Uhusiano unapovunjika nani hasa mwenye hasara?

Ngekewa

JF-Expert Member
Jul 8, 2008
7,705
1,288
Salaam wanajamvi. Kama kawaida yangu nikitingwa na jambo nakimbilia Great Thinkers!
Nimekuwa nikisoma malalamiko mengi humu jamvini kuhusu kuvunjika kwa mahusiano baina ya wapenzi au wanandowa. Nami nimekuwa nikijiuliza hivyo mwanamme analalamika nini iwapo mwanamke kwa hiari yake anaamuwa kuvunja uhusiano? Pengine mtizamo wangu sio sahihi hivyo naomba mawanzo ya jamvi kuhusu hili.Uhusiano unapovunjika nani hasa mwenye hasara zaidi?
 
Wanawake wengi ni wazuri na hakuna shida sana ya kupata aina ya mwanamke wa kureplace aliyeamuwa kuondoka!!
 
well mara nyingi yule ambaye amebwagwa ndio anakuwa ana hasara. nasema hivyo kwa sababu kwanza kabisa lazima atakuwa amewekeza katika huo uhusiano emotionaly na pia ata financially. pia atakuwa amejenga matarajio fulani ambayo sasa ghafla hayatatimia. yule anaye bwaga pia alikuwa ameweka hivyo ila yeye amefikia point ambapo anaona freedom yake ina thamani zaidi kuliko vitu ambavyo amewekeza katika muda wote huo aliokuwa katika huo uhusiano.
 
Pengine uko sahihi kabisa lakini kwa fikira zangu ni kuwa mwanamme ana upeo mkubwa wa kujiliwaza kwa kupata mbadala pale anapobwagwa kuliko mwanamke, jee na hili vipi?
 
upeo mkubwa wakujiliwaza kwa kupata mdadala na yupi anapata hasara sana ni vitu viwili tofauti. achana na kubwagwa bana especially kama mwana ndio ulikuwa unatia nanga kabisa. yale maoutings malove uliyokuwa unatoa yote kwishney bana inauma. pamoja na uwezo wa mwanaume kujiliwaza kwa kupata mbadala mara nyingi hii substitute inakuwa ya kujipoza lakini bado uchungu wakubwagwa upo pale pale.
 
Muathirika ni yule aliyependwa na kwa ujinga wake hakuthamini penzi lile; kwani kila atakapoenda atajuta na kukumbuka penzi la kweli alilolichezea.

Yule mwenye mapenzi ya kweli ataumia mwanzoni na baadaye ataheal, na akipata mwingine anayeweza appreciate pendo lake he/she will move on!
 
Athari za Pale Pale ni Yule aliyeachwa.... Ila inategemea Na Umri Umeendaje?

Ikiwa Mwanamke ameachwa anaumri umekaribia na MENOPAUSE hasara ni kwa Mwanamke... Lakini kama ndo Bado analipa hakuna Tatizo atapata Mwingine.

Mwanaume atapeta Tu hata akiachwa na Umri mkubwa. Bt awe na Pesa au famous. Ingawa ataumia
 
Inategemeana nani kapenda sana na namna gani mtu kafungwa nae namanisha hv mfano Mwanamke kazalishwa na hana kazi hapo mwanamke imekula kwake,Mwanaume kamsomesha mwanamke halafu mwanamke kambwaga hapo itakula kwa mwanaume na mengineyo kwa kweli issue ni kwamba inategemea na position ya muhusika katika penzi hilo hiyo ndo itadetermine nani ataumia kuliko mwenzake.
 
Anayepata hasara ni yule aliyeachwa..kwa sababu bado alikua ana mategemeo fulani kwenye uhusiano huo!
 
Wote wanaasara,sababu kama walikua wakiishi pamoja mazowea,mambo waliokua wakifanya pamoja kama kuna watoto
ndio itawaumiza zaidi,pesa mali yote matokeo unaweza ukaachana na mume nyote mnapesa lakini zisiwasaidie kituchochote
kwenye maamuzi.....
 
well mara nyingi yule ambaye amebwagwa ndio anakuwa ana hasara. nasema hivyo kwa sababu kwanza kabisa lazima atakuwa amewekeza katika huo uhusiano emotionaly na pia ata financially. pia atakuwa amejenga matarajio fulani ambayo sasa ghafla hayatatimia. yule anaye bwaga pia alikuwa ameweka hivyo ila yeye amefikia point ambapo anaona freedom yake ina thamani zaidi kuliko vitu ambavyo amewekeza katika muda wote huo aliokuwa katika huo uhusiano.

well said...i completely agree with you
 
Wanaume wengi wana pesa hivyo sio kazi kumpata mwenye nazo zaidi ya aliyenibwaga!

Tatizo ni kuwa uzuri ni maumbile na Mola katika hilo amekuwa mkarimu zaidi kwa wengi lakini fedha walionazo ni wachache na kwa bahati mbaya si kama uzuri ambao kila mtu ana sifa yake kuona uzuri,Pesa uzuri wake ni uleule na wahitaji ni woooooote!!!!
 
Wote wanaasara,sababu kama walikua wakiishi pamoja mazowea,mambo waliokua wakifanya pamoja kama kuna watoto
ndio itawaumiza zaidi,pesa mali yote matokeo unaweza ukaachana na mume nyote mnapesa lakini zisiwasaidie kituchochote
kwenye maamuzi.....

Sasa kwanini huwa tunatafuta mabwana au mabibi wa nje?
 
Muathirika ni yule aliyependwa na kwa ujinga wake hakuthamini penzi lile; kwani kila atakapoenda atajuta na kukumbuka penzi la kweli alilolichezea.

Yule mwenye mapenzi ya kweli ataumia mwanzoni na baadaye ataheal, na akipata mwingine anayeweza appreciate pendo lake he/she will move on!

....umeiweka vyema, hasa mpendaji nae awe anajitambua alipowekeza sipo....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom