Uhasama CHADEMA, CUF wakolezwa

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
1,225
Tuesday, 29 May 2012 21:16

Geofrey Nyang'oro, Mtwara

CHAMA cha Chadema kimekoleza uhasama baina yake na CUF baada ya kutangaza kuwa moja ya dhamira ya kuendesha operesheni vua gamba vaa gwanda katika mikoa ya Kusini Mtwara na Lindi imetokana na chama hicho kutoonyesha nia ya kuwasaidia watanzania.


Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu Mkuu wa Chadema Dk Wilbroad Slaa ambapo alisema kitendo cha CUF kujiunga na CCM, kimeonyesha kutokuwa na dhamira ya kweli ya kuwakomboa wananchi wa maeneo hayo na badala yake ni kuwanyonya watanzania wanyonge kwa kuwalipisha kodi.

Dk Slaa alikuwa akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika kata ya Mkanaledi.

Mbali na mkutano huo chama hicho kilifanya mikutano kwenye kata zote 15 za Wilaya ya Mtwara mjini.

"CUF tulikubaliana nao,kwa kuwa wote ni wapinzani na wao wana nguvu huku na maeneo ya Pwani ni vema tukawaachia ili waendeleze jukumu la kuwakomboa watanzania"alisema Dk Slaa.


Mikoa ya Kusini na Pwani mwa Tanzania Bara pamoja na Zanzibar tangu kurejeshwa kwa upinzani mwaka 1992 na kufanyika kwa uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi vya siasa, chama cha CUF ndicho pekee kimekuwa kikiungwa mkono na wananchi walio wengi.


"Ndio sababu hatujawahi kuweka mgombea urais katika uchaguzi wowote kwa serikali ya Mapinduzi Zanzibar,lakini kitendo cha CUF kuungana na CCM kimeonyesha dhahiri hawana nia ya kuwakomboa watanzania"alisema.

Dk Slaa alisema wakati wa wakazi wa Mtwara,Lindi na maeneo mengine kuendelea kunung'unika umepita na kinachotakiwa ni kuchukua maamuzi magumu kwa kuikataa CCM na kujiunga na Chadema.

Udini
Akizungumzia propaganda ya udini,ukabila na ukanda aliyodai imekuwa ikitumiwa na CCM kuwalaghai watanzania alisema mwanasisa anayeondoa hoja na kukimbilia siasa aina hiyo amefilisika kisiasa.

"Mwalimu Nyerere alisema,ukiona mtu anazungumzia ubaguzi wa aina yoyote,….udini,ukabila na ukanda huyo amefilisika kisiasa,leo tumekuja kuwafumbua macho ili nanyi muweze kufanya uamuzi kwa kuchambua na kuelewa vema juu ya hoja hizo"lisema.

Dk Slaa aliwataka wakazi wa eneo hilo kupuza hoja hizo kwa kuwa chama hicho hakina dhana ya udini na dhamira yake ni kutumikia wananchi.

"Chadema ilifanya uchaguzi mwaka 2009,kabla hata ya proganda hizo za udini ukabila na ukanda hazijaanza kutumiwa na CCM,katika uchaguzi ule viongozi sita wa juu Waislamu wanne wakristo wawili tena madhehebu tofauti,kama ingekuwa na udini chama hicho kingeitwa dini gani?"alihoji na kuwataka kupuuza aina hiyo ya Propaganda na badala yake kuunganisha nguvu kutetea hoja ya rasimali zao.

Madini, gesi na mafuta
Katibu huyo Mkuu aliituhumu serikali ya CCM kushindwa kujenga mazingira mazuri yamatumizi ya gesi,madini na mafuta yanayotarajia kuchimbwa katika mikoa ya kusini na badala yake kuelekeza nguvu kwa wawekezaji.

Alikosoa gesi,mafuta na madini mengine yanayopatikana katika eneo la Mtwara kuwa kitendo cha wananchi kutonufaika na rasimali hicho ni cha kinyonyaji.

Korosho na Mihogo
Katika mkutano huo Dk Slaa alisema mikoa ya Lindi na Mtwara inaongoza kwa kuzalisha zao la Muhogo na Korosho na kama mazao hayo yangetumika vyema yangesaidia kuleta maendeleo.

"Zao la korosho linalolimwa Tanzania katika mikoa ya Lindi na Mtwara limetoa ajira laki tatu kwa vijana wa India,leo wakulima wa zao hilo wanauziwa kwa kukopwa na pia wakati wa kulipwa wanakatwa michango kibao"alisema Dk Slaa na kuongeza,

"Kama serikali ingekuwa na nia ya kuwaendeleza wananchi wake isingeuza kiwanda cha kubangulia korosho kwa Mama Mkapa kwa Sh 50 milioni na badala yake ingekiimarisha ili vijana wapate ajira"alisema.

Kuhusu zao la Muhogo alisema linamatumizi mengi na kwamba serikali ingeamua kuwekeza katika zao hilo kwa kufungua viwanda,vijana wangepata ajira.

"Muhogo unatengeza karatasi,ni chakula na pia hutumika kutengeza wanga ambao hata polisi hutumia kupigia pasi nguo zao"alisema.
 

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,375
2,000
cuf imeverunda sana kuungana na chichiem... SIKU hizi simsikii hata maalimu akisema chochote..sijui yuko wapi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom