Uhusiano huu siuelewi naomba msaada tafadhali

mwafrica2010

New Member
Sep 16, 2011
2
1
Natumaini wote mu wazima,

Tafadhali naomba mnisaidie kweli nahitaji ushauri.

Mimi ni msichana, Nina mpenzi wangu tumeanza nae uhusiano wa kimapenzi mwanzo wa mwaka huu na kabla ya hapo tulikuwa ni marafiki wa kawaida tu kwa muda mrefu sana japo alishawahi kunitaka kimapenzi miaka 3-4 iliyopita lakini haikuwezekana coz nilikuwa na mpenzi mwingine ambapo nilikuwa wazi kumuelezea naye akawa amelielewa hilo,aliendelea na maisha yake tena na akaanzisha uhusiano na dada mmoja tulikuwa tunajuana nae.

Tukabakia kuwa marafiki wa kawaida kabisa japo aliendelea kuniita majina ya kuonyesha tuna uhusiano hata mbele ya GF wake na kunitumia msg za salamu i.e habari mpenzi or swthrt/darling kila asubuhi, na mchana kunitakia mchana mwema na usiku kunitakia usiku mwema na nyingine nyingi kiasi kwamba kikaleta ugomvi mkubwa kati yangu na BF wangu …..

Mimi nikawa nimeachana na BF wangu but among the things zilichangia kuachana nae ni yeye, alinisanibabishia ugomvi mkubwa ambao haukuwa na ukweli wowote (it's a long story) so niliamua kukata mawasiliano nae kwa kipindi cha zaidi ya mwaka huku akiendelea kunitumia msg za kuniomba msamaha.

Kwa Bahati mbaya tuliachana na BF wangu na yeye akawa ameachana na GF so we decided kuwa pamoja kama wapenzi…….ever since nimekuwa nae ugomvi wetu mkubwa ni kuchat na wasichana ambao anawatetea na kudai ni marafiki zake wa kawaida tu na wengine ni ma ex-girlfriend wake na msg wanazotumiana ni kama zile alizokuwa ananitumia mimi anyway nikasema let me just ignore it coz hata mm alifanya the same but hatukuwa wapenzi……

Kuna kipindi akawa ameniomba tutafute nae mtoto, nilipomwambia mambo ya kufunga ndoa kwanza akawa hataki anasema mtoto ni 1[SUP]st[/SUP] priority, kwa kweli sikuwa tayari kwa hilo wazo lake na alipokuwa amening'ang'ania sana nikamwambia atafute mwanamke mwingine anayeweza kuzaa nae kabla ya ndoa, akawa ananiambia kama utani okay mchakato unaendelea wa kutafuta huyo mwanamke…

Siku moja nikaenda kwake usiku kama saa 2 by surprise na nikamkuta na dada mmoja ambaye alishawahi kuwa GF wake, huyo dada najuana nae na kipindi walikuwa wapenzi nilikuwa najua pia kama wako nae by that time nikiwa rafiki wa kawaida…..that day nimewakuta (it's another long story)

In short mwanaume hakuwa in a position kuelezea exactly walikuwa wanafanya nini, yule dada akadai ya kuwa amemwambia hana GF, so wote wawili (mimi+dada) tukawa tunademand maelezo kutoka kwake bila mafanikio but nilipomuuliza yule dada walikuwa wanafanya nini akadai walikuwa wamekaa kukubaliana kuanzisha tena mahusiano yao na walikuwa wamefikia conclusion kuwa wako pamoja……

Kitendo hicho kiliniumiza sana then tukawa tumeondoka na kumuacha pekeyake coz alikuwa hataki kuongea kitu. Next day alinitafuta na kutaka kuonana na mimi ili anipe maelezo akidai kuwa jana I was in a very bad shape nisingeweza muelewa, tulipokutana naye akaniambia kuwa alimuita huyo dada ili waongee kuhusu kutafuta mtoto since mimi nilikataa kuzaa nae kabla ya ndoa so ule mchakato alikuwa ananiambia ndio huo alikuwa anaendelea nao na angekuja kuniambia but imetokea tuu bahati mbaya nilienda kwake kwa surprise……

Hicho kitu kilinisumbua sana kikanifanya nianze kuwaza kuwa hao marafiki zake anao chat nao inaweza kuwa pia anatembea nao coz mimi kipindikile nilikuwa na msimamo na sikumpa chance ya kuwa nae kimapenzi je ni wanawake wote wapo kama mimi?

Ameomba kuendelela kuwa na mimi na kukanusha kuwa hawana uhusiano na huyo dada, nilipomwambia ampigie simu mbele yangu ili aconfirm akakataa akidai kuwa nimuamini tu, nimemwambia kama ameamua kuwa na mimi sitaki kuona ana chat wala kukutana na huyo dada na pia asilete hao ma ex GF wake nyumbani kwake, jambo ambalo amelipinga sana na kudai naingilia uhuru wake wa nani aje kwake na nani asije……..

Ilipofikia kwamba hatukubaliani then nikamwambia hamna haja ya kuendelea kuwa pamoja, then akasuggest tutafute mshauri ambae tutamuelezea story yetu na atushauri ili ajue nani yuko right …..


Kwa mtazamo wangu namuona kuwa hana msimamo hajui anataka nini au hataki nini, kila siku tunagombana kwa sababu ya marafiki anao waprotect wanampigia simu anytime even at mid nite nikiwa nae……mimi kitendo hicho kinanikera sana maana naona atanipotezea muda wangu for nothing……

Jamani naombeni ushauri wenu na kama kuna watu wanatoa ushauri kwenye mambo haya ya mahusiano…..

