Idara ya Uhamiaji imeanza kufanya uchunguzi wa madai kuwa meya wa zamani wa Manispaa ya Moshi na mgombea ubunge wa Moshi Mjini, Jaffar Michael (Chadema) siyo raia wa Tanzania.
Michael aliewekewa pingamizi na mgombea wa Chama cha Sauti ya Umma (Sau) , Issack Kireti kuwa ni raia wa Kenya, lakini baada ya kuwasilisha cheti cha kuzaliwa na pasi ya kusafiria, pingamizi hilo lilitupwa na msimamizi wa uchaguzi, Shaban Ntarambe.
Michael amekuwa diwani na Meya wa Manispaa ya Moshi kwa miaka mitano. Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Kilimanjaro, Embrossy Mwanguku alisema uchunguzi kuhusiana na tuhuma za mgombea huyo kuwa ni raia wa Kenya umeanza lakini
akakataa kufafanua.
Chanzo: Mwananchi 28/08/2015