Uhalali wa "titles" (Wachambuzi wasemavyo) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uhalali wa "titles" (Wachambuzi wasemavyo)

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Lekanjobe Kubinika, Aug 12, 2010.

 1. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #1
  Aug 12, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Nimeifuma hiyo ikizunguka, nadhani kuitafakari ni faida.

  UHALALI WA “TITLES” NI NINI?

  Kuna aina nyingi za “title” lakini si kweli kwamba mtu yeyote ama bodi yoyote inaweza kuibuka na “title” na kuwapachika watu. Kinachofanyika huwa ni kuwapa watu “sifa za kifani au kitaaluma” yaani “professional credentials” ama ‘academic credentials” na pia vyeo (kama vya kwenye majeshi) na hata heshima tu. Hizi “titles” hazitoki tu kuzimu na kutua kwenye vichwa vya watu. Kwa ufupi kabisa, HAKUNA “TITLES” INAYOTOKANA NA USAJILI wowote ule popote pale, hata kama Wachina, Wajapani na Wajerumani wanafanya vioja hivyo. Kuna “TITLE” moja tu inayozaliwa na shahada moja ya utabibu, “DAKTARI.” Haya tuchambue.

  1. Taaluma kama wahasibu, huchukua shahada, kufanya kazi na kisha kufaulu mitihani ya bodi na kupewa kitu kiitwacho CPA (Chartered Public Accountant) ama ACCA huko Uingereza. Watu hawa hawajikwezi na kutanguliza kabla ya jina eti Mhasibu au Accountant. Watu hawa pia huwa wakaguzi wa hesabu, yaani auditors kwa Kingereza. Wahasibu huweka CPA au ACCA kwenye kadi zao na barua/nyaraka za kikazi/kifani na matangazo ya biashara. Pia wapo Chartered Financial Analysts (CFA) ambao huweka kisifa chao, mbele ya jina lakini kamwe hawawezi kuitwa chochote kabla ya jina.

  2. Aidha, taaluma nyingi zina usajili, mathalani wasanifu majengo (architects) , wachumi wa ujenzi (quantity surveyors ama building economists), marubani, wauguzi, mawakili, na wengineo walimu wa chekechea hapa Marekani, madalali wa nyumba, watunza wagonjwa na vikongwe, washauri binafsi wa fedha, mafundi wa kompyuta, watoa mitihani ya lugha za kigeni, wakaanga nyama, n.k. Wote hawa hawana hiki kioja cha kujiita Pilot Kweche Kwichi ama Architect Kuja Kuondoka. Kulikoni wahandisi?

  3. ENGINEER (MHANDISI): Hii ni sifa anayopata mtu mwenye shahada ya kwanza ya uhandisi ambaye baada ya kufanya kazi ya uhandisi chini ya usimamizi kwa muda fulani na kufaulu mitihani ya bodi ya usajili, hupewa HAKI ya KUTAMBULIWA kama mhandisi (engineer). Anaweza kuandika kisifa hicho mbele ya jina lake kwenye kadi (business card), barua za kikazi na nyaraka za kifani. Hiki si kitangulizi kabla ya jina. Huenda wapo watu kwenye nchi zingine ambao hufanya hivi, hao wamo kwenye kundi moja na Watanzania wetu wanaofanya hivyo. Ni UJUHA na USHAMBA tu. Mhandisi si “title,” bali ni professional qualification na haiwezi kutangulia kabla ya jina, FULL STOP.

  “TITLES” ZINGINE ZINAZOKUBALIKA

  4. Kuna watu kama Reverend au Pastor (Mchungaji) kwa Wakristo ambao kazi zao zinawapa “titles” na pia Sheikh kwa Waislamu na Rabi kwa Wayahudi. Hawa RUKSA hata kama hatuwapendi.

  5. Kuna JUSTICE kwa majaji, hii iko wazi na inakubalika, lakini hakimu hata kama amesoma sana na kufanya kazi kwa miaka 100, hapati kitu. Hii kitu hutolewa na Mkuu wa Nchi.

  6. SENETA ama LORD au LADY ni hadhi za wanasiasa wanaofanya kazi kwenye mabunge ya juu (upper chamberof the House) kwenye nchi zao. Hizi zinatumika kabla ya jina, lakini MBUNGE haina fursa hii, bali inaweza kuwekwa mbele ya jina (suffix) kama MB au MP.

  7. Kuna PROFESA. Hiki ni cheo cha kitaaluma kwenye chuo kikuu ambacho mtu hufikia kutokana na kufundisha, kufanya utafiti, kuchapisha na kufanya kazi kwa muda mrefu huku akipanda vyeo kuanzia uhadhiri usaidizi hadi uprofesa mshiriki ama uprofesa msaidizi na kisha PROFESA. Cheo hiki hakipaswi kuchanganywa na jina la kijumla wapewalo walimu wa vyuo Marekani la PROFESA, kama alivyokuwa Rais Barack Obama. Huyu hakuwa profesa wa cheo bali profesa kumaanisha mwalimu tu, kama ilivyo kwenye Kihispania ambapo mwalimu yoyote hata wa darasa la kwanza ni PROFESOR (“s” moja).

  “TITLES” ZA HESHIMA

  Tunaweza kutofautiana kuhusu uhalali wa “titles” za heshima lakini ukweli ni kwamba watu wamepewa na wanazitumia na hizi hazimsaidii mhandishi yeyote kutanguliza kidokezo MHANDISI kabla ya jina lake.

  1. Kuna watu kama Mwalimu Julius Nyerere ambao walikubalika na “titles” za heshima ambazo hazipatikani kwenye jambo lolote lile. MWALIMU si “title” katika hali ya kawaida, bali ni heshima tu na anaweza kupewa binadamu mwingine.

  2. MAALIM Seif Shariff Hamad amezoeleka kwa kisifa za MAALIM na sina maelezo alikipataje. Naamini ni heshima yake sasa.

  3. Pia kuna watu kama DKT. Kenneth Kaunda ama DKT. Milton Apollo Obote ambao waliitwa hivyo kwa heshima tu lakini hawana sifa hiyo kifani wala kitaaluma. Viongozi hawa bahati mbaya hawakufanikiwa hata kupata shahada moja ya chuo kikuu katika maisha yao.

  4. Mtanzania mwenye heshima ya kuitwa “DOCTOR” lakini bila kuwa na PhD ya darasani, ni SALIM AHMED SALIM ambaye ana shahada ya kwanza ya India na shahada ya uzamili ya Marekani. Ingawa ana shahada za udaktari wa heshima SITA, lakini hiyo si sababu ya kuitwa “DAKTARI” bali ni heshima aliyopewa duniani.

  5. ALHAJ pia ni “title” ya kidini kwa mtu aliyekwenda Mecca kuhiji lakini sifahamu kwa nini wanaokwenda kuhiji Vatican ama Israel huwa hawana “title” hii.

  6. MHESHIMIWA kwa wabunge, MTUKUFU kwa marais, MSTAHIKI kwa mameya, MWASHAMU mwa makadinari, na vingine vya Kiingereza, kama His Highness, au Prince of Wales, au her Majesty, na nyingine nyingi zinaingia katika kundi moja – HESHIMA kutokana madaraka. Hizi haziwasaidii wahandisi kuibua cha kwao.

  7. NDUGU au COMRADE ni kundi moja na BW., BIBI, na BI au MR au MESSRS kwa wingi, MRS., MISS au MS, MDM kwa MADAM, n.k. zote hizi ni heshima kwa mshikaji yeyote. Nawashauri wahandisi wazichangmkie hizi kabla hazijaisha.

  “TITLES” ZA UTANI NA MIZAHA

  1. SIR GEORGE KAHAMA: Kwa utani tu, Mwalimu Nyerere alimpachika jina hili na hatimaye likashika hadi leo lakini ya kudumu. Ili uwe SIR kuna taratibu zake nchini Uingereza mpaka Malkia ama Mfalme akutunukie. Kahama wetu hakupitia humo.

  2. PROFSA MAJI MAREFU: Na waganga wengine wengi wa kienyeji hujiita hivi kama mzaha wa kuvutia biashara na kila mtu anajua hili.

  3. DOCTOR REMMY ONGARA: Ni jina alilojipa kimzaha kwa utani wake kwenye muziki na limeshika hivyo kama lilivyo.

  4. JENERALI HEZEKIAH OCHUKA: Huyu alikuwa mwanajeshi wa Jeshi la Anga la Kenya asiye na cheo aliyeandaa na kufanya jaribio la kumpindia Rais Daniel arap Moi Agosti 1, 1982. Askari wenzake walimpenda na kumwita Jenerali hata kabla hajaleta zahma na kukimbilia Tanzania kwa ndege na mwenzake mmoja.

  5. HIS EXCELLENCY, PRESIDENT FOR LIFE, FEILD MARSHAL, AL HADJI, DOCTOR IDI AMIN DADA, VC, DSO, MC, Conqueror of the British Empire in Africa in General and Uganda in Particular.Pamoja na vibweka vyake na kujipa majina haya, lakini Idi Amin alijua maana ya visifa vya baada ya jina (suffix) kuliko WAHANDISI wetu.

  UHALALI WA “TITLES” YA “DOCTOR”

  Ukiondoa watu waliogushi shahada zao za uzamifu, na kubakiza watu safi, bado mjadala wa nani ni “doctor”unabaki na pia iwapo “titles” hii inaweza kulinganishwa na “title” zingine. Chambua.

  “TITLE” ITOKANAYO NA SHAHADA YA KWANZA

  1. Kuna shahada mbili tu za kwanza duniani kote ambazo humpa mtu “title.” Bahati “title” hiyo ni moja tu: DAKTARI (Dkt) au DOCTOR (Dr) kwa Kiingereza. Nazo ni:

  (a) Shahada ya Udaktari wa Utabibu, yaani Doctor of Medicine kwa Kiingereza au kwa Kilatini Medicinæ Doctor (MD), na hutolewa Tanzania huku Chuo Kikuu cha Colombia, Marekani, kikiwa kilianza kuitoa mwaka 1767. Shahada hii zamani kidogo nchini Tanzania ilijulikana kama MBBS ambayo ni kifupi cha Bachelor of Medicine & Bachelor of Surgery zote kwa pamoja. Jina jingine ni MBBCh, ambayo ni kifupi cha Kilatini kitupu,MedicinaeBac calaureus, Baccalaureus Chirurgiae.

  (b) Shahada ya Udaktari wa Meno, kwa Kiingereza, Doctor of Dental Surgery (DDS) kama kwetu Tanzania, au kwa jina jingine lolote kitakachoamua chuo husika, mathalani Bachelor of Dentistry (BDent) katika vyuo fulani Marekani.

  2. Shahada za kwanzazifuatazo pamoja na kubeba kidokezo cha neno “utabibu” au “daktari” lakini haziwezi kumpa mtu hadhi ya kuitwa “Daktari.” Hizi ni:

  (a) Bachelor Veterinary Medicine (BVM), mathalani ya Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine au Chuo Kikuu cha Cambridge, Uingereza. Ina majina mengine pia. Huchukua miaka mitano katika nchi nyingi kama si zote.

  (b) Juris Doctor (JD) ambayo ni shahada ya kwanza ya sheria katika nchi kama Marekani ambako ni lazima kwanza uchukue shahada nyingine yoyote kabla ya kusomea JD Wamarekani wanaiita JD kuwa ni professional degree, yaani shahada ya fani. Katika nchi zingine kama Tanzania zinazofuata mfumo wa elimu wa Uingereza, shahada ya kwanza ya sheria huitwa LL.B, yaani Legum Baccalaureus, ambayo si lazima isindikwe na shahada nyingine kwanza, kama ilivyo India. Lakini zote huchukua miaka mitatu.

  3. Swali linakuja, je, “daktari” maana yake ni nini? Neno hili la Kiswahili limetoka kwenye neno la Kiingereza “doctor’ ambalo nalo limetoka kwenye neno la Kilatini “doctoris” maana yake ikiwa ni “mwalimu.” Asili ya neno hili si utabibu bali ni ualimu. Kama ungalitafsiri cheo alichojipa Julius Nyerere cha “Mwalimu” kwa kutumia Kilatini, basi ungalimwita “Daktari.” Mjadala wa kwa nini watabibu huitwa madaktari huo siku nyingine.

  4. Jambo la kuzingatia ama kufahamu hapa ni kwamba: HAKUNA ‘TITILE” YOYOTE NYINGINE DUNIANI INAYOZALIWA NA SHAHADA YA KWANZA.

  “TITLE” ITOKANAYO NA SHAHADA YA UZAMIFU

  Kuna shahada za aina mbili au tatu hiviza udaktari usiokuwa wa utabibu, yaani shahada za uzamifu, ambazo humpa mtu haki ya ‘title” ya kuitwa ‘Daktari” au “Doctor.” Nazo ni:

  1. Shahada ya Uzamifu, yaani Udaktari wa Falsafa, au kwa Kiingereza Doctor of Philosophy au kwa Kilatini, Philosophiæ Doctor. Kwa kifupi ni Ph.D. Hii ni shahada ya kitaaluma, kwamba imebebwa na UTAFITI WA KITAALUMA (pure academic research) ikiambatana na UALIMU WA CHUO KIKU. Shahada hizi huweza kuwa katika fani mbalimbali, mathalani kwenye Kemia, Fizikia, Historia, Thiolojia, n.k.

  2. Shahada ya Uzamifu, iitwayo Udaktari wa taaluma iliyosomewa. Mathalani, Udaktari wa Elimu, yaani Doctor of Education na kifupi chake cha EdD, au Udaktari wa Utawala wa Biashara, yaani Doctor of Business Administration au DBA. Hii ni shahada ya kifani (professional doctorate), kwamba imebebwa na UTAFITI WA FANI na haina shabaha ya kumwandaa mhitimu kuwa mwalimu wa chuo kikuu, bali kuwa mtaalamu kwenye fani husika. Shahada za utabibu wa binadamu pia zina heshima hii.

  3. Hata hivyo, kuna shahada za udaktari chache ambazo ni za kitaaluma na si kifani lakini haziitwi PhD. Mfano ni Udaktari wa Sheria (Doctor of Laws) ambayo pia huitwa Doctor of Juridical Science, au kwa Kilatini Scientiae juridicae Doctor, SJD. Shahada hii ni lazima ije baada ya mhusika kuhitimu LLB au JD, na kisha LLM (shahada ya uzamili ya sheria, kwa Kilatini Legum Magistra).Lakini pia iwapo chuo kikuu kitaamua kuita Shahada ya Udaktari wa Falsafa katika Sheria (PhD in Law), hiyo itakuwa ni halali yake.Pia kuna Udaktari wa Sheria za Kanisa, yaani Doctor of Canon Law, kwa Kilatini Juris Canonici Doctor, JCD ambazo hutolewa kwa mapadri na sidhani kama wao hujiita madaktari lakini kitaaluma wanayo haki hiyo.

  4. Jambo la kuzingatia hapa ni kwamba, wahitimu hawa wana HAKI ya kuitwa “DOCTOR” ama “DAKTARI,” mfano Dkt. John Pombe Magufuli. Lakini pia wengine hawatakimtindo huu, mfano, Marekani watu wengi wenye PhD, haundika majina yao bila kitangulizi (prefix) cha “DR” na kisha kuweka kihitimisho (suffix) mbele ya jina cha “PHD” kama hivi, Condoleezza Rice, PhD. Wengine hawafanyi chochote na hatuwezi kuwalazimisha. Kimsingi hata madaktari wa utabibu Marekani, tena wengi tu, huandika majina na kuweka “MD” mbele yake, mfano Sanjay Gupta, MD. Suala hapa ni HAKI ya “TITLE”

  HAKUNA “TITLE” ITOKANAYO NA SHAHADA YA HESHIMA

  Kuna shahada zitolewazo na vyuo vikuu duniani zijulikanazo kama Daktari wa Falsafa wa Heshima au Daktari wa Heshima, maarufu kamaHonoris Causa kwa Kilatini kumaanisha “for the sake of the honor.” Ziko katika makundi mawili. Hizi hazimpi mtu heshima ya kuitwa “DOCTOR” ama “DAKTARI.” Nazo ni:

  1. Udaktari wa Heshima kutokana na mchango MKUBWA wa kitaaluma ama kifani. Hii pia huitwa Higher Doctorate na hutolewa baada ya mtu kuwa na shahada ya Udaktari wa Falsafa (PhD) au ya Udaktari (Doctor of) kwenye fani husika. Shahada hii hutolewa kwa watu mahiri kwenye utafiti na uchapishaji kwenye majarida ya kitaaluma ambao kwa kweli hawapatikani kirahisi. Mfano wake ni Daktari wa Sayansi au Doctor of Science (SD au D.Sc) kwenye taaluma za sayansi asilia kama uhandisi, fizikia, kemia, utabibu, n.k. Pia Doctor of Humanities, au D.Hum kwenye taaluma nyingi zenye mchepuo wa sayansi ya jamii, bahati sina Kiswahili chake. Hali kadhalika, Doctor of Letters, au kwa Kilatini Litterarum Doctor, au D.Litt. kwenye taaluma zisizokuwa za sayansi asilia, ila nasikitika sina Kiswahili chake.

  2. Udaktari wa Heshima kutoka na HESHIMA. Hizi ni maarufu kwa viongozi wa kisiasa kama marais, na watu wengine maarufu na zote ni za udaktari wowote kadri chuo kitakavyoamua. Zinaweza kuwa Doctor of ... mathalani aliyopata Rais Jakaya Kikwete hapa Marekani mwaka 2006 ya Doctor of Law; au PhD in ... mathalani aliyopata John Malecela mwka 1977 kutoka Chuo Kikuu cha Texas iliyoitwa PhD in Humanities.

  3. Jambo la msingi hapa ni kwamba, hawa hawaitwi madaktari, hata wakihonga, hakuna hiyo. Utamaduni wetu Tanzania wa kuwaita wanasiasa wenye nazo eti “madaktari” ni ujuha ama ni kufanya mzaha.

  Mdau, Washington DC.

  [FONT=arial, helvetica, sans-serif]Mpolya, E.A [/FONT]
  [FONT=arial, helvetica, sans-serif]Sendai[/FONT]
  [FONT=arial, helvetica, sans-serif]Japan[/FONT]​
   
 2. Shoo Gap

  Shoo Gap JF-Expert Member

  #2
  Aug 19, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 236
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Profesa Nkunya na vyuo vya kutengeneza shahada

  [​IMG]
  Idd Amiri​
  Agosti 18, 2010[​IMG]
  WIKI iliyopita Profesa Mayunga Nkunya, Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, alizungumza na waandishi wa habari na baadaye akatoa tangazo juu ya kuwapo kwa vyuo vikuu visivyotambulika nchini na huko nje vinavyotoa shahada za udaktari wa heshima wa falsafa kwa wabunge, mawaziri na hata marais. Marais wetu wawili nao ni madaktari wa falsafa.
  Katika tangazo lake kuhusu kuzuka kwa vyuo hivyo, amebainisha kuwa kumekuwa na mbadilishano wa fedha kati ya wahusika na vyuo hivyo na hili ni kwa nia ya kujipa hadhi wasiyositahili waheshimiwa hao kwa wanajamii.
  Profesa Nkunya amekuja na kauli hii baada ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe, kutoa ufafanuzi juu ya kutolewa kwa shahada hizo kutoka katika vyuo hivyo ambavyo kwake yeye hakuviita visivyotambulika au vyuo vya kutengeneza shahada kama Profesa Nkunya alivyoviita.
  Profesa Maghembe alitoa ufafanuzi katika mkutano wa mwisho wa Bunge La Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma. Waheshimiwa aliowataja Profesa Maghembe ni pamoja na aliyekuwa Mbunge wa Kwera, Chrisant Mzindakaya na Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume.
  Katika kikao hicho cha Bunge wakati wa kuchangia mijadala mbalimbali, Juma Ngasongwa, ambaye kwa kiwango cha elimu au usomi ni daktari wa falsafa, alilalamika kuwa pamoja na kuwa na shahada nzuri ya udaktari wa falsafa katika uchumi lakini haitwi member of the learned brothers!
  Mara nyingi wanasheria huitwa hivyo ingawa binafsi sijui inakuwaje msomi mwenye shahada ya kwanza awe katika kundi hilo na madaktari wa falsafa katika fani nyingine wasiwe katika kundi hilo, kwa leo hilo si sehemu ya mjadala huu.
  Profesa Maghembe alisema ya kuwa Mzindakaya amepewa shahada ya heshima ya udakatari wa falsafa kwa kutambua mchango wake katika upenzi, ujenzi na maendeleo ya viwanda na Rais Amani Karume alitunukiwa shahada yake kwa kufanikiwa kutokomeza malaria Zanzibar.
  Lakini hii si mara ya kwanza kuhojiwa kwa shahada za heshima za watu mbalimbali katika vikao vya Bunge. Miaka ya nyuma Dk. Hassy Kitine aliwahi kuongelea suala hilo na aliyekuwa Waziri wa Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia Dk. Pius Ng'wandu alimjibu kuwa haoni kama kuna ubaya wowote kwani hakuna madhara kwa mtu kupewa hadhi hiyo. Lakini hoja ya Kitine ilikuwa zaidi kwa maprofesa wa mitishamba.
  Kwa wale waliowahi kutembelea makumbusho ya Bagamoyo watakuwa wanamfahamu Profesa Kejeli, huyu jamaa ni mahiri kwa kuelezea historia ya mji wa Bagamoyo tena kwa kasi ya ajabu.
  Kumbukumbu za watu, miaka na habari alizonazo Profesa Kejeli kwa kweli zinakuacha mdomo wazi anaposimulia. Nilibahatika kumwuliza ilikuwaje akaitwa profesa alinijibu kuwa alipewa hadhi hiyo na Meshack Maganga (sasa marehemu) aliyekuwa Mkuu wa Chuo Cha Uandishi wa Habari Tanzania (TSJ).
  Miaka mitatu iliyopita nilikuwa nikifuatilia mwendelezo wa kipindi Reality Show cha kila mwaka cha luninga cha Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) katika BBC Two, kinachoitwa ‘You're Fired' ambacho huongozwa na milionea wa Kiingereza Sir Alan Sugar.
  Lengo la kipindi hiki huwa ni kutafuta mtu mmoja ambaye bila kuangalia kiwango cha elimu yake anaweza kuwa na mbinu za kijasiliamali na kimenejimenti kwa kuwaongoza wenzie katika kutafuta faida iwe katika hoteli, kiwanda na mahali popote ambapo uzalishaji kwa lengo la kutafuta faidi unafanyika.
  Mshindi wa mchakato huo huajiriwa katika moja ya makampuni ya milionea huyo na kwa mwaka analipwa pauni za Kiingereza laki moja (100,000).
  Ili kufanikisha mkakati wake huo, Sir Alan Sugar, aliwagawa washiriki wake wapatao 20 katika makundi mawili ya kila upande watu kumi, akawagawia mtaji wa kuendesha biashara ya kufua nguo ambapo makundi yote mawili yalitakiwa kupita kwa wateja majumbani na kujitangaza na hatimaye wateja walikubali kuwapa nguo zao zikafuliwe na kunyooshwa kwa gharama walizokubaliana.
  Hatimaye ikafika wakati wa kuangalia nani kapata nini na kapoteza nini, makundi yote mawili yalipata faidi lakini moja lilipata faidi ndogo na hapo Sir Alan akawa mbogo akitaka kujua nani kasababisha kutopatikana kwa faidi kubwa na kwa bahati mbaya nguo za mmoja wa wateja zilikwenda kwa mteja ambaye siye mwenye nazo!
  Katika kutafuta uzembe ulikuwa wapi alijitokeza mshiriki mmoja katika kundi hilo akapaza sauti kuwa tatizo katika kundi lao kuna washiriki ambao si wasomi, ndipo Sir Alan akamwuliza kuwa ana elimu ya kiwango gani?
  Mshiriki yule akajibu kuwa ana shahada ya uzamili katika uchumi. Swali la mwisho na ambalo lilimwondoa katika ushiriki ule lilikuwa ametumiaje elimu yake katika kuleta faida, mshiriki akawa kimya na Sir Alan hakuwa na la ziada ila kumfukuza huku akisema wale wafanyakazi wake ambao hawana shahada lakini wanamwingizia faida wana tatizo gani.
  Mshiriki aliyekuja kushinda na hatimaye kuajiriwa kwa mshahara wa pauni 100,000 alikuwa ni yule aliyekaa chuo kikuu kwa miezi mitatu na kuacha kwa sababu alionyesha kuwa ana mbinu za kijasiliamali na kimenejimenti za kuweza kuzalisha faida katika kampuni.
