Uhaya wetu siyo shida, Chalamila tafuta suluhisho

conductor

JF-Expert Member
May 29, 2013
718
570
UHAYA WETU SIYO SHIDA, CHALAMILA TAFUTA SULUHISHO.

Anaandika Mo Mlimwengu.

Kagera ni mojawapo ya mikoa ambayo inajulikana katika nchi ya Tanzania. Mkoa wa Kagera umekuwa ukijulikana siku zote kwa sifa ya kuwa mkoa wenye mandhari nzuri na hali ya hewa nzuri ambayo ni nzuri kwa shughuli za kilimo na ufugaji.

Mbali na hivyo imezungukwa na Ziwa Victoria ambapo shughuli kubwa ya watu wazungukao ziwa ni uvuvi. Mkoa huu umezalisha wasomi wengi ambao almaarufu huitwa nshomire ambao wamesaidia kwa kiasi kikubwa kwenye ujenzi wa taifa letu.

Kagera tumebahatika kupata viongozi wa aina mbalimbali hususani wakuu wa mikoa ambao kila aliyepita hapa alikuwa na aina ya uongozi wake. Ila hivi sasa mkoa huu unaongozwa na Mh Chalamila. Huyu Chalamila amekuja na aina tofauti ya uongozi wake ambao umepelekea watu wengi kushindwa kumuelewa ana shida gani na watu wa Kagera.

Kila akipanda jukwaani ni mtu wa kebehi na kejeli kwamba watu wa Kagera wana fitina na majungu, watu wa Kagera ni wavivu na watu ambao hawapendi maendeleo. Tunaamini Mh Rais wetu Samia Suluhu amechagua mtu wa kuja kumsaidia kuijenga Kagera ila siyo kuleta mtu wa kuja kuwasimanga, kuwasema vibaya, na kuwadhalilisha kwa sifa mbaya ambazo anasema hajawahi kuziona katika mkoa wowote.

Chalamila anasema watu wa Kagera wanaongoza kwa fitina na majungu kuliko mikoa yote. Je anaweza kutuambia huo utafiti aliufanya lini na akalinganisha mikoa ipi. Na je alitumia njia gani kwa hiyo tathmini yake?. No research no right to speak . Watu wa Kagera ni wakarimu sana lakini inapotokea kiongozi kutumia kofia yake kudhalilisha kabila na kutupa sifa mbaya hiyo haikubaliki.

Je hizo sifa anazotoa yeye kama Mkuu wa Mkoa ni watu gani watapenda kuja kuwekeza Kagera. Ni mtu gani ambaye atapenda kufanya kazi Kagera kwa sifa ambazo anazinadi kila siku kwenye vyombo vya habari dhidi ya ubaya wa watu wa Kagera?. Rais hajatuletea mtu wa kuja kutuchafua watu wa Kagera bali kaleta mtu wa kuja kusimamia sera ambazo zitainyanyua Kagera.

Kagera hatuna Stendi ya mkoa, Kagera hatuna soko. Chalamila anasema hayo hayapo kwa sababu watu wana majungu na fitina na wanapenda kuongea viingereza. Je, kujenga Stendi na soko ni kazi ya wananchi au ndio inabidi serikali ijenge.

Tulitegemea yeye kama kiongozi aongoze njia kupata hizo stendi na soko. Lakini anaendelea kutuzomea kwamba hatuna vitu hivyo kwa sababu ya majungu na fitina. Kauli zake zinaonyesha serikali haiko tayari kuwapatia watu wa Kagera stendi na soko kwa sababu wana majungu na fitina. Viingereza vyetu vina mahusiano gani na maendeleo?

Leo hii Kagera ni mkoa wenye uchumi duni kuliko mikoa yote. Tukiangalia sababu kubwa ni athari ya vita ya Idd Amin , kuzama kwa Meli ya Mv Bukoba, Athari ya ugonjwa wa UKIMWI , soko la kahawa kutoeleweka pamoja na kilimo cha migomba kuingiliwa na ugonjwa wa Mnyauko . Na hayo mambo ni serikali ambayo inatakiwa iangalie namna ya kuweka sura nzuri ambazo zitafufua uchumi wa Kagera.

Lakini anakuja Mkuu wa Mkoa ambaye kazi yake ni kuwasema vibaya watu wa Kagera kwa kutusema ni wavivu. Suala la watu wa Kagera kuwa na majungu na fitina pamoja na uvivu umekuwa wimbo wake kabisa. Hii inatuchafulia taswira ya mkoa wetu. Tunaamini kiongozi mzuri ni yule ambaye vitendo vinazidi maneno. Tulitamani kuona initiatives za kupandisha uchumi wa Kagera lakini siyo kutusimanga.

Hivi huo ni uvivu gani ambao anausemea Mkuu wa Mkoa. Je, kufa kwa KCU na BCU ni uvivu wa wana Kagera? Je, kutokuwa na viwanda vya kutosha ni uvivu wa wananchi wa Kagera.

Mshaurini Chalamila aache kejeli na kebehi asimamie sera vizuri ndani ya mkoa wetu tuone kama hatutapata matokeo chanya. Kagera inahitaji usimamizi mzuri wa sera ili kuweza kunyanyuka. Athari zilizopo ni tafsiri ya viongozi kutokuwa wanyambulifu. We reap what we sow (tunavuna tunachokipanda) ukilima chuki utavuna chuki.

Huenda kuna watu wanamsifia kwa kuweza kusema chochote anachojisikia. Yeye kama kiongozi lazima achague maneno ya kusema. Kiukweli kauli zake zimenyongonyesha mioyo yetu, kauli zake zinatudidimiza, kauli zake zinatujengea uhasama na serikali, kauli zake zinatutonesha vidonda vyetu kwa madhira yaliyotupata, kauli zake zina chuki na uhaya wetu na mwisho kauli zake siyo za kiongozi. Baada ya kutatua tatizo yeye anashugulika na uhaya wetu.

Kuna methali moja ya kiingereza inasema hivi " embwa keeba etakahiire mukira teruga mmahiga kwa tafsiri ambayo siyo sisisi ni kwamba anachokitafuta atakipata.

# makeKageraGreatAgain

Screenshot_20230311-122129.jpg
 
Bado mnazileta hizi habari za kumlalamikia Chalamila? Tumeshawaambia jichunguzeni na kujitathimini, tatizo ni ninyi wenyewe, siyo Chalamila.

Mnajidai kuwa nshomile, lakini mkoa wenu unaongoza kwa umaskini nchini; kwani chalamila ndiye kawaletea huo umaskini?

Mna aridhi nzuri yenye rutuba, na mvua zinanyesha vizuri, lakini kimapato mnazidiwa na singida ambayo ni semi desert, huoni kuwa hilo ni tatizo lenu?

Nyie watu wa kagera mna matatizo!
 
Mpaka leo hamna Soko na Stendi??!!!

Hakika WAHAYA mmetawaliwa na Majungu na Fitina!!

Mkoa umetoa Mawaziri kibao lakini eti hata Soko hamna!! Punguzeni ujuaji

Mnasingizia Vita ya Idd Amin wakati mikoa yote iliathirika kutokana na michango ya hali na mali pamoja na askari!!

Mkimsikiliza CHALAMILA mtajinasua kwenye dimbwi la majungu na Fitina.

Chalamila shikilia hapo hapo mpaka wabadilike hawa wajuaji.

Chalamila Hoyeeeee
 
Sababu za uchumi duni :-
1. Vita ya kagera 1978- 1979
2. UKIMWI 1980s
3. Kuzama kwa Mv Bukoba 1996

Kwa kijana aliyezaliwa 1996 barobaro mwenye miaka 27 sasa ataelewa hizo sababu???
Nadhani RC Chalamila atakuwa sahihi Sana!! Acheni majungu, chapeni kazi
 
Mkuu tuache unafiki!!mkoa wa kagera kuna shida tena kubwa sana,mimi nimesoma hapo nimeishi hapo ninawajua vizuri sana!!sisi ambao sio wahaya ilifikia kipindi mwalimu anafundisha kwa kihaya tena ni shule iliyopo hapo mijini(halimashauri ys mji)kwani mnakuta darasani ambao sio wahaya ni kama 4!!

Stendi na soko kikwazo ni madiwani hapo!!daaa wahaya hapana!!hadi ofisi za serikali(mkoani)ilibidi waweke vibao SPEAK SWAHILI!

Mungu akupumzishe peponi Kanali fabian Masawe ukiwa RC pale ulipambana sana na kiasi kikubwa ulifanikiwa!!na kama baada ya kutoka huyu mtu angeingia hapo hapo Chalamira,sasa kagera ingekuwa imebadirika.
 
Mkuu tuache unafiki!!mkoa wa kagera kuna shida tena kubwa sana,mimi nimesoma hapo nimeishi hapo ninawajua vizuri sana!!sisi ambao sio wahaya ilifikia kipindi mwalimu anafundisha kwa kihaya tena ni shule iliyopo hapo mijini(halimashauri ys mji)kwani mnakuta darasani ambao sio wahaya ni kama 4!! Stendi na soko kikwazo ni madiwani hapo!!daaa wahaya hapana!!hadi ofisi za serikali(mkoani)ilibidi waweke vibao SPEAK SWAHILI!!Mungu akupumzishe peponi Kanali fabian Masawe ukiwa RC pale ulipambana sana na kiasi kikubwa ulifanikiwa!!na kama baada ya kutoka huyu mtu angeingia hapo hapo Chalamira,sasa kagera ingekuwa imebadirika.
Itakuwa tumesoma wote ww....enzi hizo fabian masawe ndiye alikuwa mkuu wa mkoa...Tulipanda naye mti kwenye uzinduzi wa hospital mpya ya wilaya hapo bukoba mjini
 
Back
Top Bottom