Watanzania tumeze moto tu hata kama moto ...ukweli kwa hali iliyokuwa inaonekana na kilichotokea jana hapa Mtwara ukweli ulio wazi jambo hili lilipangwa na wako wanaoliongoza ila walikuwa wanangoja sababu ya kuanzia kutekeleza uhaini wao... Cha kushangaza kwa vurugu zinazolipuka wakati huo huo ni nadra kuyapata mabomu ya samaki na magobore, mapanga... Hili jambo tukatae tukubali lilipangwa na wako wanaofanya mipango hiyo.. Na walipanga wafanye hiki na hiki...
Binafsi nawapongeza jeshi la polisi kwa jitihada zao walizozitumi kunusuru hali isiendele kuwa mbaya ukweli hata mkiwabeza lakini ukweli uko wazi wamesaidia kwa kiwango kikubwa..Tukumbuke pia si wananchi wote wanapenda kinachoendelea hapa Mtwara. Naomba JWTZ endelee kuangalia hali inavyoendele ili amani iwepo msiingie kazi kutekeleza sheria za kijeshi mana khali itakuwa mbaya zaidi kwa wananchi mana jeshi 99% mafunzo yao ni kuua..
Shime watz turudi nyuma tuache ushabiki wa kisiasa tuliangalie hili jambo kiiundani zaidi na nyuma kuna nini tusiingizwe kichwa kichwa .
Binafsi nawapongeza jeshi la polisi kwa jitihada zao walizozitumi kunusuru hali isiendele kuwa mbaya ukweli hata mkiwabeza lakini ukweli uko wazi wamesaidia kwa kiwango kikubwa..Tukumbuke pia si wananchi wote wanapenda kinachoendelea hapa Mtwara. Naomba JWTZ endelee kuangalia hali inavyoendele ili amani iwepo msiingie kazi kutekeleza sheria za kijeshi mana khali itakuwa mbaya zaidi kwa wananchi mana jeshi 99% mafunzo yao ni kuua..
Shime watz turudi nyuma tuache ushabiki wa kisiasa tuliangalie hili jambo kiiundani zaidi na nyuma kuna nini tusiingizwe kichwa kichwa .
Leo asubuhi ya saa mbili na dakika 56 (08:56:16am) nimepokea ujumbe wa simu kutoka kwa mmoja wa Viongozi wa juu wa Chama Cha Mapinduzi CCM, ambae kwa cheo ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC). Ujumbe wenyewe ni huu ufuatao:
Ujumbe huu uliniongezea simanzi na majonzi niliyonayo juu ya maafa mbalimbali yaliyojitokeza katika vurugu za Mtwara jana. Simanzi hii ilitokana na kuona hali ya unyonge, woga na wasiwasi mkubwa walionao viongozi wenzangu wa Chama, wasiwasi huo hautokani na woga wa kitoto bali kutokana na hatari wanayoiona mbele yao ya kuwindwa, kushambuliwa na kufanyiwa hujuma na matendo mengine ya kudhuru mwili.
Swali la msingi na lenye kufikirisha ni kwanini wahaini hao wanawalenga wanaCCM..? je inaweza kuwa watu hao wanamlengwa mwingine wa kisiasa ambao unakinzana na CCM hivyo kuifanyia CCM na Viongozi wake mambo haya..? Sitaki kuamini kuwa vurugu hizi zina unasaba wa aina yeyote na Siasa zetu hapa nchini bali najilazimisha kuamini kuwa vurugu hizi ni hujuma na uhaini unaofanywa na wahuni, wahaini ambao hawaitakii mema nchi yetu. Najilazimisha kuamini hivyo kutokana na maana halisi ya Siasa, ama harakati za siasa kuwa hazihafikiani na kinachofanyika mtwara, bali vitendo hivyo vinashabihiana na maana ya hujuma na uhaini kama ifuatavyo.
Maana ya maneno mawili ya mwanzo ya yaani hujuma na uhaini yanafuatana kwa maana hujuma inaweza kutumika kama mkakati wa uhaini. Uhaini ni tendo la kusaliti nchi, serikali au mfadhili; uasi. Hujuma ni shambulio ama vamio: fisidi, kuvuruga ama kuharibu.
Maana ya kipengele cha tatu ambacho kimebeba maneno mawili harakati na siasa, ama siasa ina maana ni mfumo wa mawazo yaongozayo utawala wa serikali ya nchi tafsir nyingine ni utaratibu wa utekelezaji au uendeshaji wa jambo kwa kutumia busara na hekima ili kufikia lengo linalotarajiwa.,na maana ya neno la mwisho yaani harakati ni juhudi zinazoafanywa na watu kwa ajili ya kufikia lengo fulani, bidii, jitihada.
Katika tafsir hizo tatu, kinachoendelea mtwara hivi sasa tunakitoa kabisa katika maana halisi ya harakati za kisiasa, kwa kuwa maana ya harakati za kisiasa ni juhudi za kupanga utaratibu wa mfumo wa mawazo yaongozayo (ama yanayolenga kuongoza) utawala wa serikali ya nchi.
Kwa maana ya Hujuma kuwa ni shambulio, kuvuruga ama kuharibu ni sahihi kwa upande mmoja kuwa hiki ndicho kinachoendelea mtwara lakini kwa tafsir ya uhaini ndiyo hasa inayoelezea kinachoendelea Mtwara.
Ndio ni uhaini uliopangwa na kutekelezwa na watu wenye nia mbaya na nchi hii, wasio wazalendo na waliokosa utaifa. Wanaoendesha mkakati wa nchi kutotawalika, kwa kuibua hujuma mbalimbali dhidi ya serikali na chama kiendeshacho serikali hiyo yaani CCM.
Sio ajenda na hoja ya gesi, bali hoja hii imetumika kimbinu kuendesha mkakati huu wa kihaini ambao unawawinda wanaCCM, ofisi zao, mali zao pamoja na serikali yao. CCM ni chama cha siasa kinafanya siasa ya kuendesha nchi hii, vipo vyama vya upinzani navyo vinalenga kuelekea katika mlengwa huu wa kisiasa, lakini wakati mwingine vinapotoka na kuacha Siasa ama harakati za kisiasa na kujikuta wakifanya hujuma na vitendo vingine vya kihaini. Kwani kama hoja ni gesi vipi vurugu zilenge katika mali, ofisi na uhai wa wanaCCM..?