Uhamaji wa wabunge upinzani, kuna umuhimu wa kujifunza kuchagua wanawake?

Gullam

JF-Expert Member
Dec 1, 2013
5,240
3,931
Wasalamu,
Kuna vitu nimejifunza juu ya uhamaji huu wa wabunge wa upinzani kurudi CCM:
1. Wanaume wanaongozwa na tamaa, ujuaji, chuki, husda na kutokujali madhara yatakayotokea nikimaanisha wana umimi.
2. Nimejifunza kuwa wanaume hawana muda wa kusubilia kesho, kwakuwa tu ameshahisi yatakayotokea basi anafanya maaumizi.
3. Nimegundua hawataki kupata ushauri wowote, kwakuwa anahisi atakuwa anaonewa wivu, kwayale matamanio anayoyasubili.
4. La mwisho maana sitaki kuwachosha, mwenyewe nimejaa hasira kifuani mwangu. Wanaume wanaamini katika hela, mali, utawala na vitu kama hivyo. Vile vile wanapenda ulinganifu wa mambo, ndio maana ni lahisi sana kukengeuka.

HITIMISHO:
Kwa muktadha huu unaowapata wanaume sasa, inabidi viongozi wa upinzani wafikirie sana kuwachagua wanawake kugombea nafasi zote za kuchaguliwa, ili kuondoa huu mkanganyiko unaojirudia mara kwa Mara.
Kwanini nawapendekeza wanawake sasa, hapa naweka sababu chache sana, ndani ya nyingi nilizozijua.
1. Wanawake wana upendo kutoka moyoni, waoga, majasiri, wavumilivu pia wanahofu ya Mungu.
2. Mwanamke kabla ya kuamua lazima aombe ushauri tena kwa watu zaidi ya watatu.
3. Mwanamke hakawii kubadilisha mawazo, hata akipata ushauri bado anakuwa na maswali maswali kichwani.
4. Mwanamke yupo kwa ajili ya watu wote, kwake yeye ana waona watoto tu. Kwahiyo wanaitaji kila kilichochema kutoka kwake.
Naomba niishie hapo mwenye la kuongeza aongeze jinsi roho itakavyo muongoza.
Nawasilisha, kila la kheri CCM kwa kupendwa na wabunge tu.
 
Nasikia kuna wengine including wanawake wanatoka muda huu ingawa JF bado kimya.
Mkanyi,zapene n.k
 
Hili nalo ni neno ingawa linahitaji ushahidi wa kisayansi kwa kiasi fulani
Sasa huo ushahidi wa kisayansi utatuchukua miaka mingi mbele. Tunapoupata tu, Taifa lishaangamia. Sasa mnaonaje tuutumie, huku tukiendelea kutafuta wa kisayansi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…