Uhamiaji imewahamisha Maofisa na Askari (59) kutoka Ofisi za Mkoa wa Dar na kupelekwa Mikoani

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,720
55,859
Screenshot from 2016-06-05 13:27:54.png


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Idara yake ya Uhamiaji imewahamisha jumla ya Maofisa na askari wa Idara ya Uhamiaji hamsini na tisa (59) kutoka Ofisi ya Mkoa wa Dar es Salaam na wilaya zake walikokuwa wakifanya kazi na kupelekwa sehemu mbalimbali nchini.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Projest Rwegasira amesema uhamisho huo umefanyika ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi katika Idara ya Uhamiaji.

Kwa mujibu wa Jenerali Rwegasira zoezi hilo la kuwahamisha Maofisa wa Idara ya Uhamiaji linaendelea kufanyika nchi nzima ikiwa ni hatua za kuboresha utendaji kazi na hivyo kuongeza ufanisi zaidi wa kiutendaji.

Jenerali Rwegasira ameeleza kuwa watumishi wote waliopewa uhamisho wanatakiwa kuripoti kwenye vituo vyao vipya mara moja na kutoa angalizo kuwa mtumishi yeyote atakayeshindwa kuripoti kwa visingizio mbalimbali atachukuliwa hatua kali za kinidhamu ikiwemo kuachishwa kazi.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali.

5 Juni, 2016
 
Watumishi 59 wa Uhamiaji Dar es Salaam wameondolewa. Katibu Mkuu pia ametaka apewe mikataba yote ya ujenzi uliofanywa na Jeshi la Polisi.
 
Hebu tulia ulete habari kamili, naamini wewe ni mwandishi wa habari unajua jinsi ya kufikisha habari,
 
Huu utumbuaji umefanyika leo hii jumapili au ulifanyika jana?
 
Lugumii sijui kawaendea kwa mganga?
Mbona hajaomba mkataba wake?

Inawezekana wizara ikawa haina mkataba wa taasisis iliyo chini yake?
 
Waandishi wa habari nchi hii wengi vilaza wengi waliishia form four wakapata four mbovu wakajiunga na vyuo vya kuunga unga hawana hata uwezo wa kuchambua mambo wanaishia kusifu kila kitu kama makasuku tu
 
huku si ndo kulifanyika interview ya watu 5000 uwanja wa taifa kumbe tayari nafasi zilizoombwa wameshaajiriwa watoto wa wakubwa!!??
 
Hakuna namna mpaka 2025 may be ccm wanaweza shindwa either wise tutaandika sana humu JF bila faida !
Umekuwa mkweli, watapoteza muda kukejeli, kutukana na hilo ni kosa lao kubwa sana. Hawapendi kufunguka na kujifunza kutoka sehemu mbalimbali za dunia. Wanapata faraja ya muda mfupi tu kupitia matusi yao lakini reality ndiyo ambayo CCM wanajua jinsi ya kuhangaika nayo.
 
Safi sana endelea kusafisha nchi baba hao uhamiaji tumelia sana namna wanavyokula rushwa na kuwalinda wageni.
 
Back
Top Bottom