza ni mshirika muhimu katika kukuza uchumi wa Tanzania.
Alisema Uwepo wa makampuni mengi kutoka uingereza ni uthibitisho wa tumaini la kukua kwa uchumi wa Tanzania kutoka kwenye umasikini kuelekea kwenye mafanikio.

Balozi huyo alisema Tanzania ina kila sifa zote za kuiwezesha kuondokana na umasikini, kwa kuanzia na rasilimali watu ambayo inaendelea kuelimishwa kufikia viwango vya juu, kiu ya kupata elimu ambayo inadhihirishwa na jinsi umati wa watu wanavyofurika kutafuta fursa za masomo Uingereza. Alisema kila mwaka kuna takriban Watanzania 3000 ambao hupata elimu katika kituo cha British Council.

Kuhusu uchaguzi mkuu, balozi huyo aliitaka Tanzania kutupia jicho upande wa Zanzibar na kufuata nyayo za siasa za serikali ya mseto kama ilivyofanyika nchini Uingereza ili kumaliza mkwaruzano wa muda mrefu.
“Tunampongeza Rais Amani Abeid Karume na katibu mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad kwa maridhiano na pia tunapongezajuhudi za Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuhakikisha hili linafanikiwa,” alisema.
Uchaguzi huru na wa kidemokrasia, huwapa fursa wananchi kuamua serikali ya kuwaongoza ambayo wanaitaka, alisema na kuongeza kuwa hilo litajenga amani, utulivu na ukomavu wa kisiasa ambao ni nguzo muhimu kwa ustawi wa nchi na maendeleo.

Pia alisema Tanzania inahitaji kutupia macho mbali zaidi na upeo wa mipaka yake na kujionea jinsi mihimili mikubwa ya kiuchumi ilipofikia. Aliongeza kuwa mafanikio hayaji kwa serikali kulinda masoko yake, bali kwa kufungua milango kwa sekta binafsi kushika uchumi wa nchi kwa kutumia nguvu ya soko huria na serikali kubakia tu kama mratibu.

Baadhi ya makampuni yaliyowekeza hapa nchini kutoka uingereza ni pamoja na CMC motors ambayo ni kampuni ya magari ya Landrover. Kampuni inayojishughulisha na biashara ya majengo ya Knight Frank na Songas ambayo inazalisha umeme wa gezi.

Nyingine ni benki ya Standard Chartered, ambayo ni moja kati ya mabenki makubwa duniani na Unilever ambayo inamiliki viwanda jijini la Dar es Salaam na Arusha. Pia inamiliki mashamba ya chai mkoani Iringa.
Chanzo> Uingereza yaichoma tena serikali

Tatizo hili la Serikali yetu Kuomba omba kwa Wafadhali litakwisha lini jamani? Kila Mwaka kwenye bajeti yetu utasikia Waziri wa Fedha anasema Wahisani watatusaidia kiasi fulani cha fedha,haya matatizo ya kungojea mpaka tusaidiwe na Wahisani yatakwisha lini Wakuu?Itafika wakati Wafadhili tuko nje watachoka kutusaidia na hiyo ipo karibu sio mbali kuanzia sasa tungojeeni mwisho wake wa kuomba omba.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom