Uhaini wa Mtwara ulipangwa

TandaleOne viongozi wa CCM Mtwara wameanza kuwakimbia kwa kuwa msimamo ya CCM ni kujitenga na Wanamtwara na matakwa yake.
Taarifa nilizozipata kwa ndugu yangu kutoka mtwara ni kwamba baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi mkoani Mtwara wameanza kuachia nafasi zao na kuungana na wananchi wa mji huo kupigania gesi iwanufaishe

Mtoa taarifa wangu ameeleza kuwa leo hii majira ya asubuhi kiongozi wa Chama hicho kata ya Mjaengo ametangaza kupitia redio moja mkoani humo kuwa anawarudishia kadi yao na wasimuhesabu kama kiongozi wa Chama hicho na mwanachama wao
 
Last edited by a moderator:
@ KIbe; mimi nianze kwa kusema inawezekana kweli huo ni uhaini ulikuwa umepangwa nadhani umejiridhisha kutokana na sababu zako, ila kwa upande mwingine zinaweza kuwa hasira za wananchi dhidi ya serikali ya ccm namna inavyosimamia rasilimali za eneo husika, mimi sikubaliani kabisa na pongezi zako kwa vyombo vya usalama, Huo ni ujinga na udhaifu mkubwa tena hata kwa viongozi/wanasiana wenye mtazamo kama wako. Pia ni udhaifu kwa kiongozi eti kuna watu wanaongoza uhaini huo, hivi usalama wa taifa uko wapi, unafanya nini, je polisi walikuwa hawajui hilo? na kama walikuwa hawajui au wanajua wakashindwa kuchukua hatua wameprove failure? nachukia sana kusikia kauli kama zako na akina Kilango malecela eti kwa sababu ya gesi na mafuta kuna watu wanatungombanisha ili wavune rasilimali, ndiyo inawekekana, je anafanyanini bungeni na serikali yake inafanyanini kuwadhibiti hao watu? kama haina uwezo huo basi haina uhalali wa kuongoza nchi? mimi natarajia kuona vurugu zaidi huko mbeleni kwani Mfumo wa kuendesha nchi yetu unadhibitiwa na ikulu yaani think tank ya nchi ni raisi akiamua amemua na hiki mi ndo naona kama ndo chanzo kikumbwa cha vurugu na ufisadi unaoendelea nchini. mwisho SERIKALI YA CCM NA WABUNGE WA CCM NDIO WATAKAO ANGAMIZA TAIFA HILI KWA UBINAFSI NA KUJIFANYA WAO NDIO WANAHAKI YA KUWAAMULIA WATANZANIA JUU YA RASILIMALI ZAO. I LOVE MY COUNTRY TANZANIA
 
Leo asubuhi ya saa mbili na dakika 56 (08:56:16am) nimepokea ujumbe wa simu kutoka kwa mmoja wa Viongozi wa juu wa Chama Cha Mapinduzi CCM, ambae kwa cheo ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC). Ujumbe wenyewe ni huu ufuatao:

Ujumbe huu uliniongezea simanzi na majonzi niliyonayo juu ya maafa mbalimbali yaliyojitokeza katika vurugu za Mtwara jana. Simanzi hii ilitokana na kuona hali ya unyonge, woga na wasiwasi mkubwa walionao viongozi wenzangu wa Chama, wasiwasi huo hautokani na woga wa kitoto bali kutokana na hatari wanayoiona mbele yao ya kuwindwa, kushambuliwa na kufanyiwa hujuma na matendo mengine ya kudhuru mwili.

Swali la msingi na lenye kufikirisha ni kwanini wahaini hao wanawalenga wanaCCM..? je inaweza kuwa watu hao wanamlengwa mwingine wa kisiasa ambao unakinzana na CCM hivyo kuifanyia CCM na Viongozi wake mambo haya..? Sitaki kuamini kuwa vurugu hizi zina unasaba wa aina yeyote na Siasa zetu hapa nchini bali najilazimisha kuamini kuwa vurugu hizi ni hujuma na uhaini unaofanywa na wahuni, wahaini ambao hawaitakii mema nchi yetu. Najilazimisha kuamini hivyo kutokana na maana halisi ya Siasa, ama harakati za siasa kuwa hazihafikiani na kinachofanyika mtwara, bali vitendo hivyo vinashabihiana na maana ya hujuma na uhaini kama ifuatavyo.

Maana ya maneno mawili ya mwanzo ya yaani hujuma na uhaini yanafuatana kwa maana hujuma inaweza kutumika kama mkakati wa uhaini. Uhaini ni tendo la kusaliti nchi, serikali au mfadhili; uasi. Hujuma ni shambulio ama vamio: fisidi, kuvuruga ama kuharibu.

Maana ya kipengele cha tatu ambacho kimebeba maneno mawili harakati na siasa, ama siasa ina maana ni mfumo wa mawazo yaongozayo utawala wa serikali ya nchi tafsir nyingine ni utaratibu wa utekelezaji au uendeshaji wa jambo kwa kutumia busara na hekima ili kufikia lengo linalotarajiwa.,na maana ya neno la mwisho yaani harakati ni juhudi zinazoafanywa na watu kwa ajili ya kufikia lengo fulani, bidii, jitihada.

Katika tafsir hizo tatu, kinachoendelea mtwara hivi sasa tunakitoa kabisa katika maana halisi ya harakati za kisiasa, kwa kuwa maana ya harakati za kisiasa ni juhudi za kupanga utaratibu wa mfumo wa mawazo yaongozayo (ama yanayolenga kuongoza) utawala wa serikali ya nchi.

Kwa maana ya Hujuma kuwa ni shambulio, kuvuruga ama kuharibu ni sahihi kwa upande mmoja kuwa hiki ndicho kinachoendelea mtwara lakini kwa tafsir ya uhaini ndiyo hasa inayoelezea kinachoendelea Mtwara.

Ndio ni uhaini uliopangwa na kutekelezwa na watu wenye nia mbaya na nchi hii, wasio wazalendo na waliokosa utaifa. Wanaoendesha mkakati wa nchi kutotawalika, kwa kuibua hujuma mbalimbali dhidi ya serikali na chama kiendeshacho serikali hiyo yaani CCM.

Sio ajenda na hoja ya gesi, bali hoja hii imetumika kimbinu kuendesha mkakati huu wa kihaini ambao unawawinda wanaCCM, ofisi zao, mali zao pamoja na serikali yao. CCM ni chama cha siasa kinafanya siasa ya kuendesha nchi hii, vipo vyama vya upinzani navyo vinalenga kuelekea katika mlengwa huu wa kisiasa, lakini wakati mwingine vinapotoka na kuacha Siasa ama harakati za kisiasa na kujikuta wakifanya hujuma na vitendo vingine vya kihaini. Kwani kama hoja ni gesi vipi vurugu zilenge katika mali, ofisi na uhai wa wanaCCM..?

Tandale onembona unaandika kama Kibe?
Kibe, mbona unachambua kama Tandale one?
Who is who in who?
 
TandaleOne, kutokana na posts zako hapa umejidhihirisha kuwa wewe ni kiongozi wa CCM.

Kwa nini huji kwa jina lako halisi ili kuyapa nguvu maneno yako. Humu JF wamo akina Nape Nnauye, Mwigulu Nchemba, Hkigwangallah, Dr. F. Ndugulile, John Mnyika, Zitto, Tundu Lissu, Dr. W. Slaa na wengine wengi.

Please jitambulishe na uendeleze uwazi na ukweli.
 
Last edited by a moderator:
Ninachosikitika ni kuwa wakati tumekubaliana na TandaleOne kwamba tujadili mjadala huu kwa hoja ili kupata kiini hasa cha tatizo; mpasa sasa keshaukimbia mjadala wake aliouanzisha na sijui kama atarudi tena.Akirudi atarudi kama guest.

