Captain tesha
Member
- Aug 6, 2025
- 88
- 200
Hiki ni kile nilichokishuhudia kwa macho yangu kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na kilichofanyika kwenye so called kuhuisha/kuandikisha wapiga kura wapya.
Ni hivi,
Mwitikio wa watanzania wengi kwenye kujiandikisha na kupiga kura kwenye chaguzi hizi za kipuuzi ni mdogo sana na watu wengi hawajitokezi kwenye kujiandikisha.
Binafsi sijajiandikisha na sitaenda kupiga kura kwenye uchaguzi ujao kwani ni uhuni mtupu unaofanyika.
Kwa miaka 3 sasa, serikali kuu kupitia Wizara ya Kilimo mbolea za ruzuku na sasa Mbegu pia zimewekwa ruzuku. Ili mkulima apate kunufaika na mbolea na mbegu za ruzuku, ni lazima mkulima yule asajiliwe na kupata namba ya ruzuku.
Kazi hii imeachiwa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) ambayo nao wameikamisha kwa wakaguzi wa mbolea ambao wapo Mawilayani na mabwanashamba wa serikali. Ili mkulima asajiliwe anatakiwa awe
1. Anatambulika eneo husika.
2. Awe ni mkazi na anamiliki shamba eneo husika.
3. Awe ana kitambulisho cha either NIDA, Mpiga Kura au leseni ya udereva au barua ya utambulisho kutoka serikali mtaa anayoishi.
Sasa akishasajiliwa anapata namba ya ruzuku ambayo ni utambulisho wa mkulima binafsi lakini pia taarifa zake muhimu hubaki kwenye database ya mfumo wa ruzuku yaani www.ruzuku.tfra.go.tz
Kinachofanyika, wakaguzi wa mbolea kwenye wilaya hutakiwa kudownload majina ya wakulima kwenye wilaya zao ambayo huja na details zake ikiwemo kijiji na namba yake ya NIDA kisha kutumwa kwa maafisa watendaji wa kata au vijiji/mitaa au waandikishaji na hapo huingizwa kwenye mfumo wa uchaguzi na kuonekana amejisajili kama mpiga kura.
Huu ndio uhuni unaofanyika na ndio imeleta ile idadi ambayo Mkurugenzi wa tume ya uchaguzi Tanzania ameisema kuwa watanzania milioni 30+ wamejisajili kwenye database zao kwa ajili ya kupiga kura ilhali watu wamegoma kujisajili na kupiga kura.
Sasa kitakachofanyika (Nilikishuhudia kinafanyika kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa), kwa kuwa details zako za msingi wanazo (NIDA, Kitambulisho cha Mpiga kura, majina kamili, utambulisho wa eneo unaloishi, namba ya simu) utaingizwa kwenye mfumo wa uchaguzi(Daftari) kama hujawahi jisajili na utaonekana umejisajili kwenye daftari la mpiga kura (wataingiza details zako) na pia upige au usipige kura, itaonekana umepiga kura kwani kutakuwa na zile kura za mashetani.
Hili nililishuhudia kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa kwani wale watendaji wa vijiji/mitaa na wasimamizi wa uchaguzi ambao wengi walikuwa Walimu na watumishi wa umma walipiga sana kura hewa na walikuwa wanafoji saini za wananchi/wapiga kura ambao taarifa zao zilichukuliwa kwenye mfumo wa ruzuku.
Mafisi ya kijani hayashindwi kitu. Moderator naomba usiufute huu uzi na pia naomba muuweke Prefix ya uchaguzi.
Nawasilisha.