  Sasa nirejee kwenye usomi na shahada za bandia na za kweli, hapa najiuliza maswali mengi lakini kwa uchache ni inawezekana vipi kwa msomi ambaye ni profesa kuteuliwa kuwa waziri wa mawasiliano na uchukuzi na baada ya muda fulani anapoondoka wizara ile mashirika karibu yote katika ile wizara yanakuwa taabani?
  Msomi mwingine ambaye ni profesa anaanzisha taasisi isiyokuwa ya kiserikali huku fedha zote za kuendeshea taasisi hiyo zikitoka nje kwa wahisani wake, anajenga jumba lake kubwa la kifahari, ananunua gari la kifahari pia na anasomesha watoto wake ughaibuni na katika kufanikisha mradi anaendesha utafiti ambao mara zote ni kuangalia kama mwanasiasa fulani anapendwa na Watanzania au la?
  Fikra zangu duni ni kuwa baada ya kuwa mtu yeyote amesoma na kuwa na hadhi ya profesa na chuo kumkubali nadhani anatakiwa kuonyesha kwa vitendo thamani ya elimu aliyopata.
  Kwa hiyo unaweza kujiuliza kutokana na yale niliyoeleza hapo juu kuwa hii ndiyo gharama ya kodi za Watanzania walizotumia kumlipia yeye wakati akisoma inasaidia nini kujua kuwa fulani anapendwa au hapendwi?
  Unakuwa na msomi mwingine ambaye ni daktari wa falsafa na waziri vilevile lakini hajui hata kutoka Mwenge jijini Dar es Salaam hadi jimboni kwake ni kilomita ngapi na huyu ndiye anayetakiwa kusimamia ujenzi wa barabara?
  Jambo linalonipa taabu ni kama kwa utashi wangu niwape heshima ya usomi waheshimiwa hawa?
  Upo mfano mmoja hivi inakuwaje kwa msomi kung'ang'ania kufanya kazi katika chuo kimoja tu wakati anaweza kusaidia mahala pengine hata kama si kwa kufundisha, kwa nini msomi kama huyu asifanye kazi nyingine yoyote zaidi ya kufundisha na kufanya utafiti ambao matumizi yake ni yamkini?
  Kwa bahati mbaya nimekuwa nikijikuta nawasilikiza au kuwatazama wasomi mbalimbali wakizungumza katika luninga na redio na wengi ni wakosoaji wazuri.
  Kuna wakati mzee Ali Hassan Mwinyi alipokuwa rais wa Tanzania alikuwa na mshauri wa uchumi ambaye ni profesa na ni huyo huyo leo hii anasema kuwa serikali inategemea sana misaada katika bajeti yake na ijaribu kuja na mbinu za kujitegemea.
  Lakini wote tunajua jinsi nchi hii ilivyopoteza viwanda na raslimali chungu mbovu wakati msomi huyu alipokuwa mshauri wa ‘Mzee Ruksa.'
  Wakati Rais Jakaya Kikwete akitoa hutoba ya kulivunja Bunge, Mjini Dodoma kulikuwa na wasomi wawili ambao walialikwa na Sirika la Utangazaji la Taifa (TBC) ili watoe tathmini yao kutokana na hutoba ile na kwa kuwa ilikuwa na takwimu nyingi hapo ulikuwa ni uwanja wao.
  Kilichonishangaza ni mmoja wa wasomi wale alipokuwa akiunga mkono takwimu zile kwa kusema kuwa zinatokana na utafiti uliofanyika wakati hali halisi haiendani kabisa na yaliyokuwa yakitoka kwenye takwimu zile, hii ilinipa simanzi sana.
  Kwa mfano, katika hotuba ile kulitajwa kuwa umasikini umeshuka kwa kiwango cha kuridhisha na kwa bahati mbaya wiki ile ile katika kituo kingine cha televisheni ilionyesha mama moja akiwa katika kijiji kimoja wilayani Kyela akiomba msaada wa kujengewa nyumba na Wazungu waliokuwa katika ziara ya kujifunza maisha ya watu wa nchi hii.
  Mama yule ana watoto saba ambao bado hawajawa na uwezo wa kujitegemea, yeye mwenyewe ni mgonjwa, nyumba anayoishi ipo mbioni kudondoka, katika hali ile takwimu za Mheshimiwa zilizopata baraka za wasomi zilikuwa sahihi kweli?
  Nirudi kwa kuuliza swali usomi wake umeisaidiaje nchi hii? Kuwa daktari wa falsafa au profesa kama hakuna ulichosaidia kupambana na matatizo ya Watanzania na kwa bahati mbaya ukafanya mambo kama si msomi bado ni hasara kwa taifa.
  Kwa wale tunaofuatilia mienendo ya hawa wote wawili, naamini hatuna shaka kwa sababu zilizotolewa na vyuo hivyo kuamua kuwaenzi kwa kwatunuku shahada za falsafa za udaktari wa heshima kwani michango yao tumeiona na hata Profesa Maghembe alikubaliana na vyuo hivyo kutoa shahada hizo.
  Hivi Karume kuitwa daktari kwa kuwaondolea Wazanzibari gonjwa linalotafuna maisha ya watu chungu mbovu katika nchi za kitropiki kuna ubaya?
  Wasomi wanaotambulika kwa kupitia vyuo vinavyotambulika mbona wameshindwa kuwaangamiza wale mbu pale Hospitali ya Taifa Muhimbili? Mzindakaya kuanzia kwenye uanzishaji wa SIDO hadi kuwa na kiwanda chake mwenyewe hilo ni tatizo? Wasomi wangapi hatujui wameifanyia nini nchi hii?
  Nina mfano moja wa kijana aliyemaliza masomo Chuo cha Maji, Ubungo, Dar es Salaam, miaka ya mwanzo ya 1980.
  Aliporudi kijijini kwake mkoani Iringa alijaribu kufanya matembezi katika moja ya milima inayozunguka kijiji chake, kwa bahati nzuri alifanikiwa kuona chemchem ya maji katika moja ya milima ile.
  Wazo likamjia akawasilisha serikalini na wanakijiji wakafanya harambee ya kuchimba mtaro wa kupitishia mabomba ya maji na yeye akatumia utaalamu wake kukinga maji yale ili yatiririke kuelekea vijiji vya karibu.
  Kwa bahati nzuri Serikali ilimsikia na kwa juhudi na maarifa aliyokuwa nayo mradi ule unatoa maji kwa vijiji zaidi ya 10 leo hii na hakuna hata siku moja maji yamekatika na wanachi wanaulinda mlima ule kama almasi yao.
