Uhamiaji vs JWTZ

Old Member (Retired)

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2012
Posts
3,401
Reaction score
1,618
Habari zenu wakuu,

Nina mdogo wangu yupo JKT, kwa kawaida vikosi tofauti huenda kufanyia usaili vijana waliopo huko mf; magereza, polisi n.k

Sasa huyu mdogo wangu alifanya usaili wa Uhamiaji na JWTZ siku chache zilizopita, elimu yake ni bachelor degree.

Kwa bahati nzuri amepata kote na baada ya wiki mbili wanatarajia kwenda JWTZ na uhamiaji ni baada ya wiki moja, yeye yupo njia panda hajajua aende wapi kati ya uhamiaji au JWTZ.

Hapa jf kuna wazoefu wa kila namna, naomba ushauri wenu. Huyo dogo nimshauri aende Uhamiaji au JWTZ, na kwanini?

Karibuni kwa ushauri wenu wakuu.
 
JWTZ wanalipa vizuri kuliko Uhamiaji but Uhamiaji kuna mianya mingi ya kumake mpunga kuliko JW, halafu Uhamiaji ni kazi ya 'kisharobaro' haina shurba, imekaa kiraia zaidi kuliko kijeshi. Ningekuwa mimi ningeenda uhamiaji
 
Choice ni yake. ...ila uhamiaji panalipa kuliko jwtz. ....ila kama ataenda jwtz na mwisho wa mafunzo akibakishwa jkt basi atakuwa kapata pazuri. .....JKT ni pazuri kuliko JWTZ ukizingatia siku hizi wakimaliza depo hawaunganishi moja kwa moja Monduli.
 

Uhamiaji kuna dili nyingi kama vile kusafirisha wahamiaji haramu, kula hongo za passport na hata kuwatishia baadhi ya watu ķuwa si si wa-TZ na kisha kuwadai hongo.
 
Mwambie aende jwtz ili tulale kwa amani sie
 
JWTZ wanalipa vizuri kuliko Uhamiaji but Uhamiaji kuna mianya mingi ya kumake mpunga kuliko JW, halafu Uhamiaji ni kazi ya 'kisharobaro' haina shurba, imekaa kiraia zaidi kuliko kijeshi. Ningekuwa mimi ningeenda uhamiaji

Uhamiaji wanalipa kiasi gani mkuu?
 
Inategemea anapenda nn yeye kama yeye,kama ameweza kumaliza mafunzo JKT anaweza pia maliza mafunzo JWTZ. Jeshi lina fursa nyingi na pia atapanua akili kwa ku mingle na jamii tofauti duniani,maslahi pia kwa elimu yake sio mabaya ukilinganisha na idara zingine za ulinzi nchini. Binafsi ningemshauri ajiunge JW
 
Inategemea anataka nini?,hela au gwanda.
 
uhamiaji mpango mzima kule ni kumake money tu maana channel kibao.
 
kwa hiyo elimu yake me nashaur aende jwtz.
Kwa sababu uhamiaj wanaopata hizo deal za pasport na wahamiaj haram mara nying ni wale wasio na vyeo (form 4 & 6) sa ye na degree yake lazma atakuwa boss na uboss michongo inapungua tho sijajua mshahara ni kias gan.

Asije jikuta anategemea mshahara tuu
 
Mwambie dogo aende jw, uhamiaji mambo yamebadilika sana na kwa kuwa anadegree jw ni poa sana, kama vp ni pm nikupedetail za uhamiaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…