Ripoti ya CAG inaonesha ACT WAZALENDO wanaongoza kwa Ufisadi Zanzibar. Allah Wasaidie Wazanzibar

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
Salaam Wakuu,

Zitto Kabwe na Chama chake cha ACT WAZALENDO, kimeshindwa kujitofautisha na CCM baadaya Ufisadi mkubwa kutokea kwenye Wizara Wanazoongoza.

Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK), waligawana Madaraka na Vyeo huko Zanzibar.

Mfano: Nassoro Mazrui ambaye ni Naibu Katibu mkuu wa Chama Cha ACT-Wazalendo (Zanzibar) aliteuliwa na rais Mwinyi Kuwa Waziri wa Afya,Ustawi wa Jamii,Wazee,Jinsia na Watoto Zanzibar. Lakini Wizara hiyo imekuwa ya hovyo kwa Ufisadi.

CAG-ZANZIBAR alisema Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa alifariki wiki moja baada ya kutakiwa kuthibitisha kwa maandishi uhalali wa deni la Tsh. Bilioni 4.9

Hii ni baada ya kubainika kuwa deni halali ni Tsh. Milioni 886.68. Hii Wizara ipo chini ya ACT WAZALENDO.

Dkt. Othman Abbas ameshauri Serikali kuanzisha mfumo mpya wa upokeaji dawa na usambazaji ili kuepuka kupokea dawa zilizopita muda na zisizofaa kwa matumizi ya Afya ya Binadamu. Wanao pokea wapo chini ya ACT WAZALENDO.

Sijasikia Mwenyekiti wa ACT WAZALENDO Babu Duni wala Zitto Kabwe akitolea tamko Madudu haya. Wameufyata.

Niwatofautisheje ACT WAZALENDO na CCM?

Je, Watapata jeuri ya kuwakosoa CCM tena?

Zitto Kabwe ukimkuta anaongelea Ufisadi wa Magufuli, anaongea hadi povu linajaa mdomoni, hadi watu wanaomsikiliza wanajifunika miamvuli kwa Mvua unavyonyesha.
20220829_153244.jpg

Waziri Nassoro Mazrui mwenyewe ndo Huyu🤣🤣
 
Kama ukweli ndio huu basi wapiga kura wa nchi hii tunatumika vibaya sana na hawa wanasiasa.

Wanawadanganya wanaenda kupeleka agenda zao kwenye serikali kupitia huo muungano wao [SUK] kumbe jamaa wana mawazo yao tofauti.

Wameingia makubaliano rasmi na serikali ya CCM, hata wakiharibu sijui ni kwa vipi watachukuliwa hatua, wanasubiri hao wezi washughulikiwe ndani ya chama lakini kama walikuwa na baraka toka kwa viongozi wakuu wa chama watashughulikiwaje?

Wezi wanaoneana aibu, wizi unaendelea, matokeo yake wanaoumia ni walipakodi wasio na chochote, serikali ya aina hii haina maana ya kuwaongoza watu.
 
Back
Top Bottom