Ugumba wawatesa Watanzania wengi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ugumba wawatesa Watanzania wengi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Sep 18, 2012.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Sep 18, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,878
  Likes Received: 83,359
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]Ugumba wawatesa Watanzania wengi
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Tuesday, 18 September 2012 12:54
  Mwananchi

  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]WASAKA WATOTO KENYA KWA SH5.4 MIL, HADI SASA WANAWAKE 60 WAMEHUDUMIWA DAKTARI WA MUHUMBILI AKIRI TATIZO NI KUBWA

  Florence Majani na Herieth Makwetta

  TATIZO la uzazi linaonekana kushika kasi nchini baada ya idadi kubwa ya wanandoa kukimbilia Kenya kupata huduma ya upandikizaji wa watoto kwa gharama ya zaidi ya Sh5 milioni.Kati ya wageni 10 wanaokwenda katika vituo vya upandikizaji vya Aga Khan na Nairobi IVF Centre nchini humo, wanne wanatoka Tanzania.
  Licha ya kuwapo kwa huduma hiyo nchini, imeelezwa kwamba Watanzania wengi wanakimbilia huko kutokana na unafuu wa gharama na ubora wa huduma.
  Huduma hiyo ni ya mwanamke kupandikizwa mbegu ya kiume ili kuweza kushika mimba na baadaye kupata mtoto.

  Mmiliki wa Kituo cha Upandikizaji cha Nairobi (Nairobi IVF Centre), Dk Joshua Noreh alisema kwa mwaka kliniki yake hupokea zaidi ya wagonjwa 270 kutoka mataifa mbalimbali likiwamo Bara la Ulaya.

  Alisema wagonjwa kutoka Tanzania walianza kumiminika katika kliniki hiyo kuanzia mwaka 2006 na ukiondoa gharama za matibabu ambazo ni Sh5.4 milioni zipo gharama za ushauri na uchunguzi wa tatizo.

  "Gharama ya ushauri peke yake ni Sh42,000 za Tanzania. Baada ya ushauri, mgonjwa hutozwa Sh420,000 kwa ajili ya uchunguzi wa tatizo. Gharama za matibabu hutegemea ukubwa wa tatizo. Tiba yenyewe ni upandikizaji wa mbegu, hadi hatua za kuirutubisha," alisema.
  Dk Noreh alisema ukijumlisha gharama za usafiri, malazi, mlo na tiba kwa wagonjwa wanaotoka Tanzania, wengi wao hutumia kati ya Sh8milioni hadi Sh10 milioni, kwa ajili ya kupata mimba.

  Imeelezwa kuwa raia wa Uganda hukimbilia Kenya kukwepa gharama kubwa kwani nchini humo hugharimu kiasi cha Sh500,000 ya Uganda (sawa na Sh9.5 milioni) wakati huduma hiyo hupatikana Kenya kwa Sh300,000 (sawa na Sh5.4 milioni) kwa mzunguko.

  "Tuna vituo zaidi ya vitano vya IVF hapa Kenya, ndiyo maana Kenya imekuwa kimbilio la wanandoa au wapenzi kupata matibabu ya aina mbalimbali za ugumba. Lakini kikubwa ni huduma bora na gharama nafuu ndiyo sababu ya ongezeko hili la wageni kutoka nje."

  Alisema baadhi ya nchi hazina huduma ya IVF hivyo wanandoa huenda Kenya na wengine wanayo huduma hiyo katika nchi zao ila wanachagua Kenya kwa sababu ya urahisi wa tiba hiyo na kuwapo kwa mbegu za wanaume wa Kiafrika zilizohifadhiwa.
  Nchi nyingine ambazo wanandoa wake wanaongoza kwenda Kenya kwa ajili ya kupata huduma ya upandikizaji wa watoto ni Uganda, Sudan ya Kusini, Marekani na Ethiopia.