Natanguliza shukrani zangu na naomba radhi kwa maelezo marefu.
 

The Finest

JF-Expert Member
Jul 14, 2010
21,607
5,968
Aisee!! Hapo hakuna mapenzi cha msingi angalia ustaarabu wako maana kutokana na maelezo yako mimi naona kama jamaa anakutumia maana wala hauhitaji tochi kumulika mwizi wako, huyo mwizi anaonekana hadharani mchana kweupe.

Pole Sana ila piga moyo konde
 

The Magnificent

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
2,694
1,244
Nahisi huna mvuto kwa wanaume ndo maana umekuwa tayari kujidhalilisha kwa huyo jamaa!
Wewe ni mjinga na mpuuzi kabisa,sema NDIYO nikufungukie upuuzi wako na ujinga ulipo,otherwise usiwasumbue maGT kwa thread zenye ishu za kitoto hv!
Good lucky!
 

Preta

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
24,316
18,709
Nahisi huna mvuto kwa wanaume ndo maana umekuwa tayari kujidhalilisha kwa huyo jamaa!
Wewe ni mjinga na mpuuzi kabisa,sema NDIYO nikufungukie upuuzi wako na ujinga ulipo,otherwise usiwasumbue maGT kwa thread zenye ishu za kitoto hv!
Good lucky!

ayi ayi....mon frere....it hurts when you tell a lady things like this.......
 

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
49,307
69,595
Mpwa wangu Mpenzi, sweet/my darling and daring!!! kwanini unapoteza muda wako kiasi hicho kwake? kwanini? kweli kabisa huna akili hata moja ya kuona huo ni mchezo wa kuigiza usio hata na mvuto? No please, utakua unawadhalilisha hata akina dada wengine kwa kukubali kurubuniwa na mtu kama huyu kwa njia nyepesi namna hii...huyo jamaa ni MALAYA na mhuni mkubwa (kama story yako uliyoeleza ina ukweli) lakini kama ni uongoo basi ulaaniwe wewe mwenyewe. Kwanini umekuwa so soft kiasi hicho? tangu lini watu wakatafuta mtoto kabla ya ndoa? (nazungumzia tamaduni za Tz) hapana huo anatafuta mwamvuli wa kufanyia uzinzi wake tu hana lolote. Sina la ziada amua kunyoa au kusuka ila warning ni hii kama saa hizi ambapo unatoka kwenu/kwako kwenda kwake ( ambapo ndio inasadikiwa kuwa kipindi kitamu zaidi cha mahusiano) jiulize je itakuaje siku mko kwenye hicho kinachoitwa ndoa? ambapo atakua anakuona kila saa? utachuja kabla hata hajakuoa, Barikiwa
 

Mtalingolo

JF-Expert Member
Aug 4, 2011
2,182
408
Mmh hapo kweli hakuna mapenzi ya dhati ni kukutumia tu, jaribu kuangalia na upande wapili wa kanda(KIMBIA FASTA)..
 

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
49,307
69,595
Basi Mpwa, twende nae taratibu bhana, nahisi kama ni mwanao ungekuwa umesha"mtafuna" mwenyewe kwa hasira......but you are very right indeed
Nahisi huna mvuto kwa wanaume ndo maana umekuwa tayari kujidhalilisha kwa huyo jamaa!
Wewe ni mjinga na mpuuzi kabisa,sema NDIYO nikufungukie upuuzi wako na ujinga ulipo,otherwise usiwasumbue maGT kwa thread zenye ishu za kitoto hv!
Good lucky!
 

Blaki Womani

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
11,234
13,393
Tapeli wa mapenzi..........mshamba huyo anatanguliza kigezo cha kuzaa ndio kipimo cha mapenzi.........inawezekana ameona mapungufu fulani kwako so analeta za kuleta
 

The Magnificent

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
2,694
1,244
<font color="#800080"><font size="4"><span style="font-family: comic sans ms">ayi ayi....mon frere....it hurts when you tell a lady things like this.......</span></font></font>
<br />
<br />
but she deserves 2b told hv,kakosa akili kidogo tu ya kujua yupo kwenye uhusiano na MUHUNI,kwani wanaume tumeisha,huyu dada sio mzima..nimeamin kweli mapenz upofu,khaaah!
 

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
49,307
69,595
kumbe maskini Mpwa wangu ndio ka-join jamvi leo leo ili tumsaidie mawazo, haya mawazo ndio hayo.....
 

Mtalingolo

JF-Expert Member
Aug 4, 2011
2,182
408
Lakini mtu kakuvunjia mahusiano yako wewe na mpenzi wako, eti baadae unakuwa nae kweli ndio tunavofundishwa??,

Anachati na wewe kimapenzi wakati anajua unampenzi na yeye anampenz bado unamwona anafaa?? Inakuingia akilini??

Umemkuta na mwanamke usiku wa saambili afu anakwambia hakuna kinachoendelea kweli?? Nawewe unaamini tu??

Mimi naona dalili zote za wazi kuwa hakupendi kakuonesha, labda usubiri akuletee ugonjwa wa hatari(HIV), funguka dadaangu na usepe mapema.
 

Vin Diesel

JF-Expert Member
Mar 1, 2011
9,083
6,334
Hujagundua tu kuwa huna chako hapo? inauma ila ndo ukweli huo...so far una wasaidiza kibao na ninadhani wewe ndio ni msaidizi na sio mdau mkuu...
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom