Uhaba wa mafuta ya taa wasababisha mauaji ya watoto wanne wa familia moja Kongwa Dodoma

Figoo

Member
May 7, 2016
80
49
Watoto hao walifariki dunia kwa kuungua na kuteketea kabisa baada ya kulipukiwa na kibatari ambacho kilijazwa mafuta ya taa yaliyochanganywa na petroli, wakazi wa eneo hilo wamekaririwa wakisema ni kawaida vibatari kulipuka ila havijawahi kuleta madhara.

Hii ni moja ya faida tunayopata makabwela kwa kupandisha ushuru wa mafuta ya taa tangu awamu4 kwa faida ya wachache,imeniuma sana wahusika hasa Ewura walitazame hili la ushuru wa mafuta ya taa.
 
EWURA walifanya mistake kubwa sana kupandisha bei ya Mafuta taa kwa kushindwa kudhibiti uchakachuaji

Mafuta taa ni nishati muhimu kwa vijijini...80% vijijini ni giza....hakuna umeme

Mafuta taa yaliongezewa kodi na serikali kupitia EWURA na Wizara ya Nishati ili kuzuia uchanganyaji

Serikali iangalia mara 2 hii bei ya mafuta taa ili ishuke..
 
Ee Mungu wangu kwann kila kitu kimekuwa ni mateso kwenye nchi hii? Daah!! R.I.P Malaika wa Mungu
 
Daah inatia huruma kuona watu wanateseka na kuteketea kwa sababu ya ulaji wa watu wachache. R.I.P
 
Watoto hao walifariki dunia kwa kuungua na kuteketea kabisa baada ya kulipukiwa na kibatari ambacho kilijazwa mafuta ya taa yaliyochanganywa na petroli, wakazi wa eneo hilo wamekaririwa wakisema ni kawaida vibatari kulipuka ila havijawahi kuleta madhara.Hii ni moja ya faida tunayopata makabwela kwa kupandisha ushuru wa mafuta ya taa tangu awamu4 kwa faida ya wachache,imeniuma sana wahusika hasa Ewura walitazame hili la ushuru wa mafuta ya taa.
Hapa kazi tuuuuuuuuu
 
Daah inatia huruma kuona watu wanateseka na kuteketea kwa sababu ya ulaji wa watu wachache. R.I.P
Sasa serikali imeshindwa, kila sehemu ni vilio,hatujamaliza kilio cha vat kwenye huduma za fweeedha tunashuhudia kupoteza vijana wetu!
 
nanukuu "nikawaida kwa vibatari kulipuka ila huwa havileti madhara" hahaha sasa hicho kimeletaje madhara?
 
Binadamu anaweza kufa kwa kupaliwa na mate,tumlaumu dada yao aliowafungia na kwenda kujitia tembo!
 
Serikali haiwezi weka sheria kila mwenye petrol station awake pump ya mafuta ya taa.
 
Watoto hao walifariki dunia kwa kuungua na kuteketea kabisa baada ya kulipukiwa na kibatari ambacho kilijazwa mafuta ya taa yaliyochanganywa na petroli, wakazi wa eneo hilo wamekaririwa wakisema ni kawaida vibatari kulipuka ila havijawahi kuleta madhara.

Hii ni moja ya faida tunayopata makabwela kwa kupandisha ushuru wa mafuta ya taa tangu awamu4 kwa faida ya wachache,imeniuma sana wahusika hasa Ewura walitazame hili la ushuru wa mafuta ya taa.
EWURA ni kibaraka tu. Wanatekeleza maagizo toka juu. Ingekuwa nchi za wenzetu angekuwepo wa kuwajibishwa kwenye vifo vya watoto hawa. Lakini hapa kwetu hutasikia TBS wala EWURA au hata Isilop wamkabe aliyeuza mafuta hayo.
 
Hawa watoto walilala na kibatari kikaachwa kikiwaka baada ya mama yao mdogo pamoja na dada yao kwenda disco idd pili. Wazazi walikuwa mashambani kwny mavuno
33eec63bbf2657a84df860fa53aeeeb9.jpg
571713f1eb5e3a12d0b43584be41a30a.jpg
9ffa41d1d18fcda8470829dbba027a3e.jpg
 
RIP wadogo zetu mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi...Stay blessed muendako.
 
Back
Top Bottom