Uimara wa CCM ya Rais Magufuli na Vita ya kupata nafasi ya ugombea urais ndani ya CHADEMA unavyomtesa Tundu Lissu.

FPT

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
1,201
1,839
Kuna mambo duniani yanafikirisha na kutafakarishi sana bongo za watu hasa suala zima la vita hasa ile vita ya madaraka. Kikawaida binadamu huwa anatafuta heshima kupitia mamlaka ya kufanya maamuzi kwa ajili ya wengine. Katika kutafuta mamlaka haya kunatokea vita ya ndani na ya nje ambayo muhusika anatakiwa kuikabili. Hali hii anakumbana nayo Tundu Lissu, anahangaika kutafuta nafasi ya kuchaguliwa na CHADEMA kama vita ya ndani na hapo hapo anatafuta huruma ya kuitoa CCM madarakani kama vita ya nje.

Mchakato na utaratibu wa kumpata mgombea urais ndani ya CHADEMA unatia kizunguzungu na haupo wazi kwa wanachama zaidi ya kueleweka kwa baadhi ya wajumbe wa kamati kuu ya CHADEMA hivyo kufanya baadhi ya wanachama kujipanga kivyao ili kuleta hali ya kukubalika na kushinikiza kupewa nafasi ya kugombea. Hali hii ndio inamuumiza kichwa Tundu Lissu na kumfanya ajiulize nitoke vipi na hivyo anatengeneza mazingira ya kushawishi na kushinikiza kupendekezwa kwa ugombea.

Anachofanya Tundu Lissu ni 'cheap politics' kwa sababu kwa tamaa yake hiyo anatumia mgongo wa kuichafua serikali kwa kufanya mambo ambaye kwake yeye hana ushahidi wa uhusika wa moja kwa moja wa serikali. Hata kama nia na dhamira ni urais lakini kwa Tundu Lissu ameonekana kukosa nguvu ndani ya CHADEMA hivyo kuitafuta nguvu hiyo kwa kushinikiza na iwe ngumu kwa chama chake kushindwa kumkata kwa kuhofia chama kukosa mvuto wa kisiasa.

Sote tunatambua nguvu, mamlaka na Uwezo wa Lowassa ambaye ipo CHADEMA. nguvu ya Lowassa haimuwezeshi Tundu Lissu kufurukuta hata kidogo wakati wa mchakato wa kumpendekeza mgombea kama utakuwepo. Mchakato huo Tundu Lissu hana imani nao kwa kuhofia kutofuatwa au kushindwa kwake ukifanyika hivyo anajijengea umaarufu wa kuushinikiza ufanye kazi kwa kadiri ya anavyotaka yeye. Upinzani mwingine ambao Lissu anauona kama kizingiti ni uwepo wa Lazaro Nyarandu ambaye naye mara nyingi ameonesha nia ya kuomba ridhaa ya kugombea kupitia CHADEMA.

Haya yote yanafanyika kwa sababu Tundu Lissu anaamini kuwa CCM chini ya Mwenyekiti wake taifa Ndg. Dkt John Magufuli imekuwa imara sana kuliko kawaida hivyo kuna hatihati CHADEMA ikampa nafasi Lowassa tena ambaye anaonekana kuwa na nguvu wa kupambanishwa na Magufuli .

Pia, siasa nyepesi za upinzani kunamfanya Tundu Lissu aamini kuwa anaweza kuiondoa CCM kwa kupigiwa kura za huruma. Huu ni mtazamo hasi na wenye kukosa mashiko kwa sababu umaarufu na uwezo wa CCM kurudi tena madarakani umeongezeka maradufu kwa kuchagizwa na umakini wa Rais Magufuli katika kutekeleza Majukumu yake na uongozi imara.

Watanzania wameamka sana, wanaona kazi za rais Magufuli na kujitoa kwako na pia wanaona mabadiliko makubwa ya CCM katika kuisimamia serikali na ushiriki wa CCM katika kutatua matatizo ya wananchi wanasema CCM ni chaguo langu la kwanza kwa sababu Rais Magufuli ana dhamira ya dhati. Hofu na mtetemo wa Tundu Lissu juu ya CCM hii ni kukosa kuungwa mkono na wananchi hivyo anaona bora azushe na kupotosha ili asipoteze mvuto wa kisisasa.

Kwa Tundu Lissu hii kwake ni vita ya madaraka amabyo anaiona kutokea ndani ya chama chake na nje ya CHADEMA na hivyo kutumia kila silaha kupambana nayo. silaha hizo ni uzushi, upotoshaji na ulaghai ili aungwe mkono. Silaha hizo zimekosa mashiko kwa sababu Rais Magufuli ameonesha ni mkweli na dhamira ya kweli na anahitaji kuungwa mkono na watu wote wanafanya hivyo. CCM na Magufuli ni kisiki cha mbuyu kilichoota juu ya nyumba ya chadema hakiwezi kung'oka bila nyumba kuathirika.

na Karlo Mwilapwa
 
Pole sana na utaendelea kuweweseka hivyohivyo.
Labda tuanze na 'let's say waliomshambulia hawajulikani na Jiwe hakuhusika kwa namna yoyote ile'.
1) Ni sahihi kwa serikali kukaa kimya juu ya sintofahamu ya CCTV camera za lile eneo aliloshambuliwa Lissu? Zinahitajika printout watu wa'zoom picha hizo ili sura za walenga shabaha zibainike, hiyo itamsafisha kila anayeshukiwa wrongly.
1) Kama anaishuku serikali kwa sababu anazozijua yeye kuna kosa gani kulalamika kule anakoona atapata msaada(hata kama hatopata matokeo anayoyatarajia)? Ni kazi ya serikali kujisafisha kwa kufanya upelelezi na kukamata wahusika, hiyo itategemea kama ni kweli hawahusiki na kama wana nia ya dhati ya kukamata wahusika.

Hizo blah blah nyingineza ki'politics za nani atagombea na nani hagombei na kwa sababu zipi zinawahusu wenyewe lakini hata tulio mbali tunapata habari nyingi za huko Tz, huo mgogoro unaojaribu kuutengeza ki ukweli haupo(sijasema hautakuwepo) na wala Tundu Lissu hajasema anataka kugombea bali amesema kama chama chake kitampitisha he is ready for the task, usimlishe maneno.

Suala ya ushawishi alio nao ndani ya chama chake,just get ready for the nightmare.
 
Back
Top Bottom