Uharibifu huu wa rasilimali za umma ni kwa faida ya nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uharibifu huu wa rasilimali za umma ni kwa faida ya nani?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Starworld, Jun 22, 2010.

 1. S

  Starworld Member

  #1
  Jun 22, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  HABARINI WANA JAMVI?
  Katika mishemishe zangu nimepitia maeneo ya Mbezi Beach baada ya kipindi kirefu. mara ya mwisho ilikuwa mwaka 2005 kipindi cha karibu na uchaguzi mkuu. Mwaka ule 2005 nilikuta eneo ambalo kwa miaka mingi lilikuwa wazi likikaliwa na jamii ya Kihindi, jamii ambayo ilijishughulisha na kufuga ng'ombe nadhani miaka mingi enzi za mwalimu.

  Cha ajabu ilikuja kusemekana kwamba eneo hilo lilishachukuliwa na serikali za mitaa kama kiwanja cha shule na hivyo nilikuta ujenzi mkubwa wa kutisha ukiendelea na katika kipindi cha chini ya miezi miwili yalinyanyuka majengo kadhaa yaliyonyanyuliwa sambamba hadi ngazi ya lenta! Ama kweli penye pesa kila kitu kinawezekana.Cha ajabu zaidi toka uchaguzi uishe mwaka 2005, hakuna kilichoendelea tena.Naambiwa hayo yamebaki magofu na maficho ya wahalifu.

  Swali je hiyo shule ilikuwa katika mipango yoyote ya Wilaya ya Kinondoni au ulikuwa mpango wa wajanja kutafuna fedha ? Je siyo matumizi mabaya ya pesa za wananchi?

  Mwaka huu, 2010 kuna harakati kadhaa za kutengeneza barabara huko huko mbezi ... mabarabara yaliyokuwa hayapitiki yamepitishwa greda na vifusi kumwagwa. Cha ajabu kifusi hicho kimesambazwa baadhi ya sehemu na sehemu nyingi kikaachwa bila kusambazwa... huku marundo hayo yakiwa kero kwa watumia barabara,Matrekta na magreda yameshaondoka siku nyingi.Je kuna haja gani kutumia mapesa mengi kufanya kazi za ovyo ovyo kama hivi zisizomalizwa?
  Viongozi , je mnaona haya au mmeona na kuridhika?

   
Loading...