Uhusiano wangu kimapenzi na "Hamida"

@JBourne59 Thanks for Sharing this Big Bro. Nasema kuna vingi nimepata asee ila kimoja kikubwa zaidi ni hiyo screening ya waarabu waliyokufanyia ili tu kujiridhisha kuwa unafaa kumuoa binti yao ama ndugu yao Aisee ni zaidi ya Interview Ya TRA ama BOT .

Napenda niseme kwamba pamoja na ubaguzi wa wenzetu katika maswala haya ila kwa namna fulani ulileta Revolution kubwa sana kifikra kuwa hayo mambo ya Ubaguzi hayana nafasi katika maisha binadamu wote sisi ni sawa japo siyo sawa sawa

Ningrpenda kujua vipi ndugu wa Mama yetu Hamida (Uarabuni) vipi bado wanaendelea kuwapa Ushirikiano mpaka sasa?

Nimejifunza mengi Upande wa Dini the way ulivyo kuwa una make progresses katika kujifunza Dini ni Exceptional kwa kweli. Yaani hata kama mtu kama angekua hajui Uislam ukoje kwa kupitia tu hii thread yako inatosha kabisa apate picha ya Dini ikoje na n.k ni somo tosha kabisa (Umewaacha mbali hata wale ambao ni Muslims by birth kwa kuijua dini na kuizingatia maelekezo yake) kwa hili nakupa hongera sana Mkuu.

Vipi una utaratibu wa kusoma vitabu? Ni vitabu gani hasa huwa unapendelea kusoma? (nje na vile vya love affairs)
Ni Ushauri gani Unaweza mpatia kijana wa enzi (wa kimaisha) kwa Uzoefu wako kwa lengo la kumsaidia aweze kuishi maisha bora Kiuchumi na yenye kumpendeza Muumba. (japo najua swali hili liko wide sana)

Mwisho nakutakia Afya njema wewe na Family yako nzima mkuu. Endelea kutupa baraka zako Legendary.
Ahsante kwa pongezi.

Kuhusu 'screening', baadaye nilikuja kujuwa kumbe ni mafundisho ya Mtume Muhammad (Rehema na Amani za Mungu zimwendee) kwamba, pindi tunapojiwa na mtu kwa ajili ya kuposa, ni vyema kumchunguza kujuwa tabia zake, tusikubali posa "kichwakichwa" hadi kujiridhisha.

Kwa kufanya hivyo hupelekea kujenga ndoa zilizo imara, hebu fikiria, mtu akioa anakuwa amekamilisha nusu ya dini. Nadhani umeona uzito wake.

Tendo moja jema la aliyeoa ni bora zaidi ya mara 70 ya matendo kama hilo kwa asiyeoa.

Nawaasa vijana waoe, waachane na fikra za kuishi bila kuoa isipokuwa tu kama hawezi kutimiza haya mambo:-

Kumpa chakula mke, kumpa makazi/malazi mke, kumpa mavazi mke , kumpa tendo la ndoa mke.

Kuhusu ubaguzi, Waarabu, wahidi, wachina, wakorea na jamii nyingine hata ndani ya nchi moja walikuwa hawataki jamii nyingine kuchanganya damu, ajabu sana.

Uislamu unashauri watu wachanganye nasaba ili kuimarisha afya za familia, lakini wengi walikuwa wagumu.

Siku hizi angalau wamelegeza kamba. Ila bado ubaguzi upo. Bado Waarabu wanawachukulia Waafrika ni watumwa. Ukiishi nao kwa ukaribu utaliona hili.

Wamesahau wosia waliopewa na babu yao Nabii Nuhu wakati akimuasa mjukuu wake aitwaye 'Misri' mtoto wa mwanaye aitwaye Ham, kwamba mama yake Misri katika uzao unaofuata atajifungua mapacha, mmoja atakuwa mweupe na mwingine atakuwa mweusi.

Mweupe ndipo kikapatikana kizazi cha Kiarabu na mweusi ndipo kikapatikana kizazi cha Kiafrika.

Na kwamba mtoto mweupe asije kumdharau mtoto mweusi na wasaidiane.

(Ipo katika simulizi za kale)

Ndoa yangu ilitikisa jiji na jamii ya kiarabu na kuleta uelewa mpana ingawaje tayari zilikuwepo ndo za namna hiyo tayari mfano mtoto wa mzee Shebe nk.

Ndugu wa Hamida wa Tz na nje walinikubali, ingawaje mwanzo walimeza kwa ugumu lakini hatimaye karibu wote 'walielewa somo', hali ya uchumi nayo ilinibeba wakati huo.

Ushirikiano upo hadi sasa na ndio maana siku za hivi karibuni nimekuwa bize kiasi cha kushindwa kupata muda wa kuandika simulizi ya 'msegemnege', lakini nitaendelea hivi karibuni.

Kuhusu dini, ukiangalia kwa jicho la juu juu unaweza kidhani ni mpango wa watu fulani ili waweze kutawala fikra za watu na dunia kwa ujumla.

Lakini ukweli ni kwamba Mungu yupo. Na ameleta muongozo wa kuishi hapa duniani.

Ukirudi katika historia miaka kadhaa nyuma utakuta kweli mtu aliyekuwa akiitwa Muhammad (peace be upon him) alikuwepo.

Ukirudi miaka mingine nyuma utakuta mtu aliyekuwa akiitwa Yesu alikuwepo...

Mafundisho yao ni yale yale tangia kizazi chao cha kwanza hapa Duniani, kumuabudu Mungu mmoja na kutenda mema.

