Uzuri wa UDOM ni majengo tu ila ukikisogelea karibu kichafu cha kutisha, yaani tatizo la maji sijui wanashindwaje kutatua chuo kikubwa kama hiki. Yaani wanaendelea kujenga majengo mengine mengi tu lakini chuo hakina maji safi na salama. wamejitahidi eti kuchimba kisima lakini hayo maji yake ni afadhali wasingechimba maana yana chumvi balaa. Yaani ukiyaoga hakikisha unaogea sabuni ya unga la sivyo hutajisikia kama umeogea sabuni.
Tuje kwenye vyoo sasa ndio balaa lenyewe. Floor nzima yenye vyumba 40 na kila chumba wanalala watu 4 ina vyoo vinne vya kuchuchumaa na vinne vya kukaa. My foot! sijui nani aliwaambia waweke hivyo vya kukaa maana vyote vimeharibika sababu ya wanafunzi kupanda na miguu kwenye vyoo vya kuchuchumaa. Haya hivi vingine vya kuchuchumaa navyo ni majanga tu. Vingi vimeziba sababu ta watu kulundika kinyesi chao kwa pamoja. Wengine wanakunya vyumbani kwenye mifuko halafu wanaitupa mifuko kwenye ma-dust bin. Yaani UDOM ni majanga kwa upande wa maji. Serikali ya chuo haioni hatari hii, kuna siku tutazika watu hapa kwa milipuko ya magonjwa.
Serikali tunaomba mtafute suluhisho la maji kwanza kabla ya kuendelea kujenga ma-college mengine maana tukifika wanafunzi 50,000 kwa mwendo huu tutaathirika kisaikologia.