Uhuru Kenyatta amemtoa Rais Magufuli knock out! Ushauri wa bure kwa Rais Magufuli

Knock out kapigwa Uhuru
Hakuna mtanzania mwenye akili timamu anaweza kwenda kenya kuomba kazi,wao ndio wanakuja kwetu kupora kazi na wanataka sana ardhi yetu
Mtanzania mwenye akili timamu anayehitaji kazi ataenda kuitafuta popote pale. Ni punguani pekee atakayekaa nchini bila kipato kwa uzalendo uchwara akaacha fursa nchi jirani kama ipo.
 
kenya hakuna ardhi ambayo haina mwenyewe,mwanagalieni machoni uhuru anapoongea anajua mkiiga maneno yake kwao hakuna ardhi wao ndio watakuja huku.
 
Uamuzi wa Rais Magufuli wa hivi karibuni wa kupiga mnada ng'ombe wa Masai waliovuka kuja Tanzania, uchomaji wa vifaranga na mapokezi ya kiserikali ya Odinga alipoitembelea Tanzania hivi karibuni, wengi wamesema yaliingiza Tanzania na Kenya katika uhusiano mbaya kuliko ilivyowahi kutokea tangu ilipovunjika Jumuiya ya Afrika Mashariki miaka ya 1978.

Wengi walitegemea Kenya ingeanza kulipiza kisasi katika mambo kadhaa madogo madogo na makubwa. Lakini cha ajabu kabisa, wakati wa kuapa kwake, Uhuru Kenyatta ametamka kuwa Watanzania wanakaribishwa Kenya na wahudumiwe kama vile raia wa Kenya wanavyohudumiwa, na hata wakiomba kazi wapewe bila masharti. Uhuru hata akatania kwamba hata Watanzania na Wakenya wakitaka kuoana wasiwekewe masharti!

Taarifa nchini Kenya zinaonyesha kwa kufanya hivyo Kenyatta amemtoa kwa knock out Rais Magufuli katika round ya kwanza kabisa! In fact, wengi wanasema "it must be very embarrassing kwa Magufuli". Wale walio katika mtazamo wa kidini wanasema Kenyatta amemwacha Magufuli ajiwekee makaa ya moto kifuani!

Ushauri wangu wa bure kwa Rais Magufuli ni kwamba pengine sasa ni wakati wa yeye kutafakari kwa kina kwamba kuna mambo katika uongozi ambayo ni kweli yanahitaji utumiaji wa nguvu, u-bulldozer, kwa mfano ufisadi, ujambazi, nk. Lakini kuna mambo mengi sana yanahitaji utumiaji wa busara na diplomasia. Nitawakumbusha machache kati ya mambo ambayo Rais Magufuli alitumia nguvu pale ambapo haikutakiwa kutumia nguvu, tangu kabla hajawa raisi hadi sasa;
  1. Kugomea usafirishaji wa boti za kasi toka Dar kwenda ziwa Victoria - ambapo baadaye Kenya walikubali zipelekwe Ziwa Victoria kupitia barabara zao kutoka bandari ya Mombasa
  2. Kufukuza mkandarasi wa barabara bila kufuata utaratibu wa kisheria - ambapo matokeo yamekuwa bombardier yetu kushikiliwa Canada
  3. Kugomea mega-buses zilizokuwa zikisafirishwa kwenda Zambia kupita barabara ya Tanzam - ambapo baadaye JK aliamuru ziruhusiwe
  4. Kushinikiza jengo la TANESCO libomolewe (wakati wa JK) badala ya kutafuta njia mbadala - ambapo JK alimwamuru Pinda amkatalie kubomoa jengo hilo (baada ya kuwa Rais Magufuli karudi tena kuamuru libomolewe kwa kuwa yeye ndiye Rais sasa)
  5. Kuchoma vifaranga na kupiga mnada ngo'ombe wa Masai waliovuka kuja Tanzania kwa desturi ya Kimasai iliyodumu kwa mamia ya miaka - ambapo Kenya walitoa tamko hawatalipiza kisasi
  6. Kutumbua viongozi kwa mambo madogo madogo kama kutoa kauli asiyoipenda - ambapo wengi wao imebidi waendelee kupata mishahara bila kuwa kazini au kuonekana walitumbuliwa kimakosa
  7. Ubomoaji wa nyumba za watu kulingana na sheria ya eneo la barabara iliyobadilishwa - ambapo kisheria mtu aliyejenga kwa kibali cha serikali au kuishi eneo katazwa muda mrefu bila kuingiliwa na serikali ana haki ya kufidiwa anapobomolewa
  8. Kutoa amri kwa hisia (impulsive directives) - ambapo mara nyingine zimekuwa ni kinyume na katiba ya nchi na hata kuleta migogoro ya kisiasa nchini
  9. Kuzuia safari za nje za ku-ujumla hata zile ambazo zimefadhiliwa na ni sehemu ya uanachama wetu katika tasisisi za kimataifa pamoja na zile za Umoja wa Mataifa - ambapo ushiriki wa Tanzania katika mambo ya kimataifa sasa umekuwa nyuma na kusababisha tukose fursa nyingi za kimaendeleo
  10. Nk, nk, nk
Hawezi kukuelewa ndg yangu. Kwa kifupi ni sikio la kufa. Na hizi damu za watu zinazomwagika kila kukicha itafikia mahali hata kusaini hataweza atakuwa anaweka dole gumba. Ukilisoma tamko la Kenyatta kwa makini utaona namna ambavyo anwaambia wafanyabiashara na wananchi wenye mawazo positive "kama huko anawaona wa nini, huku tunajitafakari tutawapataje, njooni huku mle mema ya nchi". Ukweli aliyemfundisha Kenyatta hiyo mbinu ni bingwa haswa na akasema "am not putting a condition that other countries should do the same". Hii ni akili kubwa. Huku kwetu akili kubwa inatumika kupanga namna ya kuvuruga uchaguzi kwa kukatakata mawakala na kuwapiga. Shame!
 
Knock out kapigwa Uhuru
Hakuna mtanzania mwenye akili timamu anaweza kwenda kenya kuomba kazi,wao ndio wanakuja kwetu kupora kazi na wanataka sana ardhi yetu
Uoni hafifu! Utaenda kenya wakati hujiamini? Unafikiri Kenya unaweza kuwaamrisha tu kajipangeni barabarani msimamishe gari la rais au kushangilia mwenge? Kwa kifupi ni wenye kujiamini na aggressive tu ndo watakaoweza kuishi na kufanya kazi Kenya. Na watakaofanya hivyo (kama mimi nimeshaanza process za kutokomea huko) nwatajifunza kuwa agressive, sifa ambayo ni muhimu kwa mtu anayetaka kudumu kwenye uchumi mamboleo
 
Kwa nin Nyerere alifikia hatua ya kujitoa E.AC ??? Tanzania hatuna cha kupoteza kwa wa Kenya wao ndo wanahtaj Tanzania zaidi ya unavyofkria...istoshe nchi yao inaenda kugawanyika vipande vipande...Wakenya hawafai..

....If wishes were horses.....Hivi wazanzibari na ile maneno yao ....''huu muungano ni kama koti tuu'' mmeshamalizana nao? Au bado undava undavu tuu??
 
Uamuzi wa Rais Magufuli wa hivi karibuni wa kupiga mnada ng'ombe wa Masai waliovuka kuja Tanzania, uchomaji wa vifaranga na mapokezi ya kiserikali ya Odinga alipoitembelea Tanzania hivi karibuni, wengi wamesema yaliingiza Tanzania na Kenya katika uhusiano mbaya kuliko ilivyowahi kutokea tangu ilipovunjika Jumuiya ya Afrika Mashariki miaka ya 1978.

Wengi walitegemea Kenya ingeanza kulipiza kisasi katika mambo kadhaa madogo madogo na makubwa. Lakini cha ajabu kabisa, wakati wa kuapa kwake, Uhuru Kenyatta ametamka kuwa Watanzania wanakaribishwa Kenya na wahudumiwe kama vile raia wa Kenya wanavyohudumiwa, na hata wakiomba kazi wapewe bila masharti. Uhuru hata akatania kwamba hata Watanzania na Wakenya wakitaka kuoana wasiwekewe masharti!

Taarifa nchini Kenya zinaonyesha kwa kufanya hivyo Kenyatta amemtoa kwa knock out Rais Magufuli katika round ya kwanza kabisa! In fact, wengi wanasema "it must be very embarrassing kwa Magufuli". Wale walio katika mtazamo wa kidini wanasema Kenyatta amemwacha Magufuli ajiwekee makaa ya moto kifuani!