  Mtaalamu kutoka Hospitali ya Chuo Kikuu cha Aga Khan Nairobi, Dk Prafull Patel alisema idadi ya wanaohitaji huduma hiyo imekuwa ikiongezeka kwa kasi kutoka mataifa ya Afrika, Uingereza na Marekani.
  Alisema zaidi ya robo tatu ya wanaopata huduma hiyo ni watu kutoka nje ya Kenya, lakini hasa ni kutokana na unafuu wa gharama za huduma hiyo ikilinganishwa na nchi nyingine.

  Nchini Uganda, IVF inagharimu Sh9,000,000 za Tanzania wakati Uingereza inagharimu zaidi ya Sh10,800,000 za Tanzania na kwa wenza zinafikia Sh21,600,000 kwa kila mzunguko huku Marekani ikigharimu Sh10,620,000 na Sh19,800,000 kwa mzunguko.

  Hii inamaanisha kwamba gharama nchini Kenya ni nusu ya gharama inayolipiwa Marekani, Ulaya na nchi nyingine za Afrika. Hiyo inaelezwa kuwa chanzo cha ongezeko la idadi ya wageni kwenda Kenya kusaka tiba ya ugumba.

  Upandikizaji unavyokuwa
  Upandikizaji huo hufanyika kwa kuchukua mbegu za mwanamume na kuzipandikiza katika mirija ya uzazi ya mwanamke.

  Mwanamke mwenye matatizo huweza kwenda peke yake kupandikizwa kwa kununua mbegu zilizohifadhiwa katika kliniki au wanandoa kwenda pamoja na mwanamume kutoa mbegu ambazo zitapandikizwa kwa mwanamke.
  "Tiba huchukua mwezi mmoja, huanzia siku ya pili baada ya mwanamke kumaliza hedhi na siku ya yai kurutubishwa lakini mwanamume hutumia siku moja tu pale mbegu zake zinapohitajika."

  Dk Noreh alisema sababu ya kuanza tiba siku ya pili baada ya mwanamke kumaliza mzunguko wake wa mwezi ni kulenga tarehe za uchavushaji, kwani kipindi hicho mbegu za mwanamume hupandikizwa na kusababisha mimba kutungwa.

  "Mbegu zilizorutubishwa huachwa kwa siku mbili mpaka tano ndani ya chombo maalumu ili kukuza kiinitete (embryo) kabla ya kuhamishwa katika nyumba ya uzazi ya mwanamke kwa ajili ya kutungisha mimba ya kawaida."
  Alisema tatizo la ugumba linaongezeka duniani na njia hiyo inatumika kuwasaidia wanawake wasiokuwa na mayai ambao mirija yao ya kuyasafirishia imeziba na wanaume ambao manii yao ni dhaifu na hushindwa kuogelea hadi kufikia yai la mwanamke...

  "Tatizo la ugumba kwa sasa ni wastani wa asilimia 10, hiyo ina maana kwamba kati ya wanandoa 10 mmojawapo hana uwezo wa kushika mimba. Kiwango hiki kwa sasa kinakua kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo wanawake wa sasa kuchelewa kuolewa wakitoa kipaumbele kumalizia masomo," alisema Dk Noreh.

  Wataalamu wa Tanzania
  Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba cha Muhimbili, Dk Henry Mwakyoma alisema ongezeko la Watanzania kufuata huduma hiyo Kenya, limesababishwa na kukua kwa tatizo la uzazi nchini.

  Dk Mwakyoma alisema huduma hiyo hutolewa kama tatizo la uzazi analo mwanamke. Alisema kama mwanamume ndiye mwenye tatizo, huduma hiyo haiwezi kutolewa.

  "Kama mwanamke ana tatizo la uzazi, kwa mfano mirija imeziba, kizazi kimelegea, anaweza kufanyiwa upandikizaji na kupata mtoto, lakini kama mbegu za mwanamume ni dhaifu, hakuna kitu kinafanyika," alisema.
  Dk Mwakyoma ambaye aliwahi kufanya utafiti na kubaini kuwa asilimia 80 ya wanaume nchini wana tatizo la ugumba wa kudumu au wa muda, alisema mfumo wa maisha wa sasa ndicho chanzo cha ongezeko la tatizo la uzazi.
  Daktari kutoka kituo kimoja cha upandikizaji nchini ambaye hakutaka kutajwa jina, alisema huduma hiyo inapatikana katika kituo hicho kwa bei nafuu kuliko huko Kenya.

