Uharibifu wa mazingira Wilayani Kiteto

koryo

JF-Expert Member
Jun 21, 2010
639
278
Leo tarehe 17.7.2016 saa mbili usiku kwenye taarifa ya ITV imeonyeshwa uharibifu wa kutisha wa MAZINGIRA Wilayani Kiteto. Miti mingi katika msitu imekatwa kwa ajili ya uchomaji wa mkaa wakati viongozi wote wapo. Kwa yeyote aliyeangalia uharibifu huu anaweza kutoa machozi jinsi miti ilivyokatwa ovyo na kwa wingi. Namshauri DED wa Kiteto na RAS wa Manyara kuwa kufikia kesho awe amemfukuza Afisa Maliasili na Mazingira wa Kiteto kazi. Uharibifu kama huu hauwezi kufanyika pasipo yeye kufahamu. KumbeTanzania bado ni shamba la Bibi ambapo kila mtu anajiamulia afanye nini. Kwa kweli uharibifu huu umeniuma sana.
 
Back
Top Bottom