Ugumba kwa wanaume hasa ni kitu gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ugumba kwa wanaume hasa ni kitu gani?

Discussion in 'JF Doctor' started by Mghoshingwa, Jun 9, 2012.

 1. Mghoshingwa

  Mghoshingwa JF-Expert Member

  #1
  Jun 9, 2012
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 305
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  Ndugu daktari na Wadau wengine wenye ufahamu wa jambo hili, ama mambo mengine ya afya ya uzazi naomba kufahamu, Ugumba kwa wanaume hasa ni kitu gani kwa kuzingatia yafuatayo:
  1. utajuaje kuwa ni mgumba? (dalili if any) UKIACHANA NA KWENDA HOSPITALI
  2. kuna aina ngapi za ugumba kwa wanaume?
  3. tiba zake ni zipi
  Je kwanini inatokea wakati mwingine mwanaume na mwanamke wanakuwa wako fit(Hawana kasoro katika mifumo yao ya uzazi) lakini huchukua muda kupata mtoto?

  Tafadhali naomba kufahamu ili NIONGEZE MAARIFA KENYE SUALA HILI.
   
 2. Kennedy

  Kennedy JF-Expert Member

  #2
  Jun 9, 2012
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 11,312
  Likes Received: 2,973
  Trophy Points: 280
  Mkuu japo si dr nadhani km una ugumba utajijua tu. Kwakuwa unahitaji madr hao ndiyo wana majibu ya kina vzr.
   
 3. Kilahunja

  Kilahunja JF-Expert Member

  #3
  Jun 9, 2012
  Joined: Dec 19, 2011
  Messages: 1,497
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  swali zuri, ugumba ni hali ya mwanaume kushndwa kutoa sperms zenye uwezo wa kumpa mwanamama mimba.

  Kuna ugumba wa kuzaliwa nao na ule unaosababishwa na magonjwa mbalimbal mwilin hususan zinaa, wale wanaopenda tigo/anul sex pia inaweza ziba mirija ya uzaz ivo kukufanya mgumba.

  Ugumba wa kuzaliwa nao huwez kupona cz matakwa ya muumba

  ugumba wa magonjwa nao huwez pona unles kama uliwai matibabu mapema kabla ya kuitwa mgumba.

  Haijawai kutokea mgumba kuzaa na ikitokea then hukuwa mgumba bali mabadiliko 2 ya ukuaji ktk mwili.


  #Damu inaweza sababisha watu kuchelewa kupata watoto. Na mara nying mimba ni matokeo ya pande mbil then upande mmoja hua unakua umezdwa tatizo thats why mimba inachelewa
  MAELEZO HAYO JUU SI YA KITAALAMU NIMEJARIBU KUKUPA JAPO MWANGA SUBIRI KINA MZIZI MKAVU KWA MAELEZO YALIYOKWENDA SKONGA, WAVEJA SANA!
   
 4. Kilahunja

  Kilahunja JF-Expert Member

  #4
  Jun 9, 2012
  Joined: Dec 19, 2011
  Messages: 1,497
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  kenned huwez jua kama we ni mgumba mpaka pale utapokua uko tayar kutafuta mtoto..ugumba hauna dalili.
   
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  Jan 27, 2014
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [h=2]Zifahamu sababu za ugumbwa kwa wanaume[/h]
  [​IMG]

  KWA UFUPI


  • Taasisi ya Taifa ya Afya ya nchini Marekani (NIH) inaeleza kwamba sababu za jumla za ugumba ni umri na asilimia nne ya wanaume wenye umri wa miaka 50 na kuendelea wanaweza kuwa na tatizo hilo wakati nusu ya wanaume wenye umri wa miaka 75 wanakumbwa na ugumba.


  Ukosefu wa nguvu za kiume nchini twaweza kusema ni janga. Hii ni kutokana na tafiti zilizowahi kufanywa na pia kuzagaa kwa vibao vya matangazo kuhusu dawa au tiba ya tatizo hilo.

  Tatizo hili halipo kwa wazee kama ilivyodhaniwa zamani, bali hata kwa vijana, wake kwa waume wamekuwa wakiguswa na tatizo hilo.

  Sababu nyingi zimewahi kuanishwa kuchochea ugumba kwa wanaume ikiwamo maradhi, kutazama luninga kwa muda mrefu na kutofanya mazoezi.

  Hivi karibuni wataalamu katika Jarida la Jinsia na Tiba la nchini Uingereza, lililochapishwa Januari lilieleza sababu kuu duniani zinazochochea ugumba kwa wanaume iwe wa muda mrefu au wa kudumu.

  Taasisi ya Taifa ya Afya ya nchini Marekani (NIH) inaeleza kwamba sababu za jumla za ugumba ni umri na asilimia nne ya wanaume wenye umri wa miaka 50 na kuendelea wanaweza kuwa na tatizo hilo wakati nusu ya wanaume wenye umri wa miaka 75 wanakumbwa na ugumba.

  Daktari wa Upasuaji na Nguvu za Kiume katika Chuo Kikuu cha Tiba cha Maryland, Dk Andrew Kramer anasema karibu nusu ya wanawake na wanaume wote duniani wanakosa nguvu za kiume aidha moja kwa moja au katika nyakati fulani za maisha yao.

  Madereva

  Dk Kava anasema wakati wa zama za chuma ilibainika kwamba wanaume wanaoendesha baiskeli kwa muda mrefu, waendesha farasi na madereva wa magari kwa muda mrefu wamo hatarini kukosa nguvu za kiume.

  Jarida la tiba lilifanya utafiti na kubaini kuwa asilimia nne ya wanaume wanaoendesha baiskeli kwa saa tatu au zaidi kwa wiki wanapata matatizo ya nguvu za kiume.

  Anasema unapokaa kwenye gari, farasi au baiskeli kwa muda mmrefu unaweka nguvu katika neva na mishipa midogo inayobeba damu kwenda katika uume.

  Anafafanua kwamba uendeshaji wa vyombo hivyo kwa muda mrefu unaharibu mishipa midogo na damu haiendi inavyotakiwa katika uume.

  Maradhi ya fizi Pengine unaweza kujiuliza fizi na nguvu za kiume vina uhusiano gani? Wataalamu wa Afya wanasema, kuwa na matatizo sugu ya fizi au fizi zilizoathirika kunaweza kuongeza hatari ya mtu kukosa nguvu za kiume.
  Watafiti wanasema maradhi ya fizi ni dalili za afya dhaifu na inahusishwa na ongezeko la maradhi ya moyo na upungufu wa nguvu a kiume.

  "Maradhi ya fizi yanaweza kusababisha matatizo katika kusukuma damu, hivyo matatizo hayo yakizidi, yanaweza kusababisha damu ishindwe kufika katika uume," anasema Bruce Kava, Mwenyekiti wa Tiba ya Mfumo wa Mkojo katika Chuo Kikuu cha Tiba cha Miami Miller.

  Kisukari ni sababu nyingine na Taasisi ya Taifa ya Afya ya nchini Marekani inasema wanaume wanaougua maradhi ya kisukari wana hatari mara tatu zaidi kukosa nguvu za kiume kuliko wanaume wasio na maradhi hayo.

  Dk Kramer anasema sukari isipodhibitiwa katika damu, inaharibu neva na misuli midogo inayodhibiti kusimama kwa uume.

  Pia asilimia 61 ya watu wenye msongo wa mawazo hawawezi kuwa na nguvu za kiume.

  Taarifa kutoka Kliniki ya Cleveland inaeleza kwamba msongo wa mawazo unasababisha mambo makubwa zaidi katika mwili na unaweza kuathiri kwa kiasi kikubwa nguvu za kiume.

  Msongo wa mawazo unasababisha Kemikali za seli za ubongo zinazowasiliana katika kusisimua mtiririko wa damu hadi katika uume kushindwa kufanya kazi.

  Pia Dk Malebo anasema wanaume hukosa nguvu za kiume kutokana na msongo wa mawazo ambao unatokana na migogoro ya kifamilia, ufukara au imani za kishirikina.

  Dk Kramer anasema dawa za saratani na zile za kuondoa vipara zinazotumiwa zaidi na wanaume zinaweza kusababisha madhara ya nguvu za kiume.

  Mkuu wa Kitengo cha Utafiti wa Tiba Asilia katika taasisi ya utafiti wa tiba nchini (NIMR), Dk Hamis Malebo anasema sababu kuu za ugumba kwa Tanzania ni mfumo wa maisha.

  Anafafanua kwamba aina za vyakula, mtindo wa maisha, msongo wa mawazo na utofauti katika vichocheo ni baadhi tu ya sababu za ukosefu wa nguvu za kiume."Baadhi ya vyakula vina kemikali ambazo zinapoingia katika mwili zinaharibu usukumwaji wa damu katika uume" anasema dk malebo ambaye aliwahi kufanya utafiti kuhusu ugumba.

  Samaki na maziwa ni sababu


  Kwa mfano, watu wengi hununua maziwa ya ng'ombe ambayo yamechomwa sindano siku mbili au moja nyuma bila wao kufahamu

  "Au samaki wanaovuliwa kwa kemikali na mabomu ni sababu zinazochangia kwa kiasi kikubwa ukosefu wa nguvu za kiume," anasema.

  Anasema kemikali hizo zinaathiri uzalishaji wa vichocheo na usukumwaji wa damu kutoka katika moyo hadi katika uume.

  Anashauri kuwa ili kuepukana na tatizo la nguvu za kiume hasa kwa wale wenye msongo wa mawazo sulushisho ni kubadili mfumo wa maisha.

  "Kuhusu mvurugiko wa homoni, udhibiti wa serikali unahitajika. Maziwa ya ng'ombe, yanayokamuliwa wakati ng'ombe amechomwa sindano pamoja kemikali za kuvulia samaki zidhibitiwe," anasema.

  Anasema uwiano mbovu wa vichocheo unaweza kutibika hospitali kwa dawa zinazorekebisha mfumo huo na pia zipo dawa za asili.

  Mmea wa Alikisusi (licorice) kwa kisayansi Glycyrrhiza Giabra una uwezo wa kutengeneza uwiano wa vichocheo kwa wanaume wenye matatizo ya nguvu za kiume.Zifahamu sababu za ugumbwa kwa wanaume - mwanzo - mwananchi.co.tz
   
 6. Kennedy

  Kennedy JF-Expert Member

  #6
  Jan 27, 2014
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 11,312
  Likes Received: 2,973
  Trophy Points: 280
  Mkuu nilikuwa na maana hiyo kwamba atakapofikia hatua za kutafuta mtoto na kuona mambo yake hayawi mazuri ndiyo huenda akaenda Hosp kujua hali yake .:A S thumbs_up:
   
Loading...