Ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers Disease): Kinga, tiba na ushauri

Kaka tafadhari naomba unisaidie ninateseka sana akili yangu haina uwezo wa kufikili sana
Kuna mtu anatibu aliwahi kunitibu mimi nashuhudia na baadhi ya ndugu zangu. Dawa ni inakuwa katika dozi mbili na bei yake ni laki 2 mpaka kupona. Utalipa kwa awamu mbili kila anapokutumia dawa au ukofuata. Au pengine inaweza ukalipia yote akakupatia kwa wakati mmoja lakini huwa anapendelea ulipie nusu uone matokeo na kisha uchukue awamu yabpili . Dawa unaweza kutumia kwa miezi miwili.

Yupo Ifakara vijijini unaweza kufuata mwenyewe au akakutumia. Uchaguzi ni wako.
 
Habari za saa hizi wakuu,

Niende kwenye mada husika. Nina mwaka wa tano naumwa sana tumbo na maumivu yakiwa yanahama sehemu mbalimbali za tumbo wakati mwingine kifuani, kwenye, mbavu na hata kiuno na nyonga. Nimetumia madawa mbalimbali sipati nafuu.

Nimeshapima magonjwa kama yote. Nimejaza mafile ya makaratasi ya hospital. Natibu vidonda visivyopona. Sina raha nimepoteza ufanisi katika uchakalikaji wa kusaka kipato. Sina raha napata riziki si haba ila siifurahi. Sili ninachokitamani.

Nimeshafanya Endoscope 3 (mpira wenye kamera tumboni) zote zinaonyesha nina vidonda lakini nakunywa dawa siponi. Hii ya tatu nimefanya majibu yametoka baada ya week 3.Dokta kaniandika madozi mengine ila anipi ufafanuzi vizuri kama niko kwenye hali gani.

Niko stage gani? Ananiambia ni michubuko ya kawaida tu nitapona. kweli? mwaka wa tano mnanipa moyo tu? Aisee hata sielewi, nataka ukweli. Picha zinanishangaza nazidi pata wasiwasi zaidi. Na nimechoka kunywa dawa za hospital zinaniongezea maumivu hata sijui nifanyaje.

Tafadhali mtaalam yeyote ama aliyepitia changamoto kama zangu naomba msaada wako wa mali. Nishauri nifanyaje maana nilisikia mpaka mkojo wa asubuhi inaponya. Nilikunywa na sikupona.

Naambatanisha na majibu ya hospital pamoja na picha (OGD). Pia naomba kufahamu kwanini hii picha hapa chini ina vidude vyeusi ni alama ya vidonda kupona au ndio nazidi kulika.

Asanteni.

View attachment 1536980

UFAFANUZI WA KITAALAMU KUHUSU TATIZO LA VIDONDA VYA TUMBO
Vidonda vya tumbo ni nini?
Vidonda vya tumbo ni matokeo ya kuharibika kwa uteute wa ndani ya ukuta wa tumbo la Chakula au ndani ya utumbo mdogo wa Chakula na matokeo yake ni ukuta wa tumbo kugusana na tindikali iliyoko tumboni ambayo ni kali sana kama maji ya betri.

Vidonda vya tumbo husababishwa na maambukizi ya bacteria waitwao HELICOBACTER PYLORI, aidha matumizi ya baadhi ya dawa za kutuliza maumivu za jamii ya Non_steroids anti inflammatory drugs kama vile ASPIRIN /DICLOFENAC huweza kusababisha uwezekano wa kupata ugonjwa huu.

Vidonda vya tumbo vinaweza kujitokeza katika utumbo mdogo na katika tumbo la Chakula na pia ni Mara chache huweza kujitokeza katika koo la Chakula ambapo hapakukusudiwa kustahimili tindikali ya tumbo.


AINA ZA VIDONDA VYA TUMBO (PEPTIC ULCERS DISEASE)
Kuna aina nyingi za vidonda vya tumbo navyo ni
(a) vidonda vinavyotokea katika mfumo wa Chakula yani tumboni
b) vidonda vinavyotokea katika utumbo mdogo
(c) vidonda vinavyotokea katika koo /koromeo la Chakula

HATUA KUU ZA VIDONDA VYA TUMBO
ni vizuri kufaham kwamba huu ugonjwa una hatua nne ambazo ni muhimu

(1)HATUA YA KWANZA ~hatua ya kwanza ya huu ugonjwa ni ule uvimbe sugu unaotokea sehem ya ndan ya tumbo.

(2)HATUA YA PILI~hapa vijidonda hujitokeza sehemu zenye uvimbe na taratibu vidonda hvyo huongezeka na kua vikubwa katika hatua hii mgonjwa hupatwa na maumivu makali ya tumbo yanayodumu kwa muda mrefu yakiambatana na kiungulia, tumbo kujaa gesi wakati wote, kukosa hamu ya kula, choo kuwa kigumu au kukosa choo kwa muda mrefu.

Hata hivyo Hali hii ya kukosa choo kwa muda mrefu (CHRONIC DYSPEPSIA) yani kushindwa kufanya Kazi kwa mfumo wa mmeng'enyo wa Chakula kutokana na tindikali nyingi inayozalishwa tumboni huingia Kwenye mzunguko wa dam hivyo mgonjwa hujisikia uchovu na kizunguzungu cha Mara kwa Mara katika hatua hii tindikali husababisha magonjwa ya ini na Figo kwa kuwa tayar iko katika mfumo mzima wa damu.