Nimepata shida kuona kuwa asili ya uzi wangu imebadilishwa na kuchanganywa na hoja isyo na mfanano wa kimsingi na hoja yangu. Lakini pamoja na hilo, sina jukumu la kushinda JF bali ninaipa nafasi nikifahamu ipo cyber society ambayo ni muhimu kuifikia na kuifahamisha. Ninapopata muda wa kushiriki nashiriki ipasavyo ila ningependa mods waipe hii thread haki na uhuru wa kujadiliwa.
 
Watanzania tumeze moto tu hata kama moto ...ukweli kwa hali iliyokuwa inaonekana na kilichotokea jana hapa Mtwara ukweli ulio wazi jambo hili lilipangwa na wako wanaoliongoza ila walikuwa wanangoja sababu ya kuanzia kutekeleza uhaini wao... Cha kushangaza kwa vurugu zinazolipuka wakati huo huo ni nadra kuyapata mabomu ya samaki na magobore, mapanga... Hili jambo tukatae tukubali lilipangwa na wako wanaofanya mipango hiyo.. Na walipanga wafanye hiki na hiki...

Binafsi nawapongeza jeshi la polisi kwa jitihada zao walizozitumi kunusuru hali isiendele kuwa mbaya ukweli hata mkiwabeza lakini ukweli uko wazi wamesaidia kwa kiwango kikubwa..Tukumbuke pia si wananchi wote wanapenda kinachoendelea hapa Mtwara. Naomba JWTZ endelee kuangalia hali inavyoendele ili amani iwepo msiingie kazi kutekeleza sheria za kijeshi mana khali itakuwa mbaya zaidi kwa wananchi mana jeshi 99% mafunzo yao ni kuua..

Shime watz turudi nyuma tuache ushabiki wa kisiasa tuliangalie hili jambo kiiundani zaidi na nyuma kuna nini tusiingizwe kichwa kichwa .

Mimi nakushangaa sana, yaani hii nayo ni habari ya kujadili? Unadhani hayo yanaweza kufanywa bila kupangwa? Nani ameyapanga si wana mtwara wenyewe? Hili walilitahadharisha muda mrefu lakini serikali "sikivu" ikapuuzia tu. Ni kama chokochoko za kidini zilivyoanza halafu Mr Dhaifu na watu wake wakakaa kimya. Baada ya mambo kulipuka wanjidai tutawachukulia hatua wote!!!! Akina nani? mbona matukio yametokea kibao hatujasikia hata mtu mmoja amechukuliwa hatua?

CCM na Serikali yake imeshajishindwa sasa ijiandae kukaa pembeni ili watanzania wengine waongoze nchi.
 
Nimepata shida kuona kuwa asili ya uzi wangu imebadilishwa na kuchanganywa na hoja isyo na mfanano wa kimsingi na hoja yangu. Lakini pamoja na hilo, sina jukumu la kushinda JF bali ninaipa nafasi nikifahamu ipo cyber society ambayo ni muhimu kuifikia na kuifahamisha. Ninapopata muda wa kushiriki nashiriki ipasavyo ila ningependa mods waipe hii thread haki na uhuru wa kujadiliwa.
Mkuu TandaleOne usiwe na tabia ya kujishuku kwamba unadhulumiwa. Unatakiwa uelewe kwamba KIBE ndio wa kwanza kuanzisha uzi kuhusu masuala ya kuhusisha kinachoendelea mtwara na uhaini na ni kitu cha kawaida kwa nyuzi zenye maudhui yanayofanana kuunganishwa ili kukusanya mawazo ya wachangiaji na ndio maana unaona zote zimekaa pamoja.Sasa cha msingi hapa tujadili hoja.Nataka ujibu hoja zangu hapo juu maana ulisema unataka facts.
 
Last edited by a moderator:
Watanzania tumeze moto tu hata kama moto ...ukweli kwa hali iliyokuwa inaonekana na kilichotokea jana hapa Mtwara ukweli ulio wazi jambo hili lilipangwa na wako wanaoliongoza ila walikuwa wanangoja sababu ya kuanzia kutekeleza uhaini wao... Cha kushangaza kwa vurugu zinazolipuka wakati huo huo ni nadra kuyapata mabomu ya samaki na magobore, mapanga... Hili jambo tukatae tukubali lilipangwa na wako wanaofanya mipango hiyo.. Na walipanga wafanye hiki na hiki...

Binafsi nawapongeza jeshi la polisi kwa jitihada zao walizozitumi kunusuru hali isiendele kuwa mbaya ukweli hata mkiwabeza lakini ukweli uko wazi wamesaidia kwa kiwango kikubwa..Tukumbuke pia si wananchi wote wanapenda kinachoendelea hapa Mtwara. Naomba JWTZ endelee kuangalia hali inavyoendele ili amani iwepo msiingie kazi kutekeleza sheria za kijeshi mana khali itakuwa mbaya zaidi kwa wananchi mana jeshi 99% mafunzo yao ni kuua..

Shime watz turudi nyuma tuache ushabiki wa kisiasa tuliangalie hili jambo kiiundani zaidi na nyuma kuna nini tusiingizwe kichwa kichwa .
Vurugu zilipoanza Libya Gadaf na wanae walikuwa na mawazo haya haya ya kipumbavu..... Ni wahuni wachache...
 
Nimepata shida kuona kuwa asili ya uzi wangu imebadilishwa na kuchanganywa na hoja isyo na mfanano wa kimsingi na hoja yangu. Lakini pamoja na hilo, sina jukumu la kushinda JF bali ninaipa nafasi nikifahamu ipo cyber society ambayo ni muhimu kuifikia na kuifahamisha. Ninapopata muda wa kushiriki nashiriki ipasavyo ila ningependa mods waipe hii thread haki na uhuru wa kujadiliwa.
Kwa hiyo wewe kwa upumbavu ilionao huoni ni kwanini wana Mtwara waichukie ccm ehe? Huku ndio kulewa madaraka. Gadafi hivyo hivyo alikuwa anapuuza kama nyie.....
 
Watanzania tumeze moto tu hata kama moto ...ukweli kwa hali iliyokuwa inaonekana na kilichotokea jana hapa Mtwara ukweli ulio wazi jambo hili lilipangwa na wako wanaoliongoza ila walikuwa wanangoja sababu ya kuanzia kutekeleza uhaini wao... Cha kushangaza kwa vurugu zinazolipuka wakati huo huo ni nadra kuyapata mabomu ya samaki na magobore, mapanga... Hili jambo tukatae tukubali lilipangwa na wako wanaofanya mipango hiyo.. Na walipanga wafanye hiki na hiki...

Binafsi nawapongeza jeshi la polisi kwa jitihada zao walizozitumi kunusuru hali isiendele kuwa mbaya ukweli hata mkiwabeza lakini ukweli uko wazi wamesaidia kwa kiwango kikubwa..Tukumbuke pia si wananchi wote wanapenda kinachoendelea hapa Mtwara. Naomba JWTZ endelee kuangalia hali inavyoendele ili amani iwepo msiingie kazi kutekeleza sheria za kijeshi mana khali itakuwa mbaya zaidi kwa wananchi mana jeshi 99% mafunzo yao ni kuua..

Shime watz turudi nyuma tuache ushabiki wa kisiasa tuliangalie hili jambo kiiundani zaidi na nyuma kuna nini tusiingizwe kichwa kichwa .
n y o o! Wanakuserukamba ww. Kaidanganya familia yako
 
Sisi waafrika sisi tuna tabu kwelisisi...visingizio kibao...sijui uhaini,siasa,uchochozi,sijui NGO's,sijui kuna watu wenye mapembe...mbona tunazunguka point.....point ni wananchi wa mtwara na lindi hawataki gesi iondoke kule bila kujua wao watanufaika vipi na hiyo rasilimali....ukizingatia wameshaona maeneo mengi yaliyo na rasilimali tz wananchi wanaishi kwa umaskini wa kutupwa....its very simple hamna mapembe ya kukata wala mkia...
 
Kwa nini hawa watu wanalenga nyumba za ccm na wanaccm hapa hutakiwi kutumia akil nyingi kupata majibu huu ni mpango wa siasa lakini watu si wajinga na hili litakoma tu.

