Uhamiaji wawazuia Okwi, Kiongera kucheza Simba

Uhamiaji wawazuia Okwi, Kiongera kucheza Simba

Rugby Union

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2012
Posts
402
Reaction score
257
okwinew.png

Idara ya Uhamiaji Tanzania, imetoa tamko la kuwazuia washambuliaji wawili wa Simba, Paul Kiongera raia wa Kenya na Emmanuel Okwi kutoka Uganda.

Uhamiaji imesema wachezaji hao hawana kibali cha kufanya kazi nchini.

Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Abbas Irovya amesema hawaruhusiwi kufanya kazi hadi watakapopata kibali."Si kucheza mechi tu, hawaruhusiwi kufanya mazoezi na Simba kwa kuwa bado hawajapata kibali," alisema.

Irovya amesisitiza Simba kuwasilisha maobi kama inataka kuwatumia katika mechi au kushiriki nao mazoezi. Pia akashangazwa kuona wanaendelea kucheza huku Shirikisho la Soka Tanzania likiwa kimya.

Wiki iliyopita Idara ya Uhamiaji ilisisitiza suala la wachezaji wa kigeni kupatiwa vibali kwa klabu zao kuwasilisha maombi. Okwi alikuwa na kibali cha kufanya kazi nchini lakini kilikuwa kimetafutwa na mwajiri wake wa zamani, Yanga.
Kabumbu
 
Hiyo nayo ni hoja? Haina mashiko kama vibali walishaomba si uwapatie tu au ndio siasa kila kona
 
wapo watu watalaumu tff takribani wiki inapita nilipost jf okwi hajapata kibali cha uhamiaji kuna watu humu wakaleta visheria vya uchochoroni ni kuniona juha sasa kazi kwenu
 
Kina Okwi mazoezi na hata mechi hawajaanza leo, inamaana hao Uhamiaji walikuwa hawawaoni?
Mpaka TFF inawaruhusu kina Okwi waitumikie Simba Sc "Taifa Kubwa" hawakujua kuwa hawana working permit?

*I Smell Something*
 
Soka la bongo kila kona sinema,ngoja tusubili mwisho wake nini kitatokea kwa hii sinema.
 
Kina Okwi mazoezi na hata mechi hawajaanza leo, inamaana hao Uhamiaji walikuwa hawawaoni?
Mpaka TFF inawaruhusu kina Okwi waitumikie Simba Sc "Taifa Kubwa" hawakujua kuwa hawana working permit?

*I Smell Something*

Keep on smelling that something
 
wanasema okwi ana kibali toka kwa mwajiri wake wa zamani yanga na sio simba
 
Kina Okwi mazoezi na hata mechi hawajaanza leo, inamaana hao Uhamiaji walikuwa hawawaoni?
Mpaka TFF inawaruhusu kina Okwi waitumikie Simba Sc "Taifa Kubwa" hawakujua kuwa hawana working permit?

*I Smell Something*

hizo hadithi za kusema hapa babu yangu alikuwa analima hili shamba kisheria serikali ndio mmiliki wa ardhi unaweza ukapewa au ukanyimwa
 
Kiongera, Kwizera na Phiri washapata working permit, kuhusu Okwi bado wanabana. Rtd Captain Zacharia Hans Pope anadai leo cha Okwi lazima kipatikane.

Kama Mtaa wa 2 walipeleka maombi ya wabrazil wao tangu kipindi cha usajili, lakini hadi leo maombi yao yanashughulikiwa, inawezekana vipi kwa Simba ndani ya masaa 6 wao wapate??!
Ndio maana nikasema,
"I Smell Something".

cc born again pagan mansoorsaid and co.
 
Last edited by a moderator:
Hivi hata wanajumuia ya Afrika Mashariki, kufanyakazi ndani ya jumuia kunahitajika kibali ! Nilikuwa sifahamu.
 
wanasema okwi ana kibali toka kwa mwajiri wake wa zamani yanga na sio simba
Kwani kibali huwa ni cha kuomba kufanya kazi katika nchi fulani au katika taasisi fulani?
 
Hivi hata wanajumuia ya Afrika Mashariki, kufanyakazi ndani ya jumuia kunahitajika kibali ! Nilikuwa sifahamu.

Mkuu kibali cha mchezaji kutoka nje ya nchi kuruhusiwa kucheza nchini hutolewa na FIFA tu.
Na hii huwa haiangalii eti kwa kuwa wote mpo CECAFA basi unahama kishikaji, Hii haipo. Lazma uombe kibali FIFA.
 
Kina Okwi mazoezi na hata mechi hawajaanza leo, inamaana hao Uhamiaji walikuwa hawawaoni?
Mpaka TFF inawaruhusu kina Okwi waitumikie Simba Sc "Taifa Kubwa" hawakujua kuwa hawana working permit?

*I Smell Something*
Kwa hiyo kama hawakuchukua hatua mapema ndio wasichukue kabisa.....hovyo kabisa wewe kumbe RAGE hakukosea kuwaita Mambumbu.
 
Kwa hiyo kama hawakuchukua hatua mapema ndio wasichukue kabisa.....hovyo kabisa wewe kumbe RAGE hakukosea kuwaita Mambumbu.

Simba imecheza mechi kibao, hao uhamiaji walikuwa hawawaoni? Mbona wakiingia wahamiaji haramu nchini kwenye malori hukamatwa fasta tu?
We Kandambili try to think beyond ur "empty" head.
 
Simba imecheza mechi kibao, hao uhamiaji walikuwa hawawaoni? Mbona wakiingia wahamiaji haramu nchini kwenye malori hukamatwa fasta tu?
We Kandambili try to think beyond ur "empty" head.

Upeo wako wa kuelewa naona umefika ukingoni nimekuuliza kama uhamiaji hawakuchukua hatua mapema dhidi ya raia wa nje anayefanya kazi nchini kinyume na sheria basi wasichukue kabisa sababu wamechelewa kuchukua...badala ya kulia na viongozi wenu kwa nini hawajakamilisha taratibu unawaza hujuma tu...ila sishangai RAGE alishamaliza kila kitu.
 
Yanga hao wana mchecheto, wameshaanza fitna kuhofu mechi na Simba....duuh, ushabiki hadi uhamiaji..poor Tanzania!!
 
Back
Top Bottom