Ushauri wangu wa bure kwa Rais Magufuli ni kwamba pengine sasa ni wakati wa yeye kutafakari kwa kina kwamba kuna mambo katika uongozi ambayo ni kweli yanahitaji utumiaji wa nguvu, u-bulldozer, kwa mfano ufisadi, ujambazi, nk. Lakini kuna mambo mengi sana yanahitaji utumiaji wa busara na diplomasia. Nitawakumbusha machache kati ya mambo ambayo Rais Magufuli alitumia nguvu pale ambapo haikutakiwa kutumia nguvu, tangu kabla hajawa raisi hadi sasa;
  1. Kugomea usafirishaji wa boti za kasi toka Dar kwenda ziwa Victoria - ambapo baadaye Kenya walikubali zipelekwe Ziwa Victoria kupitia barabara zao kutoka bandari ya Mombasa
  2. Kufukuza mkandarasi wa barabara bila kufuata utaratibu wa kisheria - ambapo matokeo yamekuwa bombardier yetu kushikiliwa Canada
  3. Kugomea mega-buses zilizokuwa zikisafirishwa kwenda Zambia kupita barabara ya Tanzam - ambapo baadaye JK aliamuru ziruhusiwe
  4. Kushinikiza jengo la TANESCO libomolewe (wakati wa JK) badala ya kutafuta njia mbadala - ambapo JK alimwamuru Pinda amkatalie kubomoa jengo hilo (baada ya kuwa Rais Magufuli karudi tena kuamuru libomolewe kwa kuwa yeye ndiye Rais sasa)
  5. Kuchoma vifaranga na kupiga mnada ngo'ombe wa Masai waliovuka kuja Tanzania kwa desturi ya Kimasai iliyodumu kwa mamia ya miaka - ambapo Kenya walitoa tamko hawatalipiza kisasi
  6. Kutumbua viongozi kwa mambo madogo madogo kama kutoa kauli asiyoipenda - ambapo wengi wao imebidi waendelee kupata mishahara bila kuwa kazini au kuonekana walitumbuliwa kimakosa
  7. Ubomoaji wa nyumba za watu kulingana na sheria ya eneo la barabara iliyobadilishwa - ambapo kisheria mtu aliyejenga kwa kibali cha serikali au kuishi eneo katazwa muda mrefu bila kuingiliwa na serikali ana haki ya kufidiwa anapobomolewa
  8. Kutoa amri kwa hisia (impulsive directives) - ambapo mara nyingine zimekuwa ni kinyume na katiba ya nchi na hata kuleta migogoro ya kisiasa nchini
  9. Kuzuia safari za nje za ku-ujumla hata zile ambazo zimefadhiliwa na ni sehemu ya uanachama wetu katika tasisisi za kimataifa pamoja na zile za Umoja wa Mataifa - ambapo ushiriki wa Tanzania katika mambo ya kimataifa sasa umekuwa nyuma na kusababisha tukose fursa nyingi za kimaendeleo
  10. Nk, nk, nk
Hayo ni maoni yako binafsi, rohoni kwa mtu ni mbali, umefikaje kwenye hiyo mioyo?, endelea na Ramli chonganishi upate mkate wa siku, paka shume mkubwa wee!
 
Kwa nin Nyerere alifikia hatua ya kujitoa E.AC ??? Tanzania hatuna cha kupoteza kwa wa Kenya wao ndo wanahtaj Tanzania zaidi ya unavyofkria...istoshe nchi yao inaenda kugawanyika vipande vipande...Wakenya hawafai..
Wana akili sana ndio maana they have a lot to loose
Tz ni soko la viwanda vyao. Ww huna viwanda ni mzee wa kuagiza bidhaa ndio maana huna la kupoteza
 
Nafikiri umesahau pia kuongelea jambo Muhimu sana juu ya Usalama wa jirani zetu;

1. Ungekaa Kenya ndio ungejua kuwa hakuna Amani. Bila Amani mengine yote ni bureee;
Sijui kama nimewahi kuangalia Citizen ikapita bila kusikia kuna watu wameuwawa????

2. Kupeleka Jeshi kulinda nchi za watu wangati Wakenya wanakufa kwa kukosa Usalama

3. Kenya wanakatiba mpya inayo waruhusu watu kuandamana
Je umewahi kuliona hilo tangia harakati za Uchaguzi zianze?

4. North Kenya wanakufaa kwa njaa kila mwaka wakati ukienda Nairobi, nakuru na mombasa utafikiri upo Ulaya

5. VYETI FEKI = Najua hili hulijui....kazi kwako fuatilia kule utashangaa. Usiogopeshwe na kiingereza..kwani hakijengi nyumba au hakiwezi kutibu wagonjwa hospitali ile ni lugha tu???

