Ugumu wa maisha usababisha vijana tufanye jinai

Latrice

JF-Expert Member
Jan 30, 2020
2,393
2,359
Habarini ny'ote. Nawaletea salam changamfu kabisa kutoka Monroe.

Ukiwa huna hela unaweza kufanya chochote, sehemu yoyote na kwa wakati wowote ili tu uipate.

Kuna kipindi nilikosa hata mia ya kununulia bange na kuomba siwezi, kwa kuwa tuliwahi kuishi Geita nikapawaza GGM huu ni mgodi nikaenda kwa rafiki zangu kuishi, nikawa nadamka asubuhi naenda kusoma mazingira ya mgodi napitia njia ya Katoma hadi lilipo dampo, lengo nifanye uhalifu wa aina yake kisha nitokomee.

Sikutaka kumshirikisha mtu, ule mgodi wanachapa sana watu wanaoenda kufanya uhalifu na wengine walikuwa wanapigwa risasi miguuni hizi ndizo habari nilizokuwa nazisikia na baadhi niliwaona waliolambwa fimbo wakiwa wanapelekwa Mahakama ya mwanzo.

Baada ya kufanya research zangu nikaona ngoma ni ngumu wakinishika wataniua inabidi nipate wasaidizi wenye akili kama zangu nikashirikisha wanne na wote wa mulemule kotaz ila wawili walikuwa wakubwa kwetu na mmoja ndiye aliyeharibu calculation za tukio.

Ilikuwa jumatano wale wakubwa walikuwa tayari wamemaliza kidato cha nne na wamepata dili la kwenda Jeshini.
Mmoja sasa akatuharakisha habari za kusoma walinzi kila siku tuachane nazo yeye ameshaenda sana na bange zetu kichwani tukaamsha saa kumi ya siku ya Alhamis na Carina ya mzee wake ambayo tuliiacha kwenye Machimbo ya Katoma (kwa miguu kutoka yalipo machimbo ya Katoma ni kama saa zima kufika dampo kuna kupanda vilima na kushuka).

Hatimaye tukafika dampo tukaona shuhuli za kawaida tu zinaendelea kwa mbali tukasogea hadi dampo kwenye begi tuna uniform za shule kama defensive mechanism tukasogea hadi ndani tukakuta sehemu kuna mawe mengi yamerundikwa (wenyeji wanaita Magwangala) mkubwa wetu akasema "Yenyewe" tukaanza kubeba (Ulinzi haukuwa mkali miaka hiyo kama ulivyo sasa) tukafikisha viroba nane tukaonwa na G4S wakaanza kutufukuza na Cruiser yao huku wanapiga filimbi.

Mdogo mwenzangu akaishiwa pumzi maana tulikuwa tunakimbia juu ya michanga wakamkamata yeye pamoja na vibaka wengine maana hatukuwa sisi tu na mchana akaletwa amechapika vya kutosha kuliko wengine.
Kosa kubwa alilofanya ni kusema yeye ni mtoto wa Askari!

Jioni nikapanda zangu Coaster kwetu ila habari zilifika tu kwa mzee.

Kwa hiyo wazazi wa sasa watoto wenu wakiwaomba hela muwape na maswali ya "Unataka hela ya nini?" tuache, Yanawatia hofu na kuamua kuzisaka kwa akili zao ndio hapo wanaiba, nyakati zimebadilika watakuja kufanya tulivyofanya sisi miaka hiyo wakione cha moto.
 
Nobody give A damn about it!!.....joined Jan 30.2020 and you post 20 new messages in every 20 seconds........
Heheheiya!
FB_IMG_15885394912627069.jpg
 
Kwa kwa kwa kwa yaani wewe kima ndo unakuja kutishia watu tuliozaliwa na silver spoon maisha bwahahahahaha
 
Acha ufala tahira wewe, NARUDIA ACHA UFALA.

Kamwite mamako hivyo kubi wewe
 
Back
Top Bottom