  "Gharama za hapa zinategemea ukubwa wa tatizo la mhusika, mchakato wake na afya yake. Wapo wengine hawahitaji kupandikizwa, wengine wanahitaji tu dawa, pia wapo wengine wanaweza kufanyiwa upandikizaji kwa zaidi ya mara moja," alisema.

  Alisema tangu kufunguliwa kwa kituo hicho Februari mwaka huu, idadi ya wanandoa wanaokwenda kupata huduma hiyo imekuwa ikiongezeka. Hata hivyo, hakutaka kuweka wazi takwimu rasmi kwa mwezi au tangu kufunguliwa kwake.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   

  Attached Files:

 2. analysti

  analysti JF-Expert Member

  #2
  Sep 18, 2012
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 704
  Likes Received: 354
  Trophy Points: 80
  [[TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  Mwanamke mwenye matatizo huweza kwenda peke yake kupandikizwa kwa kununua mbegu zilizohifadhiwa katika kliniki au wanandoa kwenda pamoja na mwanamume kutoa mbegu ambazo zitapandikizwa kwa mwanamke.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]  Is this really ethical!!?. Mtu unapandikizwa mbegu za mtu usiyemjua, maana yake ni kwamba huyo mtoto hatakuja kumjua baba yake hata siku moja!!. Are there women doing this in this world, wanawake hawa watakuwa wanatengeneza binadamu wa aina gani?.

  My take: Mwanamke anaeweza kuenda kupandikizwa mbegu za mwanaume asiyemfahamu, ni mwanamke asiyetambua ni nini thamani ya ubinadamu, na kamwe hafikirii ni kitu gani anakitengeneza.
   
 3. Mwanahisa

  Mwanahisa JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2012
  Joined: Jun 29, 2012
  Messages: 1,397
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ni wakati sasa watu wawe makini na utaratibu wa milo na lishe wanazotumia, haya mafuta ya transformer watu wanakula kwenye mikaango ukichanganya na methanol (CH4O) kwenye pombe hakuna mbegu ya mwanaume inaweza pona hapo, kawaida shahawa zinatakiwa kua na rangi ya unjano flani, ukishaona tu weupe wa maji, maziwa flani ujue hati hati kuogelea kulifikia yai.
   
 4. awp

  awp JF-Expert Member

  #4
  Sep 18, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,714
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  teh teh! mi nilijua zile za njano kama jamaa amekaa muda mrefu bila kupata, kumbe inatakiwa kila mnapokutana ziwe za njano. mmh! somo zuri lakini kuziangalia akimaliza huwa nahisi uchafu kwi kwi
   
 5. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #5
  Sep 18, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Wana JF,

  Tatizo kubwaa ni wakina dada wetu hapa nchini kuto penda kufanya vipimo kwa madoctor husika Gynecology. Ni kweli kabisa tatizo kubwa twatakiwa kuwashauli wake zetu dada zetu na hata mama zetu wengine ambao hawajapata watoto Huko Arusha kuna Dr. anaitwa Mkoyogo ni kwa ajili ya akina mama hapo arusha kwasaidia wakina mama wengi sana kwa ukiritimba wa seriklai alikuwa anaanda clinic yake watu wa Halmashauri wakamsumbua kuhusu kiwanja ati atoe hongo mzee wawatu kakaaa sana UK hajui hongo akagoma mpaka leo anatumia ofice ya Dr Urasa.na kazi anapiga Nchi hiii hata kama kuna mtum anakuja kutusaidia tutataka hongo yaani ni taaabu kweli.

  Kwa wakina mama huko dar huyo Dr. huwa anakuja Premier Care mbele ya best beat Moroco. wakina mama wenye matatizo wekeni appointment mtasaidiwa mtaona ni gharama lakini utamu wa kupata mtoto jamani.

  My Take;
  Msije mka puuzia hili jambo wakina Dada wakina mama na wale wenye ndoa. me ni mfano na nina mtoto na ninpanga mwakani mungu akijalia kupata mtoto wa pili
   
Loading...