Kwa staili hii CCM haipaswi kuaminiwa tena, kwani ni ndumilakuwili. Wanahitaji jimbo la Igunga zaidi kuliko kusimamia misingi ambayo wametwambia ni mkakati wao kichama ili kukirejeshea mvuto. Kama wameimba wimbo wa kujivua gamba na kumtaja Rostam kuwa ni mmoja wa makada ambao wamekipotezea chama mvuto kwa vitendo vyao vya ufisadi halafu leo tunaona vichwa vya habari vya magezeti vikituambia RA atakuwapo siku ya uzinduzi mimi naangalia tu wenye chama chao watuambie kwani tunao humo kwenye jamvi. <br />
<br />
<br />
Kwamba jimbo la Igunga limebaki wazi kwa sababu ya dhana ya kujivua gamba sasa usafi wa Mkapa uko wapi? Au katika hili yeye ni nafuu kulinganisha na makada waliobaki? Chonde sana sana tumieni nafasi hii katika jimbo la Igunga kufafanua msimamo wenu hata kama gharama yake ni kupoteza jimbo lakini watanzania watakuwa wamewaelewa. Better to loose but maintain your political integrity than win and loose your political integrity. Kindly dont contradict yourself as it will haunt you in the long run indefinitely.