Baraka Mina

JF-Expert Member
Sep 3, 2020
581
574
Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere alisema mwaka 1995 kuwa "Ukipewa kazi ya nchi, lazima ujiheshimu. Huwezi kupewa kazi ya nchi halafu ukaishi kihunihuni." Ni kweli kuwa dunia inaenda kasi na pia wakati ni ukuta; muda ni mchache na mambo ni mengi lakini kama umepewa kazi ya nchi ni lazima ujiheshimu. Ndugu zetu wabunge na watumishi wa umma kuna sauti ya mtu iliayo nyikani. Tafadhaini itengenezeni njia na yanyosheni mapito katika kazi za nchi ili sisi sote tupate kuyaona maendeleo jumuishi ya nchi.

Jana tarehe 08/07/2021 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo akiwa Sumbawanga mkoani Rukwa alitoa maagizo mawili ambapo agizo moja lilienda kwa wabunge na jingine lilienda kwa watumishi wa umma.

WABUNGE
Kuna wabunge tangu kuahirishwa kwa mkutano wa 3 wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bungeni jijini Dodoma Juni 30, 2021 bado hawajarudi majimboni, wako Dodoma, Dar Es Salaam, Njombe, Kigoma ama wapi jamani? Mimi na wewe hatujui ila sauti iliayo nyikani imetoa maagizo ya Chama kwa kuelekeza "Maagizo kwa Wabunge wote, lazima warudi kwenye majimbo yao kule walikoomba ridhaa ya kuwatumikia wananchi na wahakikishe wanawapelekea taarifa ya kilichopangwa kwenye bajeti kwa ajili ya majimbo yao."

Sisi wananchi tunawasubiri huku majimboni kwa ajili ya kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM 2020 - 2025 hususan katika suala la fedha za barabara za vijijini zile milioni 500 kwenye kila jimbo na zimeshathibitishwa. Karibuni na njooni tutatue changamoto na kupata maendeleo kwa sababu kupitia hiyo fedha katika barabara za vijijini kila bonde litajazwa, kila mlima na kilima kitashushwa, palipopotoka patakuwa pamenyoka na palipoparuza patalainishwa.

WATUMISHI WA UMMA
Ukiwa mtumishi wa umma una wajibu wa kuwa mwadilifu, kuhakisha wananchi wanapokea huduma bora na unakuwa mzalendo kwa taifa (maslahi kwa taifa yanatangulizwa mbele). Kuna mkwamo wa upatikaji wa dawa; sauti iliayo nyikani imesema kwamba itawasiliana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk. Doroth Gwajima, pamoja na uongozi wa Bohari ya Dawa (MSD) kujua mamilioni ya fedha yanayotolewa kwa ajili ya kuwezesha upatikanaji wa dawa yanakwama wapi? “Watueleze (Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto) nani anasababisha mkwamo katika upatikanaji wa dawa. Viongozi tuna wajibu wa kufuatilia na kusimamia thamani ya fedha katika kila eneo.” Amesema Ndg. Chongolo.

Sambamba na hilo amewaonya watumishi umma juu ya fedha ya umma kuwa CCM haitacheka na mtu “Tutakuwa wakali, ni lazima tuogope fedha ya umma. Ukizitumia vizuri (fedha za umma) zitakujengea heshima, ukizitumia vibaya zitakuvunjia heshima. Kila mmoja anapaswa kuwa mwadilifu.” na pia akasititiza uwajibikaji “Ni lazima tufanye kazi yenye tija. Wananchi wakiona mambo hayaendi, watatuona sisi (CCM) tunapiga porojo. Hatuko tayari kuitwa wapiga porojo.”

Ndugu zetu wabunge na watumishi wa umma tubuni pale mlipokosea, fanyeni kazi kwa bidii, nyosheni utendaji na kuwa wema katika matendo maana wakati umekaribia kama mlivyoisikia sauti ya mtu anaita jangwani kwa kuwa atakayekuja baada ya huyu ana nguvu kuliko sauti hii yeye anashika mkononi chombo cha kupuria nafaka ili aipure nafaka; akusanye ngano ghalani na makapi ayachome kwa moto.
 
View attachment 1847346
Sasa kama ni wakukumbushwa majukumu ya kumtumikia mwajiri wao,sio kuwa kunashida katika kuajiriwa kwao,tujikumbushe uchafuzi mbili,ule wa mitaa na ule wa sirikali kuu 2019 na 2020 okutuba.
 
Wanakumbushwa kukitumikia taifa kwa ajili ya maendeleo ya watanzania wote.
 
Hili la ukosefu wa dawa katika vituo vya afya linaleta ukakasi sana na haswa:-
1)Iwapo fedha zinapelekwa kulingana na bajeti iliyopitishwa na kwa muda muafaka;
2)Bajeti inayoombwa inakidhi mahitaji halisi ya dawa, vifaa tiba na vitendanishi;
3)Wasimamizi na timu za usimamizi wa masuala ya afya zinafanya kazi na kuwajibika ipasavyo;
4)Watumishi wa kada husika za afya wanawajibika ipasavyo.

Vinginevyo kila siku itakuwa ni vilio.
 
Ndg. Chongolo ameahidi kulifuatilia lakini katika siku za karibuni kulibainika madudu katika suala la dawa. Wale wapigaji lazima wachukuliwe hatua.
 
Arudi kufanya nini si alipita bila kupingwa.
Mahitaji ya wananchi yako sawa jimboni.
Kama hayupo anatakiwa kurudi kwa sababu yeye ndiye kiongozi wa jimbo lile. Aende akasimamie maendeleo na kuhakikisha anatekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM 2020 - 2025. Uongozi ni wito.
 
Kwa hiyo na wale 19 hili agizo linawahusu?
Haliwahusu kwa sababu wale wanatokea CHADEMA, John Mnyika atawaita katika kikao cha Baraza Kuu la CHADEMA kusikiliza rufaa zao maana bado mpaka leo rufaa hazijasikilizwa ila CHADEMA wanafanya shughuli nyingine na kuacha hili jukumu ambalo inabidi lifike mwisho ili tuendelee kuijenga nchi.
 
Unazungumzia watumishi wa umma wapi? Mkuu hawa hawa ambao wanasubiri barua za kupanda madaraja au wapi
Ni watumishi wa umma hawa ambao wamepandishwa madaraja na wengine watapandishwa na PAYE imeshushwa sambamba na kufutwa kwa tozo ya 6% iliyolenga kutunza thamani ya fedha za mkopo (retention fee).
 
Back
Top Bottom