Uhalifu Kwa Mtandao unaoweza Kutokea 2010 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uhalifu Kwa Mtandao unaoweza Kutokea 2010

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yona F. Maro, Jan 5, 2010.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Jan 5, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mwaka 2010 ndio uko mwanzoni kabisa pamoja na ni vizuri tuangalia matisho ya uhalifu unaoweza kufanyika kwa njia ya mtandao kwa mwaka huu ili wengi wetu waweze kuwa makini zaidi .

  Si unajua kwamba mwaka huu kuna Michuano ya kombe la dunia nchini Afrika ya kusini , wahalifu kadhaa wameanza na wengine wameshafanya majaribio kadhaa ya kuuza tiketi feki kwa njia ya mtandao au kumdanganya mtembeleaji wa mtandao aingie kwenye tovuti ambazo ni bandia kwa kujifanya zina mahusiano na kombe hilo la dunia ni mambo kama hayo .

  Je hili la kusajili namba za simu ? kusajili namba ya simu inakuwezesha wewe kuwa karibu zaidi na kampuni za matangazo kwahiyo utegemee kuletewa matangazo mengi sana kwenye simu yako ya mkono na aina nyingine ya uhalifu kwenye simu hiyo hiyo ya kiganja .

  Pia kuna suala la kuangalia sana jinsi tunavyotembelea mitandao ya jamii kama facebook au hi5 kuna wahalifu wanajificha kwenye mitandao hiyo kwa majina bandia au kuweka taarifa ambazo sio sahihi kwa ajili ya kuvutia watu ambao wanaweza kuangukia kwenye mikono ya wahalifu hao mwishowe kutendewa vitendo viovu .

  Ni wakati kwa kampuni mbalimbali zinazoruhusu wafanyakazi wao kutembelea au kuweka taarifa zao kwenye mitandao hii kuwa na sheria maalumu zinazohusu mitandao jamii kuweza kutetea maslahi ya kampuni hizo kwenye mitandao ambayo inahusu jamii kama facebook bila kusahau kingine kwamba taarifa unazoweka kwenye mitandao hii au picha zako zinaweza kutumika dhidi yako wakati wowote bila ya wewe kutegemea kwahiyo ni vitu vya kuangalia sana .

  Kwa wale wapenzi wa kutafuta vitu kwa njia ya mtandao kwenye search engines nao wawe makini sana ni kweli kwamba kuna baadhi ya programu zinazoweza kutambua tovuti na linki mbaya lakini hili sio kwa asilimia 100 na kwa sasa unaweza kutegeka na majibu unayoyapata kwenye tovuti hizo ambazo ukitembelea unaweza kudownload program za kuharibu kompyuta yako na vitu vingine .

  Kwa kipindi cha mwaka jana tumeona jinsi uhalifu ulivyofanyika kwenye mashine nyingi za ATM kwa habari nilizosoma kwenye vyombo kadhaa vya habari zinasema kwamba Mashine nyingi za ATM zimekuwa na matatizo ya hapa na pale ila sijasikia matukio mengine zaidi ya kuibiwa pesa kwa njia hii lakini kuna la kujifunza hapa kwanini Mashine nyingi zinapata matatizo mara kwa mara ?

  Uharibifu wa kitu kama Mashine hizi unaweza kumaanisha uthaifu wa mashine hizo kwahiyo udhaifu huu unaweza kutumika na wahalifu kwa ajili ya kufanya mashambulizi makubwa zaidi kwenye mashine hizi na kwa njia ya mtandao huko mbeleni kwahiyo watu wawe makini sana .

  Na mwisho ni kuhusu mwendo wa huduma za mtandao kwa sasa ulivyokuwa wa kasi kuliko ulivyo huko nyuma , hii inaweza kuvutia wahalifu kwa njia moja au nyingi na ukizingatia hatuna sheria za masuala ya mitandao inawezekana kabisa nchi yetu ikageuka shamba la mashambulizi ya kimtandao kama hali ikiachiwa kuendelea kama ilivyosasa .

  Tusisahau mwendo huu wa mitandao umesababisha watu wengi pia waweze kuchukuwa vitu haswa program nyingi kwa njia ya mtandao ambapo mitandao mengine inatoa program hizi kwa njia ambazo sio halali hizi programu zinaweza kuwa na virus ndani au aina nyingine ya programu za kiuhalifu

  Ni vizuri kampuni na mashirika ya ummah kuwa na sera zao zinazohusu matumizi ya mitandao na vifaa kama komputa na kadhalika ili kuweza kukabiliana na hali hii kwa sababu kampuni nyingi sana zimekubali kuuziwa programu hizi pasipo kujua au wafanyakazi wa kampuni hizi wameuziwa programu hizi pasipo wao wenyewe kujua na matokeo yake ni kufanya uhalibifu ambao kungekuwa na taratibu nzuri ungeweza kuzuilika .

  Haya ni maoni yangu tu hayahusiani na kampuni yoyote au kikundi chochote cha watu .

  www.wanabidii.net www.naombakazi.com www.askmaro.blogspot.com
   
 2. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #2
  Jan 5, 2010
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  mkuu shy sio vizuri kubandika thread kwenye majukwaa mawili wa wakati mmoja, Hivi unajua siku hizi watu wamechoka makala zako za kutafsiri?
   
 3. M

  Magezi JF-Expert Member

  #3
  Jan 5, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Ni kweli kabisa uhalifu wa mtandao na ATM machines utaongezeka mwaka 2010. Nchi kama tanzania ni sehemu watakapo kimbilia wahalifu wa mtandao hasa wa kutumia simu za kiganjani.
   
 4. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #4
  Jan 5, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Samahani sikujua kama nimetafsiri
   
 5. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #5
  Jan 5, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Unaponituhumu kwamba nimetafsiri kazi ya mwingine ni vizuri ukaja na makala niliyotafsiri kutokea huko ili uweze kukubalika na tuhuma zako au weka linki tu inatosha kuongea tu juu juu kwa kulalamika hatutofika badala yake wewe ndio unaonekana hufai
   
 6. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #6
  Jan 5, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  kwa tuhuma hizo nitaacha kuchangia chochote kwenye forum hii mpaka utakapokuja kuuuonyesha ummah hapo nilipotafsiri hizo makala unazosema wewe
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...