Ile nchi imegawanjika sana kwa UKABILA, ukanda, kichumi nk nafikiri wana mengi ya kujifunza kwetu kuliko sisi kujifunza kwao. Ukisikia Kenya kuna maendeleo, ujue unaongelea kama 30% ya Nchi huko kwingine ni shida!!!
Think twice!!!!!
 
Ametukamata kuoa Kenya? Kupiga mifugo mnada? Kuchoma vifaranga?

I say na wewe una mapenzi ya ajabu. Sie tunaongelea mambo makubwa yanayohusu geopolitics, sasa hivyo vingine ni namna tu ya kum-profile Magufuli ili uelewe ni mtu wa aina gani. Magufuli anapopiga mnada ng'ombe wa Masai wa Kenya watu wenye akili wanaona beyond ng'ombe kupigwa mnada. Inaonekana wewe unachoona ni kwamba serikali imepata hela ya kuuza ng'ombe wa Kenya na ndio unatetetea.

Let me tell you something lover boy, sidhani kama kuna Mtanzania mwenye akili ambaye hatafurahia Magufuli kuondoa ufisadi, kulinda rasilimali zetu, kuondoa uozo wa uongozi. Lakini kuna mamia ya Watanzania ambao watajiuliza kama ni busara kwa Magufuli kubomoa nyumba za watu bila kufuata utaratibu wa kisheria, kukaidi amri za mahakama, kuvunja katiba kimakusudi, kuzuia ushiriki wa Tanzania katika taaasisi za kimataifa ambazo sisi ni wanachama, kutumbua watu kishabiki, kutumia fedha za serikali bila kufuata taratibu za kitaifa za ununuzi au uanzishaji miradi ya kitaifa, kukandamiza vyama vya upinzani, kunyanyasa viongozi wa upinzani kwa kutumia polisi, kutoa maagizo kwa Bunge kukandamiza wapinzani, nk.

Elewa tunakiri kwamba Magufuli anafanya mazuri mengi tu, lakini hayafanyi iwe halali yeye kufanya yale mengine mabaya mengi tu. Hivi wewe utakubali daktari akutendee kinyume cha maumbile na kuona ni sawa na halali kwake kufanya hivyo kwa kuwa alikufanyia operation na kuokoa uhai wako au wa mtu wako wa karibu? Tumia akili sio ushabiki kutafakari mambo.

Unaishi Tanzania ya wapi mkuu, huwezi ukalilia uwazi na uwajibikaji katika serikali ukiwa unakumbatia unapindisha sheria, 80% ya watanzania tumedekezwa sana, ndio maana unakuta mtu anajenga sehemu ambayo hairuhusiwi na bado anaachwa na anachekelea, nieleze ni mahali wapi duniani ambapo mtu atajenga sehemu ambayo hairuhusiwi asiondolewe, jibu ni Tanzania, ndio maana miji yetu iko kama kiholela , kubadili watu kutoka katika hali hiyo kwenda katika hali nyingine lazima maumivu na malalamiko yawepo, lasivyo tutakuwa hatuna uwezo kuplan miji, sewage system itabaki kuwa mbovu kama ilivyo Dar es salaam, hivi wew unafurahia mvua kidogo ikinyesha Dar inabadilika kuwa ziwa? huo hali ilivyo Dar kweli ?.

Kutumbua watu kishabiki, sio kweli, kama ni ushabiki basi waziri wa mambo ya ndani kitwanga asingefukuzwa ambae ni rafiki wa raisi, Lugumi nyumba zake zisingepigwa mnada,nimekutajia hawa ambao ni watu wa kanda alikotoka yeye, kama ni ushabiki au kuonea mtu basi hawa watu wasigechukuliwa hatua, tuondoeni dhana ya kuonea kila mara hata kama watu wanafanya makosa, hatuwezi tukawa na serikali inayowajibika kama bado tunakumbatia maovu, hali hii ndo imelifanya bara la afrika likasinyaa, tunakuwa na viongozi bora viongozi hata hawawezi kutoa maamuzi.

