ESPRESSO COFFEE
JF-Expert Member
- Sep 6, 2014
- 6,146
- 7,683
Wakuu Habari
Leo nimeona nije na ushauri kidogo kuhusu Watanzania wanaotafuta scholarship za kwenda kusoma nje ya nchi au ndani ya nchi.
Nianze kwa kusema tu kupata scholarship ni bahati kama Ilivyo bahati ya kubet. Sio kwamba unajua hapana ila ni Mungu anakuwa amekupangia.
Hivyo hivyo kwenye kupata scholarship. Kwa sasa Tanzania kumekuwa na wimbi kubwa la vijana wanaotafuta scholarship wakihisi ni kitu rahisi rahisi tuu. Wengine wamejikuta wanatumia pesa nyingi sana kutafuta scholarship bila mafanikio, Wengine wamediriki hadi kuingia mkenge kwa kufanya tendo la ndoa na wale wanaojiita msaada wa kutafuta scholarship mwisho wa siku wanatoswa.
Watanzania tuwe wa kweli usimwambie mtu kuwa kupata scholarship ni kitu rahisi rahisi tu hapana.
Wakati unamshauri mtu kuomba scholarship mwambie na ugumu wa kupata Scholarship. Wakati upo Form 4 watakwambia Scholarship za Diploma/Degree nje ya Tanzania ni easy tu kupata,
Unamaliza Form 4 unahangaika unatumia pesa nyingi mwisho wa siku unakosa, unaenda Form 6, Degree/Diploma, baadae Masters mwisho wa siku unajikuta umetumia zaidi ya 10M katika kutafuta kwako Scholarship bila mafanikio.
Kuwa Makini na hizi Scholarship za kwenye mitandao. Saa hizi utaambiwa umepata scholarship 50%, 50% unajitegemea kumbe ni uongo unakuta hiyo 50% ni karibia Million 30/20 wizi umekuwa mkubwa sana.
Na hasa wajinga ndio waliwao! Kuwa makini na Scholarship unazopata nusu nusu, kuwa makini wakati wa kuomba scholarship.
Scholarship kuomba huhitaji hata kulipia senti ili upate Scholarship kuwa makini. Ni bora ukaamini zile zinazotangazwa na Serikali ila ukipata ni vizuri ukaauliza kwa waliopita ukajua maana Serikali nayo imekuwa ikiwaingiza mkeng watoto wa kitanzania unaambiwa umepata Scholarship ukienda huko mambo yanakuwa magumu sana.
Kupata kwenyewee ni kwa kindugu. Hakuna kitu kinacho nikera kama matangazo ya GLOBAL EDUCATION LINK na mengine ya aina hiyo, yamejaaa wizi sana kwa Watanzania na huwa ninashangaa kuona Serikali bado inawaachia waendelee kuwepo.
Kikubwa tuwe makini na hizi Scholarship uchwara. Dunia imebadilika sana utoaji wa Scholarship miaka hii sio sawa na zamani. Wazungu wamesthuka na wamebadilika sana.
Maisha sio kama zamani kwa sababu uongo umekuwa mwingi. Zamani asilimia kubwa ya vituo vya watoto yatima wazungu walikuwa wanafadhi ila kwa sasa wamebadilika kwa sababu ya uongo hii ipo hadi kwenye Scholarship za shule.
Hasa huko China na nchi zingine kuweni makini msije mkaingia mkenge mkajuta baadae. Amini usiamini elimu ya Tanzania sio mbaya kama unavyofikiria wala usidanganywe kuwa kusoma nje ndio kupata ajira. Tukomae hapa hapa bongo tutatoboa.
Yapo mengi sana kuhusu Scholarship mengine tutapata kupitia comment za watu.
Tupendane kwa kuambiana ukweli. Maisha sio rahisi kama tunavyofikiria.