  Baada ya mradi ule kufanikiwa aliendelea kufanya kazi katika miradi ya maji sehemu mbalimbali nchini na kila alipokwenda na kuondoka wananchi walimlilia, je, huyu akipewa shahada ya heshima ya udaktari wa falsafa kuna tatizo?
  Kuna wakati niliwahi kuuliza swali kwa raia mmoja wa nchi za Magharibi kuwa kwa nini Waziri Mkuu wa Uingereza wa wakati huo, Gordon Brown na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Condereza Rice hawapendi kuitwa kwa majina ya kisomi ya Daktari na Profesa wakati wanastahili hivyo kwa elimu zao? Alinijibu kuwa si vizuri kuitwa msomi na kesho yake ukafanya mambo kama si mtu aliyekwenda shule.
  Lakini hoja ya Profesa Nkunya ni kuwa hapendezwi na tunu wanazopata watu mbalimbali kutoka katika vyuo visivyotambulika na kwa hili yuko sahihi, angependa shahada hizi zitolewe zaidi kwa wale wanaosomea kwa kukaa vyuoni na kusimamiwa na wahadhiri na kwa vile huwezi kupata shahada ya udaktari wa falsafa bila kufanya utafiti kwa vigezo vilivyowekwa na chuo ni dhahiri ni lazima uhenyeke au utaabike kabla hujavaa joho hilo.
  Kwangu mimi ambaye si msomi, sioni tofauti yoyote kati ya viwanda vya kutengeneza shahada kama Profesa Nkunya alivyoviita na vyuo vinavyotambulika.
  Lazima tukubali ya kuwa vyuo vyetu ni mahali pa kwenda kuchukua vyeti ili kupata ajira kwa sababu hilo ndilo sharti kubwa la kuwa na elimu ya shahada ya kwanza, ya pili, tatu hadi mwisho, na hii yote inategemea mshahara atakaolipwa mtarajiwa kwa elimu yake na majukumu atakayopangiwa na ofisi inayomwajiri.
  Hapa ni kama mashindano ya Bongo Star Search kwani aliyeshinda mwaka jana amefanya kazi yoyote ya muziki? Si ni fedha tu ndizo zinazotafutwa kipaji ni jambo jingine. Unaweza kumwiga mwanamuziki unayempenda na kumudu vizuri ili watu wakupigie kura upate mahela!
  Na kwa upande wa shahada ni hivyo hivyo kinatafutwa cheti kwa gharama yoyote iwe kwa kuiba mitihani, kuhonga mwalimu kwa fedha au ngono, kukodi mtu akufanyie mtihani, kunakili utafiti wa mtu mwingine na hata kukodi mtu wa kufanya utafiti wenyewe, suala ni maisha, nani anabisha?
  Si siri kuwa kupata shahada hakuendani na hadhi au muktadha na mantiki ya shahada hiyo, tujiulize wakati tuna wanasheria wenye shahada lukuki, inakuwaje mikataba ya madini inakuwa kama ya machifu wetu wa enzi za kuanza kwa ukoloni?
  Taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuwa chafu na wahasibu wasomi si ndio hao?
  Waandishi wa habari wanaofanya uandishi wa habari kama maofisa uhusiano wa makampuni si ndio hao wenye shahada zao? Makocha wa soka wasioleta kombe hata moja la kimataifa huku si ndio hao wanaotaka waitwee super coach.
  Wahandisi wa barabara zinazoharibika siku ya kwanza ya ufunguzi wakati si ndio hao wenye shahada zao? Wahandisi wa maji wanaotandaza mabomba ya maji wakati wakijua kuwa hakuna maji yatakayotoka si ndio hao hao pia wenye shahada zao?
  Fani zote zina matatizo na zina wasomi wa vyuo vyetu tunavyovipenda sana na kuviita vinatambulika.
  Kutambulika kwa chuo bila ufanisi ni sifuri tu. Kama wasomi wetu wangekuwa wanaonyesha mifano kwa wasiosoma ingekuwa ni halali kuwanyooshea kidole wanaofanya ujanja wa kielimu.
  Msomi hawezi kutuonyesha jinsi alivyoweza kutumia elimu yake kuwa na shamba lenye mazao na mifugo iliyonona, kila siku anafanya utafiti ili iwe nini?
  Kwa hapa nirudi miaka ya nyuma kwa upande wa mahakama. Kulikuwa na mawakili ambao watu wengi walipenda kwenda kuwaona wakitoa hoja zao mahakamani kwa mfano, akina Murtaza Lakha, Ismail Muccadam, Francis Uzanda na baadaye wakaja akina Abass Mselem, Dk. Masumbuko Lamwai na Michael Wambali.
  Wakati huo mashahidi walikuwa na wakati mgumu sana kwa waheshimiwa hawa kwa hoja na maswali waliyokuwa wakiwatupia wakati wakitoa ushahidi wao mahakamani.
  Nilitarajia leo tungekuwa na wanasheria wakali zaidi ya hawa lakini hilo halipo na bado tuendelea kuzalisha kundi learned brothers kila mwaka katika vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi kwani si vinatambulika kwenye mafaili yetu?!
  Kwa waandishi wa habari ambao kwa kweli kwa wakati huo kulikuwa hakuna hata chuo kimoja ambacho kilikuwa kikitoa shahada za uandishi wa habari nchini watawakumbuka akina Stanslaus Katabaro na John Rutayisingwa.
  Hawa wote ni marehemu lakini bado wanakumbukwa kwa sasa kwa jinsi walivyoweza kuwa waandishi wa habari mahiri na kuwafanya wasomaji wa magazeti kufuatilia habari zao kila magazeti yalipokuwa yakitoka.
  Naye Mnenge Suluja alivyokuwa akiandika habari za mahakamani kwa ustadi mkubwa na kumfanya msomaji ahisi kama alikuwapo mahakamani siku ya shauri.
  Leo tunao wenye shahada lukuki, si ndiyo?! Habari gani ambayo wameandika ikionyesha kuwa inaendana na usomi wao?
  Nimeanzisha mjadala huu ili wachangiaji wengine wanisaidie kupata picha halisi ya viwanda vya kutengeneza shahada na vyuo vinavyotambulika kwani mimi si msomi na sina nia mbaya ya kuleta utetezi wa shahada za heshima, tatizo langu ni ujinga na uelewa mdogo nilio nao. Bado sielewi tofauti iko wapi na nini mchango wa wale tunaowaita wasomi waliobobea katika maendeleo ya nchi hii?
   
