Uhandsome wamponza

Uhandsome wamponza

Steven mushi mushi

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2016
Posts
533
Reaction score
741
Ni kijana ambaye ni jirani yetu, sasa huyu kijana huwa anatabia ya kutaniana sana na mama yake mzazi yaani wana ule utani tu wa kawaida wa mama na mtoto. Jana jioni baada ya kutoka shule maana yeye ni mwanafunzi anasoma kidato cha tatu akiwa nyumbani na mama yake wakawa wanataniana kama kawaida yao sasa ndiposa huyu dogo akamtania mama yake kuwa eti kwa jinsi alivyo handsome enzi zake huyu mama kama angekuwepo akamtokea angekataa. Sasa kumbe wakati wanataniana dingi alikuwa ndani na akasikia ile kauli ya dogo aliyemuambia mama akakasirika na akaona Kama ni dharau mtoto kumwambia mama maneno kama yale hata kama walikuwa wanataniana, Baba yake akatoka na kiti na kumpiga nacho mtoto wake lakini kwa bahati mbaya kile kiti kikampiga dogo mguuni na kumtengua mguu na baadaye wakampeleka hoapitali maana kilimuumiza kweli. Sasa huyu dogo leo ndo karuhusiwa kurudi home na analia sana huku akimlaumu sana Baba yake kwa kitendo alichomfanyia ilihali ule ulikuwa tu ni utani na dingi yake naye anasema hakujua Kama kile kiti alichompiga nacho kingemuumiza vile na anadai alikasirishwa na yale maneno ya dogo aliyomwambia mama yake kuwa kwa jinsi alivyo handsome enzi zake angekuwepo akamtokea Kama angekataa. Daah hata kama una utani na wazazi wako wakati mwingine inabidi uwe makini na kauli zako maana wakati mwingine sinawezaleta madhara hata Kama mlikuwa mnataniana
 
Hyo ilivuka mipaka ila na mshua nae naona. Kama wivu ulimshika kias...
 
....isijeikawa hainaga ushemeji wala umaza, dingi kasoma mchezo sio bure....
 
iko siku atalala na mama yake nawaambia, mambo huanza kama utani vile. ilaa mm ningekua baba yake ningempga coz ananiona sina kifaa cha maana
 
Hiyo tu mimi kuna dogo kabisa wa mtaa flani age yake kama miaka mitano hivi sasa mama yak kaumbika balaa sasa mama akipita dogo utasikia, "mama kuda kuda kuda" na mama anatingishwa kama twanga pepeta yaani makusudi
wa mama wengine bwana ni shida tupu
 
Mama angu ndie alikua rafiki yangu mkuu.
hata mimi nilikua namatania mama namwambia mama ulivyo mrembo na nilivyohandsome isingechomoa kwangu,
mama anacheka anasema umekua Handome bcoz of me. mama alivyotangulia mbeleza haki dada zangu ndio watani zangu.

huyo mdingi hajielewi
 
Teh teh hawa vijana wa siku hz hawa hata mama akikaa vibaya wanawezakula hawa yaani hawarembi
 
....isijeikawa hainaga ushemeji wala umaza, dingi kasoma mchezo sio bure....
Kweli mkuu hata dingi mwenyewe alishangaa huu utani ni wa namna gani ndiposa akaamua kumpa dogo kichapo hadi akamtengua mguu
 
Mama angu ndie alikua rafiki yangu mkuu.
hata mimi nilikua namatania mama namwambia mama ulivyo mrembo na nilivyohandsome isingechomoa kwangu,
mama anacheka anasema umekua Handome bcoz of me. mama alivyotangulia mbeleza haki dada zangu ndio watani zangu.

huyo mdingi hajielewi
Ni kweli haya mambo ya utani kati ya mama na mtoto yapo ila wakati mwingine umakini unahitajika
 
Hana adabu huyo mtoto na mama yake......utani na mzazi unatakiwa uwe na vigezo vya heshima......hawa mama wa siku hizi bure kabisa......yaani wanashindwa kabisa kutetea taji la heshima.....!
 
Hana adabu huyo mtoto na mama yake......utani na mzazi unatakiwa uwe na vigezo vya heshima......hawa mama wa siku hizi bure kabisa......yaani wanashindwa kabisa kutetea taji la heshima.....!
Ni kweli kabisa utani kati ya mzazi na mtoto haukatazwi lakini ni lazima uwe na mipaka na sio kwa vile ni utani basi muanze kuongea vitu visivyo na maadili
 
Utani WA namna hii na mtoto mh Mie siwez utani lazima uwe na mipaka..
 
Back
Top Bottom