Ni muhimu sana kuishi katika hali ya ucha Mungu na baraka zake utazishuhudia waziwazi.

Vitabu nilisoma sana enzi hizo mfano Dogs of War, Wooden Horse, Invisible man, Man with 100 faces, A passage to India, 100 years of solitude nk na zile simulizi za kale kabisa.

Katika haya maisha, ukipata nafasi ya kufika Ethipia na Israel na ukapekua maktaba zao utajifunza mengi. Pia kuna elimu nyingi zipo katika lugha za Kiarabu laiti watu wangejua.

Ushauri kwa vijana, ni kufanya kazi kwa bidii, kumcha Mungu mengine huja kama baraka.

Mwisho, afya njema iwe kwetu sote mimi na wewe na kila asomaye post hii pamoja na familia zetu.

Amin.
 
Ukirudi katika historia miaka kadhaa nyuma utakuta kweli mtu aliyekuwa akiitwa Muhammad (peace be upon him) alikiwepo.

Ukirudi miaka mingine nyuma utakuta mtu aliyekuwa akiitwa Yesu alikuwepo...

Mafundisho yao ni yale yale tangia kizazi chao cha kwanza hapa Duniani, kumuabudu Mungu mmoja na kutenda mema.

Ni muhimu sana kuishi katika hali ya ucha Mungu na baraka zake utazishuhudia waziwazi.

Vitabu nilisoma sana enzi hizo mfano Dogs of War, Wooden Horse, Invisible man, Man with 100 faces, A passage to India, 100 years of solitude nk na zile simulizi za kale kabisa.

Katika haya maisha, ukipata nafasi ya kufika Ethipia na Israel na ukapekua maktaba zao utajifunza mengi. Pia kuna elimu nyingi zipo katika lugha za Kiarabu laiti watu wangejua.

Ushauri kwa vijana, ni kufanya kazi kwa bidii, kumcha Mungu mengine huja kama baraka.

Mwisho, afya njema iwe kwetu sote mimi na wewe na kila asomaye post hii pamoja na familia zetu.

Amin.
Shukran Sana sana Mkuu JBourne59 hakika umekata KIU ya swali barabara Ndugu yangu. Itoshe tu kusema uwepo wako hapa jukwaani ama hakika ni hazina tosha tunafaidika na mengi sana, busara za kale, mafundisho na miongozo mbali mbali kwa mafundisho ya dini, uzoefu wako kwenye mambo mbali mbali ya kimaisha n.k Mungu akujaalie zaidi Mkuu 🙏
 
Nimefanikiwa kusoma na kuimaliza simulizi yote, kwa dhati niseme Asante sana mzee wetu jbourne59 kwa kushare sehemu ya historia ya maisha yako. Kwa umri wako wew ni sawa na baba yangu na mimi naweza lingana na mwanao wa pili kama sikosei.

Yafuatayo ni mambo niliyojifunza kupitia simulizi hii.

1. Maisha ni hadithi jinsi unavyoishi ndivyo unavyo tengeneza hadithi yako, hata kama hutapata fulsa ya kusimulia mapito yako wale waliyoishi karibu nawe watasimulia hadithi yako. Hivyo basi tunavyoishi ndivyo tunavyopata cha kusimulia. Kama uwepo wako hapa duniani ulikuwa baraka kwa wengine basi mema yako yataishi vinywani mwa watu. Na pia kama itakuwa ni kinyume vivyo hivyo maovu yako yataishi vinywani mwa watu. Funzo ni tujitahidi kuishi maisha ya kuacha alama njema kwa vizazi vijavyo

2. Hekima ni msingi wa ufumbuzi wa changamoto yeyote. Hekima aliyoitumia mzee katika changamoto yake iliweza kumpatia mtokeo chanya yaliyodumu kwa muda mrefu (sustainable solution). Pengine zilikuwepo njia nyingine ambazo zingeweza solve swala la mzee ila hekma iliweza muongoza katika njia iliyo bora ambayo matunda yake yalidumu kwa kitambo. Vijana tuitafute hekima kwa gharama yeyote ile tuweze kabiliana ama kuepeka changamoto nyingi zinazotukabili.

3. Tusijitenge na jamii inayotuzunguka. Chongamoto nyingi zinatuwia ugumu kutatua sababu tuu tunaji isolate sana watu wanaotuzunguka. Tunaweza ona mzee kupitia wazee aliokuwa akijumuika nao kwenye mchezo wa bao aliweza pata msaada mkubwa hatimaye akasolve chengamoto yake. Vijana tushushe mabega hawa tunaowapita mtaani na vigari vyetu vioo juu wanaweza kuwa msaada mkubwa kwetu bila ya sisi kufahamu.

4. Muheshimu aliyekuzidi mlinde na muongoze aliye chini yako. Kuna manufaa mengi ktk kusikiliza na kuheshimu wazazi (wazee) lakini pia tunapoinuliwa ni swala la muhimu kukumbuka kuwainua walio chini yetu maana huu ni kama uwekezaji ambao matunda yake hunufaisha jamii na familia kwa ujumla. Mzee hukuwapinga wazazi walipotaka uoe binti mwingine lakini pia hukumshawishi mama yetu kwenda kinyume na wazee wake, halikadhalika tunaona ulivyowapambania wadogo zako.

Kiukweli yakujifunza ni mengi mengine wengi wameshayasema huko juu, lakini kubwa niseme tuu story kama hizi ndizo zinazonifanya kuiona JF kuwa sehemu bora ya kuperezi kuliko mitandao mingine. Mwenyezi Mungu akujaaliye afya njema wew na familia yako mzee wetu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom