Uhawara miaka 10

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,877
2,756
Kuna wadau wawili mwanamke na mwanaume. Wote wana ndoa zao. Wameanza kuchakachuana tangu 2001 hivi na hadi leo hawana dalili za kubandukana. Mke mumewe anajua kinachoendelea ila kachemka kuzuia. Sasa hawa wagoni ndio kwamba wanapendana sana? Ndio kusema wangeoana wasingechakachua? Nadhani unapotafuta mwenza tafuta anayekuvutia ili kuepuka haya.
 
Haya mambo bwana,
Mi nasema tu kama Mungu yupo na kama kweli tunavyoamini ndiye anayetupatia mume/mke mwema basi na atuhurumie tu, atukutanishe na wale watu ambao nafsi zetu zinaendana nao!!

Vinginevyo haya mambo sio marahisi kabisa!!
 
mapenzi hayana formula RF....kuna watu wana mivuto na wanaume/wanawake zao wanatoka nje vibaya.....kuna kuchokana,tamaa,nguvu za giza,company,kuoa/kuolewa kwa kulazimisha au kwa sababu nyingine na si upendo kama hela,elimu,umaarufu etc.......nafikiri inabidi kuwepo tu na umakini,busara,utulivu na juu ya yote msaada wa Mungu katika kuchagua wenzi na maisha ya ndoa kwa ujumla wake!!!!!!!!!!
 
absolute! Yan ninakubal ana na wewe asilimia mia moja kwel kwamsaada wa mungu mambo yatakuwa poa ndoa co ki2
 
Mara nyingi watu huwa wanaingia kwenye ndoa na watu ambao hawana vigezo wavyo kuwa wakivihitaji, ndio anapo kuja kuona mtu mwenye vigezo vile anatokea kuanza kumpenda kuliko hata yule aliyenaye.
 
Ndio maana tukaamrishwa tusiingie kwenye mahusiano kabla ya ndoa, na tuingiapo kwenye ndoa tusijihusishe kwenye mahusiano nje ya ndoa. Hii inazuia mtu kujua kwamba mwenza wake ana vigezo au hana, kwa sababu unakuwa huna comparison. Hii ina rule out maswala ya kusema mtu ana vigezo au hana. Tuzingatie maandiko kujiepusha na majaribu kama haya.
 
Wafanye kama bureau de change; wabadilishane ndoa zao ili kila mtu aendelee na hawara yake awe mwenza wake. Hiingiii akilini mtu ujue mwenza wako ana hawara kwa miaka kumi halafu unaridhia tu eti kwa sababu umeshindwa kumuachanisha na hawara yake. Yaani kichwani mwangu nimeshachora katuni ya tukio hili, ni kituko.
 
Nadhani hili tatizo haliepukiki. Wapo watakaomudu kuwa na mwenza mmoja (kama mimi lol!) na wakaishi kwa muda mrefu bila zinaa. Kiukweli kama unayeishi nae unamtamani si rahisi kutoka nje ya mahusiano. Uzuri si kigezo cha kutotoka nje ya mahusiano, bali unautumiaje huo uzuri kumteka mwenza wako?
 
Haya mambo bwana,
Mi nasema tu kama Mungu yupo na kama kweli tunavyoamini ndiye anayetupatia mume/mke mwema basi na atuhurumie tu, atukutanishe na wale watu ambao nafsi zetu zinaendana nao!!

Vinginevyo haya mambo sio marahisi kabisa!!

hope hauko mbali na wazo langu. Halafu...bado hujakutana nae tu?
 
Ndio maana tukaamrishwa tusiingie kwenye mahusiano kabla ya ndoa, na tuingiapo kwenye ndoa tusijihusishe kwenye mahusiano nje ya ndoa. Hii inazuia mtu kujua kwamba mwenza wake ana vigezo au hana, kwa sababu unakuwa huna comparison. Hii ina rule out maswala ya kusema mtu ana vigezo au hana. Tuzingatie maandiko kujiepusha na majaribu kama haya.

hii yako kali. Hana comparison, duh! Yaani haoni huko njiani wala kusikia stori? Binadamu ni mdadisi ndugu.
 
mapenzi hayana formula RF....kuna watu wana mivuto na wanaume/wanawake zao wanatoka nje vibaya.....kuna kuchokana,tamaa,nguvu za giza,company,kuoa/kuolewa kwa kulazimisha au kwa sababu nyingine na si upendo kama hela,elimu,umaarufu etc.......nafikiri inabidi kuwepo tu na umakini,busara,utulivu na juu ya yote msaada wa Mungu katika kuchagua wenzi na maisha ya ndoa kwa ujumla wake!!!!!!!!!!
gaaaal,,,nakukubali
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom