Mtazamo hasi wa jamii unawakwamisha wanawake kuingia na kukua kwenye sanaa

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,115
Sanaa ni kazi za ubunifu ambazo zinatumiwa kuelezea mawazo, hisia, na maoni ya binadamu kwa njia ya kisanii. Sanaa inaweza kuwa katika namna tofauti kama vile muziki, maigizo, uchoraji, uchongaji, ushairi, uandishi wa hadithi, filamu, ngoma, na michezo ya kuigiza. Sanaa inaweza kuwa ya kufurahisha, kuelimisha, kuhamasisha, au kuburudisha, na ina jukumu muhimu katika tamaduni na maendeleo ya jamii.

Sanaa ina faida nyingi kwa msanii baadhi kama
  • Husaidia msaanii kujua kujieleza
  • Kuboresha ustadi wa mawasiliano
  • Kuchochea ubunifu
  • Kuimarisha ujuzi wa kujitambua
  • Kuwasiliana na jamii
  • Kuboresha afya ya akili na ustawi
  • Fursa za kazi
  • Kupata umaarufu
  • Kupata fedha za kujikimu
Wanawake katika sekta ya sanaa wanakabiliwa na changamoto kadhaa ambazo zinaweza kuathiri maendeleo yao na mafanikio katika tasnia hiyo.

Baadhi ya changamoto hizo ni kama ifuatavyo
Ubaguzi wa Kijinsia
: Wanawake hukabiliwa na ubaguzi wa kijinsia kwenye kazi zao za kisana, Wanaweza kukabiliwa na imani potofu kwamba wanawake hawawezi kufanya kazi nzuri kama wanaume au wanastahili malipo ya chini. Ubaguzi huu unaweza kuwa katika fursa za kupata kazi za kwasilisha sanaa zao, malipo, fursa za kuonyesha kazi zao au kupata ufadhili.

Kutokuwepo kwa Uwakilishi: Sekta ya sanaa imekuwa na uwakilishi duni wa wanawake, haswa katika nafasi za uongozi na maamuzi. Wanawake wanaweza kukosa fursa za kuwa na sauti katika kubuni sera, mipango, na maamuzi muhimu yanayoathiri tasnia ya sanaa.

Unyanyapaa na Vitisho: Wanawake wanakabiliwa na unyanyapaa, vitisho, na matusi katika tasnia ya sanaa wengi hutuhumiwa kuwa wanafanya kazi za sanaa ili wapate fursa za kufanya umalaya. Hii inaweza kuathiri ujasiri wao na kujiamini na kuwafanya wahisi kutoheshimiwa na kudhalilishwa na ivyo kukata tamaa na kuacha vipaji vyao vife.

Ushindani Mkubwa: Sekta ya sanaa ni ngumu na ina ushindani mkubwa. Wanawake wanaweza kukabiliana na ushindani zaidi na upinzani kutoka kwa wanaume na hivyo wanahitaji kuonyesha uwezo wao mara mbili ili kuthibitisha uwezo wao.

Upungufu wa Fursa za Kazi na Ufadhili: Wanawake katika sanaa wanaweza kukabiliwa na upungufu wa fursa za kazi na ufadhili. Hii inaweza kuwa kutokana na vikwazo vya kijamii, kiuchumi au mfumo dume unaopendelea wanaume.

Changamoto za Usawa wa Kazi na Maisha: Wanawake wengi wanakabiliwa na changamoto ya kudumisha usawa kati ya kazi na maisha ya kibinafsi. Jukumu la kijinsia na wajibu wa kifamilia mara nyingi huwa mzigo mkubwa kwao, na hivyo kuathiri uwezo wao wa kujitolea kikamilifu katika kazi yao ya sanaa.

Uhaba wa Vigezo vya Uadilifu: Sekta ya sanaa inaweza kuwa na ukosefu wa vigezo vya uadilifu na uwazi katika fursa za kazi, mikataba, na malipo. Hii inaweza kuwafanya wanawake kuwa katika hatari ya kunyanyaswa na kudhulumiwa.

Udhalilishaji wa kingono: Wanawake wamekuwa wahanga wa kudhalilishwa kingono pale wanaonesha nia ya kuingia kwenye kazi za sanaa, wengi huwalahai kingono kwa ahadi za kuwasaidia ili waweze kuwashika mkono

Udhalilishaji mitandaoni: Wanawake waliopo kwenye sanaa wanakabiliwa na janga la kudhalilishwa mitadaoni kwa namna mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutuhumiwa kwa uuzaji wa miili yao, matusi mazito na hata kuitwa majina ya kukera.

Matazamo hasi: Mtazamo hasi kama mwanamke ni wa kukaa nyumbani na kulea watoto umekuwa kikwazo kwa wanawake wengi kuzuiwa na waume zao kujihusisha na kazi za sanaa kwani wanaume huona mwanamke hana umuhimu wa kujishughulisha na kazi za sanaa akishakuwa mke wa mtu.

Kutokana na mchango wa sanaa kwa jamii kukuza uchumi na kuwa fursa ya ajira kwa watu wengi ni vyema watu wawachukulie wanawake kuwa wana haki na wana vipaji ivyo wawasisitize kuingia kwenye sanaa ili waweze kujikwamua kiuchumi, Jamii iondokane na fikra hasi juu ya wanawake wasanii kuwa wapo kwenye sanaa kwa kuwa hawana maadili au wanafanya umalaya kupitia sanaa.
 
Back
Top Bottom