Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 98,204
- 144,100
Jambo la muhimu waruhusiwe kwanza wafanye huo uchunguzi.
Kitendo cha serikali kukataa huo uchunguzi huru unaleta picha gani ilihali vyombo vyetu vya usalama hadi sasa havijafanikiwa kukamata hao wasiojulikana japo namba za Nissan Patrol zimetajwa.
Uchunguzi huru uruhusiwe, matokeo yana sehemu mbili(positive & negative) na hayaepukiki
Vyombo vya usalama vitamkamata nani ikiwa mashahidi wa muhimu wote wapo Nairobi?
Kila mtu mwenye akili anajua kilichotokea kwa hiyo hata ukijaribu kuisafisha vipi ccm ni kazi bure, ccm wananuka damu za watuTokea Mh. Lissu anusurike kwenye shambulio dhidi ya uhai wake siku ashara na kitu zilizopita, kumekuwepo na sauti kadhaa zinazodai au zinazotaka tukio hilo lichunguzwe na wachunguzi 'huru' kutoka nje ya nchi.
Sababu yake kubwa ni kwamba vyombo vya ndani [ya nchi] vya usalama haviko huru kuweza kufanya uchunguzi huo kwa sababu vyenyewe ndivyo vinavyoshukiwa kupanga na kutekeleza jaribio hilo ili kutimiza matakwa ya mtu au watu wa huko serikalini na kwenye CCM.
Hisia hizo [za kuishuku na kuituhumu] nazielewa. Hivyo watu wanaotaka kuona wachunguzi huru wakichunguza nao nawaelewa.
Ila, kuna vitu vinanitatiza kidogo kuhusu huo u huru wa hao wachunguzi na utayari wa kambi ya Lissu na kambi ya serikali kuyakubali matokeo ya huo uchunguzi wao endapo utatokea.
La kwanza, ni nani atayeingia gharama za hao wachunguzi?
Tuseme CHADEMA na wafadhili wao ndiyo wataingia hizo gharama.
Kama hivyo ndo itavyokuwa, je, hao wachunguzi watakuwa huru kiasi gani ilhali wanalipwa na upande wa mnusurika wa jaribio?
CHADEMA kweli inaweza kuwalipa hao wachunguzi huru halafu hao wachunguzi watoe uchunguzi ambao ni kinyume na madai ya CHADEMA [kwamba serikali kupitia vyombo vyake vya usalama ndiye mhusika]? Kama wataletwa na CHADEMA maana yake ni kwamba wao ni waajiriwa wa hicho chama. Akili yangu haioni ni jinsi gani hao wachunguzi huru wanaweza kutoa matokeo yaliyo kinyume na hisia za watu waliowaajiri.
Je, serikali nayo ipo tayari kweli kuyakubali matokeo ya hao wachunguzi huru ambao huenda wakalipwa na hicho chama pinzani?
Na vipi kwa mfano serikali ikubali ujio wa hao wachunguzi na iingie gharama kwa kazi watayoifanya, je, CHADEMA ipo tayari kuyapokea na kuyakubali matokeo ya huo uchunguzi hata kama yakiwa tofauti na vile wao wadhaniavyo?
Kumbuka, kama serikali ndiyo itayoingia gharama za hao watu maana yake ni kwamba watakuwa wanaitumikia serikali iliyopo madarakani ambayo ni ya CCM.
Kwa mtaji huo hao wachunguzi huru watakuwa wapo huru kiasi gani?
Hili suala ni gumu kwa kweli. Kila ninapowaza na kuwazua sipati majibu.
Sijui nyie wadau mnalionaje hilo suala.
Jumapili njema.
Kwa sababu hawana uweledi wa kazi yao ndio maana hiyo imekuwa sababu ya kujitetea.Vyombo vya usalama vitamkamata nani ikiwa mashahidi wa muhimu wote wapo Nairobi?
Kila mtu mwenye akili anajua kilichotokea kwa hiyo hata ukijaribu kuisafisha vipi ccm ni kazi bure, ccm wananuka damu za watu
We ndo hujatumia akili! anachomaanisha huo upelekezi ungekuwa huru kiasi gan kwa maana ungeweza kuegemea kwa upande uliowaleta na kuwalipa, ungeanza hapo kujadiliKuna mda hutumiagi akili. hilo Ni changamoto? Ata mashahidi wangekuwa wamekufa upepelezi ungefanyika na wahusika wangepatikana think out of box.
Mkuu uwezo wa wanaccm kufikiri vizuri ni mdogo sana ndiyo maana wakikosa nguvu ya hoja wanakimbilia kwenye matusi na mauajiKuna mda hutumiagi akili. hilo Ni changamoto? Ata mashahidi wangekuwa wamekufa upepelezi ungefanyika na wahusika wangepatikana think out of box.
We ndo hujatumia akili! anachomaanisha huo upelekezi ungekuwa huru kiasi gan kwa maana ungeweza kuegemea kwa upande uliowaleta na kuwalipa, ungeanza hapo kujadili
My imagination is loud and clear like jean claud van dammeYou're entitled to your imagination.
My imagination is loud and clear like jean claud van damme
Vyombo vya usalama vitamkamata nani ikiwa mashahidi wa muhimu wote wapo Nairobi?
Kiingereza cha kutuibia hela serikalini hicho, usomi wenu haulisaidii taifaPure hilarity!
We ndo hujatumia akili! anachomaanisha huo upelekezi ungekuwa huru kiasi gan kwa maana ungeweza kuegemea kwa upande uliowaleta na kuwalipa, ungeanza hapo kujadili
Hapo ndiyo wangedanganya na kupamba uchunguzi utafikiri Scotland yard kumbe hakuna lolote, sasa matumbo yanaunguluma maana wahusika walionekana na Lissu na dereva wakeJe wangekua wamekufa?