Hata mimi nashangaa. Ugomvi wao ni kati yao na serikali sasa sijui kwa nini wasivamie sehemu za wana-chadema na wana-CUF ambao ndio wameunda serikali ya tanzania, badala yake wanavamia sehemu za CCM, inashangaza sana.
 
Watanzania tumeze moto tu hata kama moto ...ukweli kwa hali iliyokuwa inaonekana na kilichotokea jana hapa Mtwara ukweli ulio wazi jambo hili lilipangwa na wako wanaoliongoza ila walikuwa wanangoja sababu ya kuanzia kutekeleza uhaini wao... Cha kushangaza kwa vurugu zinazolipuka wakati huo huo ni nadra kuyapata mabomu ya samaki na magobore, mapanga... Hili jambo tukatae tukubali lilipangwa na wako wanaofanya mipango hiyo.. Na walipanga wafanye hiki na hiki...

Binafsi nawapongeza jeshi la polisi kwa jitihada zao walizozitumi kunusuru hali isiendele kuwa mbaya ukweli hata mkiwabeza lakini ukweli uko wazi wamesaidia kwa kiwango kikubwa..Tukumbuke pia si wananchi wote wanapenda kinachoendelea hapa Mtwara. Naomba JWTZ endelee kuangalia hali inavyoendele ili amani iwepo msiingie kazi kutekeleza sheria za kijeshi mana khali itakuwa mbaya zaidi kwa wananchi mana jeshi 99% mafunzo yao ni kuua..

Shime watz turudi nyuma tuache ushabiki wa kisiasa tuliangalie hili jambo kiiundani zaidi na nyuma kuna nini tusiingizwe kichwa kichwa .
unapoteza mda wako kusupport ujinga wakati raia wanaonewa....!Watu wote waliochangia we ndio umejiona una akili ya kuisifia serikali kugawa gesi kwa wachina.Vyovyote watakavoita iwe ni uhaini,ujambaji,ukuwadi,wizi,ufisadi,ukorofi,vurugu,uwendawazimu,ubinafsi,kutokuwa na uzalendo ilmradi tu ni kwa maslahi ya taifa na wananchi wake bado sioni tatizo.

Kwani huo umeme ukizalishwa mtwara hautakuwa na nguvu?tutumie akili zetu kufikiria sio kutumia za viongozi wetu
 
Sisi waafrika sisi tuna tabu kwelisisi...visingizio kibao...sijui uhaini,siasa,uchochozi,sijui NGO's,sijui kuna watu wenye mapembe...mbona tunazunguka point.....point ni wananchi wa mtwara na lindi hawataki gesi iondoke kule bila kujua wao watanufaika vipi na hiyo rasilimali....ukizingatia wameshaona maeneo mengi yaliyo na rasilimali tz wananchi wanaishi kwa umaskini wa kutupwa....its very simple hamna mapembe ya kukata wala mkia...

mbona wameelezwa chungu nzima watanufaikaje na jana hotuba ya muhongo imeeleza wazi ..pinda kaja mtwara kaeleza wazi na wakamwambia yumeelewa ..sasa nini kinaendele na khali hii inaendelea kutokea..tujiulize sote hapa..
 
Mahali popote penye WATAWALA patakuwa shwari tu kama WATAWALIWA watakubali kutawaliwa. Ikitokea wakapinga kutawaliwa basi wataitwa kila aina ya majina kama WAHAINI, WANAHARAKATI, WASIOPENDA AMANI etc.
Hizi mnaziita fujo lakini ni harakati za kupinga kutawaliwa. Wananchi wanahitaji kuongozwa sio kutawaliwa. Kiongozi hawezi kufanya mkataba wa rasilimali za nchi kuwa SIRI kwa wananchi husika. Tuulizane kwa nini mkataba ni wa siri nani yuko nyuma ya hiyo siri na anafaidika vipi na hiyo siri.
 
wewe kibe! Ishu ya kugoma gesi kugomewa na wanamtwara haikuanza jana ni muda wabunge wa upinzani kwa muda mrefu walipigia kelele bungeni kuhusu mgawanyo wa mapato, mwaka jana wananchi wa mtwara waliandamana sana kupinga, hadi baadhi wakaja ikulu ya dar, na kama utakumbuka vizuri kuna bibi alilaani kwamba wakichimba tu bomba litatowa maji na sio gesi........., akatumwa mn'goa kucha mmoja kwa bibi wananchi wakamshtukia nusura auwawe akakimbia gari lake likachomwa moto. Wananchi wa mtwara wakaendelea kuwa na msimamo kwamba gesi haitoki..kwa hiyo yanayofanyika ni ya wanamtwara wenyewe na sio msukumo toka nje.