Kutumia fedha za serikali bila kufuata taratibu, sio kweli, bunge hupitisha makadirio na kiasi cha pesa kinachotumika kwa wakati Fulani, pia hupitisha mpango wa maendeleo wa wa muda wa miaka Fulani, nadhani Tanzania huwa wanapitisha mpango wa maendeleo wa miaka mitano mitano, ndani ya mipango hiyo kuna projects ambazo huwa serikali inakusudia kuzianzisha na kuzifanya, pia hutengewa budget ya kiasi cha pesa kitakachotumika katika miradi ile, kasha serikali huachiwa majukumu ya kuanza kutafuta pesa na kuzisimamia miradi ile. Swala la budget ikishapitishwa na bunge kuwa ni kiasi Fulani, basi serikali huchukua pesa kuanza kutekeleza miradi ile, ila pia serikali inaruhusiwa kuhamisha pesa zilizotengwa kwa ajiri ya elimu ikaipeleka kwenye barabara ilimradi miradi hii yote iwe inajulikana katika mpango wa maendeleo kwa mwaka husika. Serikali haijawahi chukua pesa ikafanya mradi mwingine mpya bila idhini ya bunge, kama pesa zilizotengwa yaani budget ya mwaka 2017 ni bil 5, basi serikali lazima itatumia hizo hizo pesa, lakini haina limitation ya kwamba ichote pesa kwa mpangilio upi ,lakini ikitokea huo mwaka serikali ikakusanya bil 7, maana yake serikali italazimika kuitisha bunge ili iweze kuizinisha pesa na matumizi ya pesa zilizozidi yaani bil 2.

Vyama vya upinzani, kunyanyasa viongozi wa upinzani kwa kutumia polisi-hili nakubaliana na wew 100%, na hili swala tumepiga sana kelele,na tatizo hili halijaanza leo limekuwepo muda mrefu katika awamu zote, na kweli tunatakiwa tubadilike maana tunatia ukakasi, swali langu tu ni kuwa je kwa nchi za EAC ni nchi ipi ambayo hainyanyasi wapinzani? ndio maana nikasema hapo juu kuwa ukiachia hili la kufukuza na polisi magufuli mengine anajitahidi, nikasema katushika vibaya maana inabidi sasa tuje na sera ambazo zinaeleweka kuweza kukabiliana na uchaguzi ujao.
 
Knock out kapigwa Uhuru
Hakuna mtanzania mwenye akili timamu anaweza kwenda kenya kuomba kazi,wao ndio wanakuja kwetu kupora kazi na wanataka sana ardhi yetu

Understanding levels za watanzania ziko chini sana, unaposema hakuna Mtanzania wa kuomba kazi Kenya una maana gani? na unatafsiri vp kazi? kuna Wanzania wangapi wako Kenya wanafanya kazi na wakenya wangapi wako hapa Wanafanya kazi?

Unapoongelea Industrialization lazima uhusishe Inter trade, unapongelea kushamilisha biashara na uhusiano lazima uuongelee labour mobility under free space environment (The borderless space) Unakuwa na akili za KIJIMA sana, na hii ndo ndo justification tosha ya Tanzania Kufungua mipaka,

u need to learn, mkutane na Wakenya wawatoe tongotongo kwenye akili zenu, na hii inawezekana (we keep our land constant) na tunaruhusu mambo mengine yaendelee, through challenges ndo watu wanajifunza. we still have a very long way to go.....
 
Uamuzi wa Rais Magufuli wa hivi karibuni wa kupiga mnada ng'ombe wa Masai waliovuka kuja Tanzania, uchomaji wa vifaranga na mapokezi ya kiserikali ya Odinga alipoitembelea Tanzania hivi karibuni, wengi wamesema yaliingiza Tanzania na Kenya katika uhusiano mbaya kuliko ilivyowahi kutokea tangu ilipovunjika Jumuiya ya Afrika Mashariki miaka ya 1978.

Wengi walitegemea Kenya ingeanza kulipiza kisasi katika mambo kadhaa madogo madogo na makubwa. Lakini cha ajabu kabisa, wakati wa kuapa kwake, Uhuru Kenyatta ametamka kuwa Watanzania wanakaribishwa Kenya na wahudumiwe kama vile raia wa Kenya wanavyohudumiwa, na hata wakiomba kazi wapewe bila masharti. Uhuru hata akatania kwamba hata Watanzania na Wakenya wakitaka kuoana wasiwekewe masharti!

Taarifa nchini Kenya zinaonyesha kwa kufanya hivyo Kenyatta amemtoa kwa knock out Rais Magufuli katika round ya kwanza kabisa! In fact, wengi wanasema "it must be very embarrassing kwa Magufuli". Wale walio katika mtazamo wa kidini wanasema Kenyatta amemwacha Magufuli ajiwekee makaa ya moto kifuani!

