Mtaje jina lake huyo Daktari anayetibu pumu na uwape watu Address yake usiseme maneno ya mkato tu.yupo dr anatibu pumu kama kumsukuma mlevi nina ushahidi wa watu kibao waliopona mfano mwl wangu amepona kabisa mwingine ni meja jeneral samuel kitundu
Mtaje jina lake huyo Daktari anayetibu pumu na uwape watu Address yake usiseme maneno ya mkato tu.
Dawa ya Maradhi
PUMU (ASTHMA): Haya ni maradhi ambayo husibu mapafu na kumsababisha mgonjwa apate shida ya kupumua. SABABU: Yawezekana kusababishwa na vumbi, aina ya unga au vumbi litokanalo na maua, baadhi ya vyakula, mabadiliko ya hali ya hewa, wanyama kama paka na mbwa, aina ya bacteria, kuvuta sigara, pumu ya kurithi. n.k.
DALILI: (3) Mgonjwa hupata shida ya kupumua ndani
hewa safi ya oksijeni na kupumua nje hewa chafu ya kabondayoksaidi.
(4) Wakati mwingine utamsikia mgonjwa akipumua anatoa sauti isiyokua ya kawaida (wheezing sound) hii ni kwa sababu ya wingi wa makohozi (mafua) yaliyosongamana ndani ya mapafu na kuzuia nafasi ya hewa. Mgonjwa hupata shida anapokua ndani ya chumba ambacho ndani yake hakuna hewa ya kutosha kwa sababu ya udogo au upungufu wa madirisha. Mgonjwa hupata nafuu baada ya kutoa na kutema makohozi na kukaa sehemu yenye hewa safi.
(5) Kukohoa au kikohozi cha muda mrefu. TIBA: Kanuni ya kwanza: Chukua bakuli yenye maji ya moto kisha udondoshee ndani yake matone kadhaa ya mafuta ya habatsoda. Kaa juu ya kiti halafu ujifunike shuka na usogeze bakuli lenye maji ya moto na
habat soda ili upate mvuke wake. Tiba hii inaitwa Aromatherapy. Baada ya kufanya hivyo jipake mafuta ya habat soda mgongoni na kifuani halafu unywe mafuta ya habat soda matone matatu. Tumia kanuni hii kutwa mara mbili asubuhi na
jioni kwa muda wa wiki mbili. Kanuni ya pili: Chukua asali nusu lita, juisi ya kitunguu saumu mili lita 200, unga wa habat soda vijiko vinne vikubwa, unga wa tangawizi vijiko viwili vikubwa, unga wa mdalasini kijiko kimoja kikubwa. Vyote changanya pamoja. Kula vijiko viwili vikubwa kutwa mara tatu.
Kama wewe Huamini Dawa za Kienyeji Nenda hospitali watakupatia Dawa ya Pumu usiulize hapa Dawa ya Pumu wakati hospitali zipo nenda ukatibiwe Hospitalini... chilubiKama ipo ata namie naitaka! Ila situmii za kienyeji coz i dont trust them
Kama wewe Huamini Dawa za Kienyeji Nenda hospitali watakupatia Dawa ya Pumu usiulize hapa Dawa ya Pumu wakati hospitali zipo nenda ukatibiwe Hospitalini... chilubi
Mkuu. TELO wewe endelea tu kutumia hiyo Asali itazidi kukusaidia nakupa na faida ya hiyo Asali kila siku unapo amka kabla kula kitu chemchsamaji ya uvuguvugu glasi moja kisha tiya ndani yake kijiko kimoja kikubwa cha Asali kunywa kila siku asubuhi kabla hujala kitu itakusaidia kuondowa maradhi hayo ya Pumu tumia kila siku katika Maisha yako muache huyo chilubi na ujinga wake anazarau Dawa za mitishamba.Mzizimkavu,
Vema,yeye kama haamini anategemea kupona kwa dawa zipi? kama ni za Hospitali si aende huko? Aache kabisa kutuchanganya wakati dawa za asili ndiyo zinatutibu.
Mimi binafsi nina matatizo ya seasonal Athma na ilikuwa ikinisumbua sana,LKN sasa ni miezi 8 hivi na hata Athma haijawahi kunisumbua sasa. Na dawa pekee ninayotumia ni ASALI. Ninatumia asali kwenye chai kila siku na pia kila siku usiku kabla ya kulala nakula kijiko 1 cha asali.Na kwasababu kwa kipindi chote hiki na hata dawa nilizopewa Aghakan sijatumia yapata miezi 8 sasa. Hivyo, naamini dawa za asili zinasaidia. Mimi naamini ASALI ndiyo imekuwa ikinisaidia kwa kipindi chote hiki. Na kuhusu ASALI nilipata humu humu JF, hivyo kama kuna mtu ambaye haamini atuache sisi wengine tunaoamini na tayari nimeona matunda ya dawa za asili na JF:
NB: Mzizimkavu na wengineo, kamwe msikatishwe tamaa na wale wasioamini, kwani tulio wengi tunaheshimu sana michango yenu na Mungu azidi kuwabiriki.
astma huwa haiponi? cha muhimu ni kuepuka vitu vinavyoweza kuiprecipitate ikaanza kama vile vumbi na poleni(chavuo) dawa nyingi za asili kama kujifukiza au kunusa majani ya mkaratusi inasaidia. lakini kwa mtoa mada kukohoa haiconclude kwamba ni astmaKuna majani yanaitwa Athma weeds, au Euphorbia hirta, au mziwaziwa, google utaona picha yake then utaumbua kwani ni very common weed!
Kausha pamoja na majani ya mpapai; sokota then smoke. Ukishindwa basi choma chumbani unapolala!
Inarelieve, sina uhakika inaponya kabisa!