Uhuru wa wachunguzi huru

Uhuru wa wachunguzi huru

Link gan unayotaka wizara ya Kazi na Ajira ipo, peleka malalamiko yako huko
Punguza povu Mkuu...... humu ndani tupo kwa ajili ya kusaidiana....Link kwa maana ya ''kushikwa mkono'' si unajua kazi za siku hizi zilivyo ikizingatia mimi sijasoma sana.......nimeishia sekondari tu na mambo ni magumu mpaka natamani Mwarobaini kuufanya Muwa.........!!! Please nisaidie kama unaweza hili.........
 
Tokea Mh. Lissu anusurike kwenye shambulio dhidi ya uhai wake siku ashara na kitu zilizopita, kumekuwepo na sauti kadhaa zinazodai au zinazotaka tukio hilo lichunguzwe na wachunguzi 'huru' kutoka nje ya nchi.

Sababu yake kubwa ni kwamba vyombo vya ndani [ya nchi] vya usalama haviko huru kuweza kufanya uchunguzi huo kwa sababu vyenyewe ndivyo vinavyoshukiwa kupanga na kutekeleza jaribio hilo ili kutimiza matakwa ya mtu au watu wa huko serikalini na kwenye CCM.

Hisia hizo [za kuishuku na kuituhumu] nazielewa. Hivyo watu wanaotaka kuona wachunguzi huru wakichunguza nao nawaelewa.

Ila, kuna vitu vinanitatiza kidogo kuhusu huo u huru wa hao wachunguzi na utayari wa kambi ya Lissu na kambi ya serikali kuyakubali matokeo ya huo uchunguzi wao endapo utatokea.

La kwanza, ni nani atayeingia gharama za hao wachunguzi?

Tuseme CHADEMA na wafadhili wao ndiyo wataingia hizo gharama.

Kama hivyo ndo itavyokuwa, je, hao wachunguzi watakuwa huru kiasi gani ilhali wanalipwa na upande wa mnusurika wa jaribio?

CHADEMA kweli inaweza kuwalipa hao wachunguzi huru halafu hao wachunguzi watoe uchunguzi ambao ni kinyume na madai ya CHADEMA [kwamba serikali kupitia vyombo vyake vya usalama ndiye mhusika]? Kama wataletwa na CHADEMA maana yake ni kwamba wao ni waajiriwa wa hicho chama. Akili yangu haioni ni jinsi gani hao wachunguzi huru wanaweza kutoa matokeo yaliyo kinyume na hisia za watu waliowaajiri.

Je, serikali nayo ipo tayari kweli kuyakubali matokeo ya hao wachunguzi huru ambao huenda wakalipwa na hicho chama pinzani?

Na vipi kwa mfano serikali ikubali ujio wa hao wachunguzi na iingie gharama kwa kazi watayoifanya, je, CHADEMA ipo tayari kuyapokea na kuyakubali matokeo ya huo uchunguzi hata kama yakiwa tofauti na vile wao wadhaniavyo?

Kumbuka, kama serikali ndiyo itayoingia gharama za hao watu maana yake ni kwamba watakuwa wanaitumikia serikali iliyopo madarakani ambayo ni ya CCM.

Kwa mtaji huo hao wachunguzi huru watakuwa wapo huru kiasi gani?

Hili suala ni gumu kwa kweli. Kila ninapowaza na kuwazua sipati majibu.

Sijui nyie wadau mnalionaje hilo suala.

Jumapili njema.
Hivi katika hili tukio kunahitajika uchunguzi kweli? na uchunguzi huo wa nini wakati waliofanya hilo tukio wanajulikana wazi na waliotoa maelekezo wapo
 
Kama hivyo ndo itavyokuwa, je, hao wachunguzi watakuwa huru kiasi gani ilhali wanalipwa na upande wa mnusurika wa jaribio?

Nahisi kuna kitu hujakizungumzia au kukifikiria, either kwa makusudi au kwa kutojua.

Unaposema wachunguzi huru una maana gani wakati huo huo kusema wanaweza kuhongwa?

Hao unaowataja siyo wachunguzi huru, ni makanjanja.
 
Hivi katika hili tukio kunahitajika uchunguzi kweli? na uchunguzi huo wa nini wakati waliofanya hilo tukio wanajulikana wazi na waliotoa maelekezo wapo

Ushahidi uko wapi?
 
Nahisi kuna kitu hujakizungumzia au kukifikiria, either kwa makusudi au kwa kutojua.

Unaposema wachunguzi huru una maana gani wakati huo huo kusema wanaweza kuhongwa?

Hao unaowataja siyo wachunguzi huru, ni makanjanja.

Nahisi hujaelewa ulichokisoma.
 
Gharama ni ya nchi husika yaani walikotoka. Lakini hawawezi kuja mpaka serikali iwaruhusu. Kwa kuwa serikali ndiyo inahisiwa kuhusika haiwezi kukubali kutoa kibali lakini Ingekuwa hai husiki ingetoa kibali chapuchapu. Kwahiyo tusubiri jibu litapatikana mapema sana kama wahusika ni serikali au la
 
Je wachunguzi wakileta majibu aliyeuziwa chama na chairman wao wanahusika watakubaliana na matokeo?
 
Vyombo vya usalama vitamkamata nani ikiwa mashahidi wa muhimu wote wapo Nairobi?
Kwan serikali imeshindwa kwenda kuwahoji kule na kuendelea na uchunguzi au mpk wakae rumande ndo itakua rahisi
 
The UK has a budget of $1.04 trillion. The US has a budget of over $3.8 trillion. They can easily afford the cost of sending Scotland Yard or FBI for few weeks to conduct an independent investigation. Also, to receive money for services rendered to a poor third world country would be shameful for U.K. or U.S.
Word I agree with u 100%
 
Back
Top Bottom