 3. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #3
  Aug 19, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Shahada ya utabibu Marekani haitolewi kama shahada ya kwanza, kipande hiki hapo juu kinaweza kutoa muonekano kwamba shahada hii hutolewa kama shahada ya kwanza Marekani.
   
 4. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #4
  Aug 19, 2010
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Shukrani sana mwandishi Lekanjobe Kubinika kwa kutoa details za kinaga ubaga..duh yaani mtu unasoma mpaka unatosheka mwenyewe..
  Shoo Gap umesema ya kweli pia, hata kama uitwe cheo gani kama hujafanya lolote la kuonekana katika jamii bado ni kazi bure tu ni kama wale copy and paste.
   
 5. Kurzweil

  Kurzweil JF-Expert Member

  #5
  Aug 8, 2014
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 4,895
  Likes Received: 4,748
  Trophy Points: 280
  Hii post ndio naiona leo.
   
 6. ONTARIO

  ONTARIO JF-Expert Member

  #6
  Aug 8, 2014
  Joined: Oct 16, 2013
  Messages: 1,901
  Likes Received: 15,330
  Trophy Points: 280
  Kitu kimeshiba haswa. Unasoma mpaka roho inasuuzika.
   
 7. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #7
  Jun 19, 2017
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Nii ni thread ya zamani sana, lakini mimi nimeoina kwa mara ya kwanza leo. Nadhani title ya Eng ilitokea Ujerumani na inapatikana katika nchi nyingi za ulaya isipokuwa Uingereza. Kwa ujerumani iwapo mtu ana Ph.D ya Engineering halafu ni Professor wa Chuo kiku huitwa Prof. Dr-Ing. Wale wenye digrii za engineering huitwa Eng. au Ing. makazini kwao. Hizi siyo title standard duniani kwani nadhani zinatumika Ulaya tu, sehemu zote duniani pamoja na zile za commonwelath hawazitumii title hizi. Kwa accountants wenny CPA, huko Marekani wanitwa CPA moja kwa moja ingawa hawaandikwi hivyo; isipokuwa katika mikutano ya kikazi wanaitana CPA ..so and so..
   
Loading...