Ushauri wangu wa bure kwa Rais Magufuli ni kwamba pengine sasa ni wakati wa yeye kutafakari kwa kina kwamba kuna mambo katika uongozi ambayo ni kweli yanahitaji utumiaji wa nguvu, u-bulldozer, kwa mfano ufisadi, ujambazi, nk. Lakini kuna mambo mengi sana yanahitaji utumiaji wa busara na diplomasia. Nitawakumbusha machache kati ya mambo ambayo Rais Magufuli alitumia nguvu pale ambapo haikutakiwa kutumia nguvu, tangu kabla hajawa raisi hadi sasa;
  1. Kugomea usafirishaji wa boti za kasi toka Dar kwenda ziwa Victoria - ambapo baadaye Kenya walikubali zipelekwe Ziwa Victoria kupitia barabara zao kutoka bandari ya Mombasa
  2. Kufukuza mkandarasi wa barabara bila kufuata utaratibu wa kisheria - ambapo matokeo yamekuwa bombardier yetu kushikiliwa Canada
  3. Kugomea mega-buses zilizokuwa zikisafirishwa kwenda Zambia kupita barabara ya Tanzam - ambapo baadaye JK aliamuru ziruhusiwe
  4. Kushinikiza jengo la TANESCO libomolewe (wakati wa JK) badala ya kutafuta njia mbadala - ambapo JK alimwamuru Pinda amkatalie kubomoa jengo hilo (baada ya kuwa Rais Magufuli karudi tena kuamuru libomolewe kwa kuwa yeye ndiye Rais sasa)
  5. Kuchoma vifaranga na kupiga mnada ngo'ombe wa Masai waliovuka kuja Tanzania kwa desturi ya Kimasai iliyodumu kwa mamia ya miaka - ambapo Kenya walitoa tamko hawatalipiza kisasi
  6. Kutumbua viongozi kwa mambo madogo madogo kama kutoa kauli asiyoipenda - ambapo wengi wao imebidi waendelee kupata mishahara bila kuwa kazini au kuonekana walitumbuliwa kimakosa
  7. Ubomoaji wa nyumba za watu kulingana na sheria ya eneo la barabara iliyobadilishwa - ambapo kisheria mtu aliyejenga kwa kibali cha serikali au kuishi eneo katazwa muda mrefu bila kuingiliwa na serikali ana haki ya kufidiwa anapobomolewa
  8. Kutoa amri kwa hisia (impulsive directives) - ambapo mara nyingine zimekuwa ni kinyume na katiba ya nchi na hata kuleta migogoro ya kisiasa nchini
  9. Kuzuia safari za nje za ku-ujumla hata zile ambazo zimefadhiliwa na ni sehemu ya uanachama wetu katika tasisisi za kimataifa pamoja na zile za Umoja wa Mataifa - ambapo ushiriki wa Tanzania katika mambo ya kimataifa sasa umekuwa nyuma na kusababisha tukose fursa nyingi za kimaendeleo
  10. Nk, nk, nk

Zihifadhi hizo tutazitumia baadae
 
Believe me, there is a bigger AH, the bigger devil, in one of the East African countries that would not have any qualms about being sworn in as president if there was only 10% of the voter turnout! I have seen all the symptoms.
Duh! You must really abhor the honourable gentleman :D. On second thoughts though, isn't that a measure of great persons of this world especially Africa? What then would you say about the one who could only stand against a "black box"? Would you "disrobe" him of the posthumous saintly aura he enjoys in this great nation of ours?
 
Hivi wewe uliwahi kufika kenya?Husipende kuongea hivyo.Nenda Mombasa,Nairobi na kisumu ndo utagundua kwamba watanzania wamejikita ktk sekta mbali mbali kwa ajili ya kijikwamua ktk shughuli mbali mbali.Mfano mombasa tu eneo la mwembe tayari utafikiri uko usambaani na Moshi vijana wanachakarika ile mbaya.Hapa simtetei mtu ila ninakufungua macho.
Vizuri umempa za akili kubwa na wengine waelewe somo. Watanzania wengi wametapakaa kila kona ya Dunia na kutuma pesa nyumbani ambazo zinakuza uchumo.jaribuni kupata exposure muone fursa na siyo kushinda bongo mkipiga mizinga na majungu
 
Back
Top Bottom