(3) HATUA YA TATU ~hii ni hatua ambayo ni ya hatari kwasababu vidonda vikubwa hupasua mishipa yote midogomidogo ya damu na kusababisha damu kuvia tumbon na kubadilisha rangi ya choo kuwa cyo ya kawaida, pia damu nyingi ikivujia tumboni mgonjwa hutapika na kuharisha damu Hali hii husababisha mgonjwa kuishiwa damu Mara kwa Mara, maumivu makali ya tumbo,hupata Homa, maumivu ya viungo na kukosa hamu ya kula.

(4)HATUA YA NNE ~katika hatua saratani ya utumbo inahusika kwani katika hatua hii vidonda vya tumbo hutengeneza tundu katika tumbo au utumbo mdogo na kusababisha kuoza kwa viungo vya ndani na matokeo yake ni saratani ya utumbo.

VISABABISHI/ VIHATARISHI VYA VIDONDA VYA TUMBO
visababishi vya ugonjwa huu vipo vingi sana hivyo yatupasa kuviepuka ili kujiepusha na huu ugonjwa.zifuatazo ni visababishi vya ugonjwa huu
i. Utumiaji wa madawa ya kuondoa maumivu kwa muda mrefu
ii.mawazo na huzuni kwa muda mrefu
iii.kutokuwa na muda maalum wa kula
iv.Utumiaji wa pombe uliopitiliza
v. Utumiaji wa madawa ya kulevya nk

DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO
~Dalili za vidonda vya tumbo ni nyingi ila sio wote wanaopata Dalili hizi Wana vidonda vya tumbo
i. maumivu makali au kiungulia maeneo ya chembe moyo (EPIGASTIC PAINS)
ii. kuvimbiwa au tumbo kujaa gesi Hali hii huweza kuendana na kucheua na kujamba Mara kwa Mara
ii. kutapika damu
iii. mtu mwenye vidonda vya tumbo (gastric ULCERS) hupata maumivu makali pindi anapokula au amalizapo kula
iv. mtu mwenye vidonda vya tumbo katika utumbo mdogo (duodenal ulcers) hupata maumivu makali pindi anapokua na njaa.
v. kupoteza hamu ya kula
vi. kupata haja kubwa yenye rangi damu Tena chenye harufu mbaya
vii. kupungua uzito

MATIBABU NA JINSI YA KUJIKINGA NA UGONJWA HUU
~matibabu ya ugonjwa huu yanapatikana vizuri nchini mwetu ila tatzo ni tiba yenyew kutokua na wataalamu wa kutosha wa kutibu chanzo cha tatizo na kumaliza tatizo pasipo kuleta matatzo mengine kutokana na matibabu yenyewe kuhusisha mfumo wa dawa za kemikal ambazo zina madhara kwa mhusika na pia , hivyo tiba bora kwa vidonda vya tumbo ni mlo kamili na dawa zisizo na kemikal pia tunapaswa kuepuka baadhi ya vyakula na kuzingatia masharti.

MAMBO YA KUFANYA KWA MWENYE VIDONDA VYA TUMBO
i. epuka kula vyakula vyenye viungo vingi kama vile pilau
ii. epuka kutumia pombe
iii. epuka ulaji wa vyakula vyenye sukari nyingi
iv. kula Chakula kidogo kwa muda maalum
v. kula vyakula vyenye fiber yan vyakula vyenye nyuzunyuzi ambavyo ni jamii ya mbogamboga na matunda
vi. epuka unywaji wa kahawa au kinywaji chochote chenye caffeine kiepuke

BAADHI YA USHAURI NA MAONI YALIYOTOLEWA NA WADAU

---

---

---

---

---

---

---

---

---




Pia unashauriwa kusoma:
1. Ushauri kuhusu dalili hatarishi za vidonda vya tumbo - JamiiForums

2. naomba kujua dawa asili ya Vidonda vya tumbo - JamiiForums

3. Yajue haya majani ni Dawa ya vidonda vya tumbo - JamiiForums

4. Ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers Disease): Kinga, tiba na ushauri

5. Angalizo: Baadhi ya dalili za vidonda vya tumbo hufanana na dalili za magonjwa ya moyo - JamiiForums

6. Vyakula Vinavyoliwa na Mgonjwa wa Vidonda Vya Tumbo
Mungu na akupiganie upone kwa jina la Yesu!
 
huyu jamaa aliomba awe wa kwanza namtafta ili nimtumie dawa ila naona yuko kimya tu mpk sasa

So, nafas yake naigawa kwa mmoja alie serious kuhitaj tiba !

Thank you
Asante boss, nimepokea dawa imenifikia leo, nitaanza itumia Jumamosi (kwa sababu zangu mwenyewe kiofisi, japo ningependa kuanza leo, thereafter nitarudisha mrejesho hapa ndani ya siku 5 hali yangu iko vipi.

Shukran sana Bob laidoo alinitumia dawa kwa basi hadi Dar. Mimi gharama niliyoingia ni ya usafiri peke yake. Dawa kanisaidia bure.

Asante mkuu.
 
Back
Top Bottom