1. Silaha za wananchi ni mabomu ya uvuvi,mishale na mapanga ambayo yapo kila siku,miaka yote hayajaagizwa kutoka nje ya nchi.

2. Hivi wewe unataka kuniambia mwananchi akidai haki zake eti "katumwa na wachochezi'' kana kwamba yeye hana akili timamu.......unataka kutuambia hata wazee wetu wapigania uhuru waliambiwa na watu wa nje kwamba nchi zetu zilikuwa zinanyonywa na wakoloni.

3. Hata kama makosa yalifanyika nyuma kwa mikoa ya tabora,shy,mza,mara (migodi ya dhahabu na almasi) sio lazima turudie mtwara.

4. Ingekuwa mza,a-town,dar,moshi serikali ya ccm ingekuja na jibu rahisi kwamba cdm inachochea, ingekuwa zenj cuf wangetuhumiwa, sasa mtwara tunadanganya ''mkono wa nje"

5. Wewe kama mtz em pita vijiwe vya watu wa kawaida kariakoo,manzese,tandale,tmk,kndoni,mza,arusha,musoma,bk jaribu kuuliza au kusikiliza maoni ya wananchi ndio uende kuwaambia wakuu wako pale lumumba.

6. Tunataka masahihisho yaanzie mtwara, mji ufanane kama miji maarufu ya uchimbaji wa madini kule africa kusini tusirudie makosa ya mwanza,shy,tbr,mara nk.

7. Unaposema mtwara ni mbali, unamaanisha mbali na wapi? Kwasababu wanaihitaji gesi watalipia gharama za usafiri kuifuata sababu ni adimu.

8. Eti mtwara hamna wataalamu ni uongo, nchi yetu haina wataalamu ndio kwanza wameenda shule.......kama hiyo ni sababu bomba lingejengwa kumwaga gesi urusi ndio kuna wataalam.

9. Wasomi wote wako dar sababu ya ajira na asilimia zaidi ya 90% si wazawa wa dar, ni matumaini yangu kwamba hata bomba lingekuwa mtwara bado wasomi wangelifuata mtwara kupata ajira nzuri, mbona migodi ya dhahabu haijahamishwa tbr,shy nk lakini vijana wasomi kibao wanakimbilia huko kupata ajira nono.

kwahiyo ni vema kukaa chini na kuja na suluhisho la juu juu, kwa sasa serikali ya ccm haiwezi kudanganya watu, sababu watu wamekufa kahama,mererani,tarime kwa manufaa ya viongozi walafi pasipo hata manufaa kwa mwananchi. Pia wananchi wakipinga usiuite uhaini, tatizo lako na ccm hamjui kwamba hata polisi na jwtz ni watanzania na hawafurahishwi dhuluma kwa wananchi...................

nimependa hapo kwenye red..
 
Haini mkubwa nchi hii ni KIKWETE,PINDA,MUHONGO,na Simbakalia hawa wote zingewatosha kichwani huu mgogoro wangeumaliza kwa njia za kiistaarabu na amani kabisa lakini kwa vile ni vichwa maji,wajivuni,na walioweka mbele masilahi yao binafsi,kwa nini toka chokochoko zianze si Pinda wa Kikwete aliyekwenda kuitisha mkutano wa hadhara,muhongo yeye ndio akatoa na matusi kabisa eti wanamtwara maskini,hawana akili,hawajui kitu majibu yake ndio hayo kuchafua tu sifa ya nchi
 
Back
Top Bottom