Uhai wetu na madereva vichaa

tz1

JF-Expert Member
Mar 19, 2011
2,121
534
18.jpg
Hapo ni maeneo ya iyovi Dar -Mby Rd.
Hapo wanaovataki kwa pamoja yakipanda mlima.
Je likitokea lori lina shuka mlima itakuwaje?
 
kwa kweli hapo panaudhi sana................. nadhani nikiwa hakimu mkaniletea kesi ya uzembe kama huu na uliosababisha ajali ama na kifo kabisa na ushahidi wa picha kama huu, asee nakwambia nitakula shingo ya mtu.................. yeah, madereva wazembe wanaua wengine kwa bangi zao kwa nini wao kitanzi kisiwatembelee???.................... aaaagrr................
 
Hapo kuna abiria zaidi ya 270,ajali ikitokea ni jangaa kubwa sana
 
Madereva wa mabasi ni tatizo kubwa sana........ajali karibia zote zinatokana na ukichaa kama huu!
attachment.php
 
Kuna hiyo tanker mbele, likija gari na kukumbana nalo, kuna hatari ya moto mkubwa kufunika magari yote hayo. Kuna anayeweza kulitambua hilo basi la kijani linalofuatia tanker kwa nyuma? Hii picha inafaa kusambazawa pia kwenye magazeti ili wananchi wajionee wenyewe jinsi maisha yao yanavyowekwa hatarini.
 
Sijui ni bangi au ni laana.Maana inaonekana hawana uoga wamaisha ya watu na yao wenyewe
 
Kuna hiyo tanker mbele, likija gari na kukumbana nalo, kuna hatari ya moto mkubwa kufunika magari yote hayo. Kuna anayeweza kulitambua hilo basi la kijani linalofuatia tanker kwa nyuma? Hii picha inafaa kusambazawa pia kwenye magazeti ili wananchi wajionee wenyewe jinsi maisha yao yanavyowekwa hatarini.

Bus hilo lililo nyuma ya lori ni 'green star', hawa huwa walau wanaustaarabu na hawakurupuki barabarani. Nimesafiri nalo mara 3 kwenda/kurudi Mbeya.
 
Bus hilo lililo nyuma ya lori ni 'green star', hawa huwa walau wanaustaarabu na hawakurupuki barabarani. Nimesafiri nalo mara 3 kwenda/kurudi Mbeya.

Mkuu hiyo c "green star" ni NGANGA EXPRESS, angalia vzuri utaona Scania hiyo. Green star wana mabasi Yutong ya kichina, kuhusu ustaarabu ni kweli wanao kiduchu!
 
Hapa palipofika ni abiria kuchukua sheria mikononi mwao na kuanza kucharaza bakora madereva woote ili hizo bangi zao ziwatoke vichwani. Haiwezekani wapuuzi hawa wawe na uhuru wa kuhatarisha maisha na mbaya zaidi kukatisha uhai wa binadamu wasio na hatia..
 
Back
Top Bottom