Uhakiki wa vyeti; Uanze na wabunge wote,Taasisi za ulinzi zote ndipo watumishi wa umma wote.

zubedayo_mchuzi

JF-Expert Member
Sep 2, 2011
4,873
1,216
Habari wadau ??

Nimeona matamko kadha wa kadha kuhusu uhakiki wa vyeti,ushauri wangu kwa WAZIRI NDALICHAKO,uhakiki huo kabla hawajaanza kwa wanyonge,waanze na magrupu yafuatayo.

Grupu la kwanza- Wabunge wote wa bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Grupu la pili-Vyombo vya ulinzi na usalama vyote.

Grupu la tatu; Watumishi wa UMMA WOTE,kuanzia ikulu mpaka mtendaji wa mtaa.

jambo hili likifanyika kwa weledi litatusogeza mbele mnoo.

Mods naomba msi iunganishe hii thread na zilizo tangulia.
 
Umesema kweli tupu. Ifuate mtiririko huo. Watumishi wa Umma wawe wa mwisho. Angalau wapumzike kufanywa wao ni sample ya kutest Hypothesis
 
Nimefurahishwa sana na uhakiki huu wa vyeti feki..na niipongeze sana serikali...

Lakini niseme wazi kuwa kama KWELI serikali ina nia ya dhati ya kuondoa watumishi hewa na vyeti feki basi seke seke hilo pia liende kwenye vyombo vya ulinzi na usalama yaani polisi na jeshi...msiishie kwa walimu na manesi tu..

Mwisho kabisa niombe serikali ifanyie kazi ushauri wa profesa Shivj alioutoa hivi karibuni wa namna bora ya kuboresha elimu..
 
Jeshini? He he heee! Wee jamaa mchokozi sana, mimi hapa ngoja nisitie neno nisije nikazingirwa!
 
Naona kama Jeshini hakuhitaji Uhakiki wa Jeshi.

Kwani ujasiri wa Mtu kushika mtutu au kuwa tayari kufa kwa ajili ya Nchi yake unapimwa na kiwango chake cha Ufaulu?
 
hiki ni kiama!!! huenda nusu ya walimu na polisi nchini wana vyeti visivyo vyao na waliingia kwa sifa zisizo zao na wanatumia majina yasiyo yao. Inatisha! Vyeti??? Kuna ofisi zitabaki tupu
 
huwa si mchangiaji lakini kwa hili zebedayo mchuzi umenikoshaaaa sanaaaa......hivi vyeti vya bandia vipo kwa watumishi wadogo tu? sheria ni msumeno Na ukate pande zote hakika. nalog off
 
Kuna kundi ukiwarudisha mitaani wataleta hofu,mh kazi zao mnazijua.Waachwe tu huko waliko.
 
wazo zuri na huko wakiwakuta hapo ndo tupime nchi imeharibika kiasi gani coz ktk nchi jeshi ni sekta nyeti..
 
Mkuu ni uonevu tu maana wanaokaguliwa vyeti feki ni hili kundi moja tu.Akifika na huko ntaamini amedhamiria kupambana kweli.
 
huwa si mchangiaji lakini kwa hili zebedayo mchuzi umenikoshaaaa sanaaaa......hivi vyeti vya bandia vipo kwa watumishi wadogo tu? sheria ni msumeno Na ukate pande zote hakika. nalog off
sitaki kabisa waende kwenye majeshi na wabunge na viongozi....
 
Nimefurahishwa sana na uhakiki huu wa vyeti feki..na niipongeze sana serikali...

Lakini niseme wazi kuwa kama KWELI serikali ina nia ya dhati ya kuondoa watumishi hewa na vyeti feki basi seke seke hilo pia liende kwenye vyombo vya ulinzi na usalama yaani polisi na jeshi...msiishie kwa walimu na manesi tu..

Mwisho kabisa niombe serikali ifanyie kazi ushauri wa profesa Shivj alioutoa hivi karibuni wa namna bora ya kuboresha elimu..
Hakuna sehemu wanakagua vyeti kwa umakini kama jeshini kama unamtu huko ulizia,unapotaka kujiunga rts kwenye usahili yupo mtaalamu wa maswala ya vyeti ambaye alikuwaga necta.kwa wale maofsa usahili wao anakuepo mtu wa rita tcu necta usalama wa taifa.uliza wangapi wanakimbiaga na kuacha vyeti vyao,sema advantage jeshini wanaajili mpaka darasa la saba so mnavyoona watu kibao walifeli wapo kule mkajua magumashi kumbe waliingilia cheti cha lasaba wao wanawaita la masela
 
nguvu kubwa ya kufikiri. wanakawaida ya kuanza na sisi walimu, sasa hii hatua itakuwa njema ktk Kutatua hili. WALIKAGUA WABABE WAKAACHWA WANYONGE .........
 
Back
Top Bottom