Shetani Lucifer ndiye muasisi wa dhambi na suala la kutokuomba msamaha, na watu wengi wana hiyo spirit (roho) ya Lucifer a.k.a sheteni. Maana ktk maandiko, hakuna hata sehemu inayooneshwa baada ya kukosea shetani aliomba msamaha, hivyo hivyo hata Adam hatuoni sehemu aliyoomba msamaha baada ya kukosea kwenye bustani ya Eden, vile vile hata kwa mkewe Eva (a.k.a Hawa), hakuomba msamaha, japo kuwa Adam alipewa masharti ya kwenye bustani na yeye kumueleza hayo masharti mkewe ila baada ya anguko hawakuomba msamaha, ila Mungu tu aliawaonea huruma maana kuwaangamiza ingekuwa ushindi kwa shetani.
Kwa hiyo ukiona mtu anakuwa mgumu wa kuomba msamaha ujue Lucifer (shetani) spirit (roho) imemkalia kooni sana. Na ndiyo maana hizo roho kwa sehemu kubwa wanazo wanawake, wanawake huwa hawasamehi kwa sehemu kubwa ila huwa wanamezea, ila wanaume ni tofauti, wao husamehe na ni wawazi. Na ndiyo maana kwenye makanisa ya wokovu, ni nadra sana kukuta wanaume wanaanguka kwa mapepo, ni wanawake tuuuuuuuuu!