Uhalisia wa mama mjamzito kumchukia 'mumewe'

Uhalisia wa mama mjamzito kumchukia 'mumewe'

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
361,100
Reaction score
831,745
Nimerejea nyumbani baada ya kuzurura mitaani.. Tuendelee sasa na mada zetu.. Leo ni mada tajwa hapo juu
Kuna mengi ya kujadili kuhusu ujauzito na adha zake kama chakula vinywaji na mapenzi ama chuki kwa watu wengine... Lakini kuweka wigo wa mada leo tutakomea kwenye mjadala wa watu watatu... Mama, baba na mtoto mimba.

Mnapokutana jinsia mbili kuna nguvu ya mvuto wa kihisia ndio huwakutanisha.. Nguvu hiyo ikisaidiwa na nyota za wawili hupelekea mahusiano kushamiri na mwishowe ndoa ama kuishi pamoja... Lakini tusisahau kuwa wawili hawa kila mmoja ana background yake, mustakabali wake, nyota yake nknk.....!!

Maisha ya mapenzi na kuwa pamoja huleta zao la mahusiano ambalo ni mimba... Mimba ni ujio wa roho mpya kwenye muunganiko wa roho mbili zilizoungana kupata roho moja... Si mama wala baba mmoja anaweza kujivunia kuwa mtoto ni wake pekee....

Roho mpya iliyo chini ya ujenzi mimba kutengeneza mtoto kamili... Ni roho huru inayohitaji mahitaji kamili ya kiroho na kimwili Kama

. Upendo
. Sifa(kusifiwa)
. Kutambulika
. Kujaliwa utu wake
. Chakula
. Malazi
. Mavazi
. Hisia kama furaha huzuni nk
Hii roho mpya ni mgeni kati ya zile roho mbili, inayosaka mahitaji kama yaleyale ya roho wenyeji... Lakini pia hapo hapo ikiwa ni roho itakayokuwa na mwili wenye tarehe tofauti za kuzaliwa, nyota nk

Nini kitatokea sasa....
Nyota ya mama na mtoto ndio huamua upendo ama chuki kwa baba wakati wa kulea mimba... Hapa kila roho itataka nafasi ileile ndani ya muktadha wa baba, wakati mama bila idhini yake kiroho ataona kama mume hamjali, huku mume akiona kama mke kabadilika... Basi utakuwa ni ugomvi mpaka kujifungua...
Vita ya kugombea nafasi na umiliki ndani ya mtima wa baba kati ya roho ya mama na mtoto hufikia half time mtoto anapozaliwa...

Huu unaitwa nusu ushindi kwakuwa mapambano hayaishii hapo... Furaha ya mtoto ndani ya nyumba kuna wakati inaweza isidumu muda mrefu kama vita ile ya kumiliki, upande wa mtoto utashinda...
Baada ya hapo ni baba au mama atahamishia mapenzi yote kwa mtoto badala ya mwenza... Hata wakipigiana simu cha kwanza kuuliziwa ni mtoto/watoto na si yule mhusika mkuu katika nafasi ya kwanza....

Tufanyeje basi...
Kwa wenzetu wanaozingatia elimu ya roho kinyota huwa makini sana kwenye kuchagua wenza wa maisha... Ni muhimu na ni lazima nyota ya baba iwe na nguvu kuliko ya mama... Ikiwa hivyo mamlaka na umiliki wa jumla huwa kwa baba Kwahiyo hata inapotokea mimba vita ya kugombea nafasi ya umiliki kwa baba huwa rahisi... Yani huwa dissolved na kukuta mama hawi na chuki kubwa kwa mumewe na mtoto mimba haleti rabsha nyingi tumboni na hata baada ya kuzaliwa na baadae makuzi
 
Nafikiri neno chuki kwa maoni yangu siyo sahihi kwani ni zito sana, labda ungetumia neno lingine, binafsi sidhani kama kwa hali ya kawaida mama mjamzito humchukia mumewe au yoyote yule bali ni kwamba tu mood hubadilika kulingana kubadilika kwa bailojia ya mwili, ni mambo ambayo nadhani hutokea tu na hawezi kufanya vinginevyo, kumbuka anabeba kiumbe ndani ya tumbo lake chenye ubongo, moyo, damu kuzunguka na kila kitu, hivyo kutegemea Binadamu kama huyo awe kawaida kama alivyo Binadamu ambaye hana kiumbe tumboni ni kutokutenda haki!

Tuwapende na kuwasaidia Wanawake wetu wakati wote!
 
Ni mada iliyo kiroho zaidi ukiichulia kwa muktadha wa kimwili itakuacha njiapanda na kushindwa kuielewa kabisa
 
Nafikiri neno chuki kwa maoni yangu siyo sahihi kwani ni zito sana, labda ungetumia neno lingine, binafsi sidhani kama kwa hali ya kawaida mama mjamzito humchukia mumewe au yoyote yule bali ni kwamba tu mood hubadilika kulingana kubadilika kwa bailojia ya mwili, ni mambo ambayo nadhani hutokea tu na hawezi kufanya vinginevyo, kumbuka anabeba kiumbe ndani ya tumbo lake chenye ubongo, moyo, damu kuzunguka na kila kitu, hivyo kutegemea Binadamu kama huyo awe kawaida kama alivyo Binadamu ambaye hana kiumbe tumboni ni kutokutenda haki!

Tuwapende na kuwasaidia Wanawake wetu wakati wote!
Wewe binti nenda ukahubiri huko Lumumba huku hupawezi
 
Mkuu mshanajr sisi tusio amni katika nyota tunasaidikaje?.
Hata usipoamini bado zipo na zinafanya kazi... Maisha yako yako connected na galaxy hivyo hata kama huamini bado utendaji utakuwepo tuu
 
Back
Top Bottom