Uingereza kuanzisha bank ya mbegu za kiume

Uingereza kuanzisha bank ya mbegu za kiume

Chizy Za kitaa

Senior Member
Joined
Jan 7, 2014
Posts
167
Reaction score
13
140630132625_sperm_512x288_spl_nocredit.jpg

Inaelezwa kuwa benki ya mbegu za kiume itatatua haja za uzazi

Benki ya Taifa ya mbegu za kiume inatarajiwa kuanzishwa nchini Uingereza kuondokana na tatizo la upungufu wa mbegu hizo.
Wapenzi wa jinsia ya kiume na kike , wale wa jinsia moja pia wanawake wasio na wenza watanufaika na huduma hii mpya ambapo kutoka jamii zisizofahamika watakuwa na uwezo wa kuchagua wachangiaji kutoka katika jamii nyingine

Benki hii itakayosimamiwa na Mfuko wa Taifa wa Gamete na Hospitali ya Wanawake ya Birmingham itafunguliwa mwezi Oktoba.
Mradi huu umetengewa paundi 77,000 na Idara ya Afya nchini Uingereza.

Kituo hiki kitakuwa katika hospitali ya wanawake mjini Birmingham ambacho kitakuwa kikihifadhi mbegu hizo.

Hivi sasa kumekuwa na upungufu wa wachangiaji wa mbegu za kiume nchini Uingereza hasa katika hospitali za taifa,huku kukiwa na ongezeko la uhitaji, hospitali hizo zikitibu tatizo hilo linaloelezwa kuwa kubwa nchini humo.

Mfuko huo umesema una matumaini kuwa uwepo wa benki hiyo utapunguza idadi ya wagonjwa wanaojiweka katika hatari kwa kutafuta huduma hii bila kufuata taratibu.


Chanzo: BBC
 
Welcome single mom era! Hawa wanaua uhusiano wa baba na mtoto unabaki na wa mama na mtoto. Sawa; lakini baadae sio wanaanza business ya DNA tena; kuanza kutafuta nani ni baba wa nani! Hili iwe kitu cha haki basi hao watoto wazalishwe kwenye chupa; hawamjui mama wala baba; siku wakikua wakalianzisha direct waivae government......
 
Itakuwa na ATM? Je wahudumu watakuwa wanaupokea mzigo mkononi au mnaingia chumba cha faraga anaku~mastbet

hahahahahahahaha........na card zake zitakuwaje!nimecheka sana.labda ufatilie katika hiyo bank nyingine iliyopo hospitali kuu,unaweza pata majibu.hahahahaha
 
Welcome single mom era! Hawa wanaua uhusiano wa baba na mtoto unabaki na wa mama na mtoto. Sawa; lakini baadae sio wanaanza business ya DNA tena; kuanza kutafuta nani ni baba wa nani! Hili iwe kitu cha haki basi hao watoto wazalishwe kwenye chupa; hawamjui mama wala baba; siku wakikua wakalianzisha direct waivae government......

mkuu,kuna movie moja inaitwa Delivery Man,kama haujaiyona,nakusihi itafute uiangalie.
 
Itawafaa sana siku za usoni...maana wanatukuza ushoga na ulesbian...else kizazi chao kitapotea...lazima watunze akiba benki...
 
not everyone who work bank; means it it the very same bank which the usual people understand.
even in blood bank it is only refers to those who collect blood only.
 
Back
Top Bottom