ACT Wazalendo
JF-Expert Member
- May 5, 2014
- 620
- 1,543
Akiwa Katika Mkutano wa Rushwa Duniani ( Global Corruption Summit ) uliofanyika Jijini London Juzi Alhamisi, Mei 12, Mkutano ambao Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu Kassim Majaliwa alihudhuria, Waziri Mkuu wa Uingereza, Bwana David Cameron wa Uingereza alisema yafuatayo:
"We are also consulting on reversing the burden of proof, so that if we suspect people of using stolen money to buy property we can force them to prove they accumulated their wealth legitimately – or they will face having it stripped from them by a court".
Tafsiri “Tunajipanga kuubadili utaratibu wa uthibitisho ili kama tunawahisi watu kutumia pesa za kifisadi kununua mali tuwalazimishe kuthibitisha kuwa wamepata mali hizo kihalali. La sivyo, mali hizo zitataifishwa na mahakama”.
Maelezo ya Waziri Mkuu wa Uingereza yanaweza kupatikana kupitiahttp://www.theguardian.com/…/fight-against-corruption-begin…
Chama Chetu Cha ACT Wazalendo, ambacho kimejitanabaisha Kuwa Chama kinachopinga Rushwa Na Ufisadi Nchini kimefurahishwa Na Hatua Hii ya Vita ya Kupiga Vita Rushwa, Ufisadi Na Ukwepaji Kodi kupata Mwitikio wa Kimataifa.
Ilani ya ACT Wazalendo ya Mwaka 2015, inasisitiza Juu ya Umuhimu wa Kuimarisha Mifumo ya Kupambana Na Rushwa Nchini, Ibara ya 6.8 (V) ya Ilani Husika inasema yafuatayo:
"Kubadili mfumo wa kisheria kwenye masuala ya rushwa na biashara haramu za madawa ya kulevya kwa kugeuza uthibitisho wa mali halali kutoka kwa Jamhuri kwenda kwa mtuhumiwa (Reverse burden of Proof)".
Chama Chetu kimefarijika Sana kwamba wito wetu huu umepata Mwitikio wa Kimataifa, tunaisihi Serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nayo kufuata Nyayo hizi, hasa Kwa Kuwa aliyekuwa Mgombea wetu wa Urais, Mama Anna Mghwira alikabidhi ilani yetu Kwa Rais John Magufuli.
Ado Shaibu
Katibu wa Kamati ya Itikadi, Mawasiliano ya Umma Na Uenezi
ACT Wazalendo
Mei 14, 2016